Rijali jandoni
JF-Expert Member
- Apr 5, 2018
- 1,936
- 1,972
Habari za jioni wana jamii leo nimekaa na kuwaza kuhusu nchi yetu ya Tanzania kwa kina na kwa upana sikuwa na budi bali kuandika haya mambo kwa sisi watanzania wote
Tanzania ni nchi ambayo imekaa vizuri kijiografia yaani tumezungukwa na nchi nane tunaweza sema tisa tukiweka na visiwa vya Comoros. Strategically Tanzania ni nchi nzuri kiuwekezaji na kiuchumi kwa namna ya kuzungukwa na nchi karibia tisa.
Tukija swala la pili Tanzania ni lango kuelekea kusini mwa afrika nchi kama maalawi,zambia na hata congo, hapa tunaweza jumuisha Burudi na hata Rwanda kwa namna fulani.
Tukiongezea kwenye idadi ya watu kwa ukanda huu wa kusini mwa afrika ni kati ya nchi yenye idadi kubwa ya watu pamoja na wanyama.
Tanzania ukiachana na idadi ya watu, ina eneo la mraba mkubwa sana zaidi ya nchi zilizo pakana nazo ukiachana na Congo upande wa magharibi.
Kwa namna hiyo kama taifa inawezekanaje bado tukawa na hali ya wasiwasi wa kichumi na ya kufikirisha na ukiongeza kwa rasilimali ni nchi naweza sema pekee duniani imezungukwa na maji katika kila pande kaskazini mashariki ,magharibi pamoja na kusini.
Kwa namna ya kawaida tunaweza sema ni nchi ya asali na maziwa ambayo kila binadamu pamoja na kiongozi huenda ana imezea mate japo sisi bado tuna wasiwasi wa namna tutakavyo amka kesho yake, hii ni kwa majority japo natambua wapo wasio na wasi wasi juu ya kesho yao, kwenye suala la kiuchumi.
Kama taifa, viongozi wake Ndugu Raisi, Makamu, Spika, Mawaziri, Wabunge, pamoja na viongozi wote kwanini tusiwe na sera za muda mrefu (miaka 10 - 20) au mfupi (miaka 2 mpaka 5) za kiuchumi kwa taifa kwenye mambo tofauti?. Juhudi za viongozi wote mlijitahidi kwenye kuitangaza nchi hasa kwenye utalii na mengine mengi lakini kuna mambo tunaweza yasahau madogo ama hata makubwa ambayo yanahitaji jicho makini na la tofauti ili kuendeleza taifa letu la Tanzania na kuweka ahuweni na imani kwa wana wa Tanzania hasa swala la uchumi :-
1. Itungwe sera ya kuwekeza kwenye miundo mbinu ya nchi kuanzia barabara, maji, umeme majengo ya shule na biashara.
Kama taifa na viongozi wake wanaweza kuweka sera ya miaka mitatu sababu tumesha jitangaza vya kutosha na kuwekeza hela kwenye utalii na mambo mengine. Je tunaweza jaribu haya:-
(i) Tujitahidi kuanza sera ya maji kwenye kila kijiji fedha zitakazo pangwa kwa ajili ya matangazo basi tuanze la maji na upatikanaji wake, kutokana na matumizi yake kuwa muhimu kwenye shughuli za kila siku. Hii tuipe hata sera ya miaka miwili itategemea na serikali itapanga bajeti kiasi gani kwa sababu kasi ya mradi nadhani huwa inategemea fungu lililowekwa pamoja na ufanisi wa watendaji wa huo mradi lakini muda utakuwa muhimu zaidi kwenye haya mambo.
(ii) Iwepo sera ya kusambaza umeme kila kijiji kila mtaa hii imeshafanyika huenda sehemu kubwa ya nchi inabidi tuupeleke kote ila hapa inatakiwa uwepo uangalifu na nyumba inayo fungiwa umeme ili kukwepa gharama za uharibifu pale ambapo majanga yatatokea hata madogo kama upepo na ukaharibu nyumba isio imara, kwasababu tunaelewa hali zetu watanzania vidole vyote havilingani na ndivyo hivyo kwenye swala la ujenzi pia kila nyumba itajengwa kwa ubora kutokana na kipato cha mtu. Hii sera ya umeme inaweza kuja baada ya maji kwa sababu uwekezaji wa bomba za maji huwa zina husisha uchimbaji wa mitaro mikubwa.
(iii) Kwenye sera ya tatu ni ujenzi wa barabara tujitahidi kila eneo ambalo linatumika kama chanzo kikubwa cha mapato basi barabara iweze kupita hapo ya kiwango bora cha lami, tujitahidi kupeleka hizi barabara mashambani, karibia na migodi, na hata mipakani mwa mbuga za wanyama bila kusahau vijijini kwa wakulima hii itasaidia usafirishaji wa hizi rasilimali zote pamoja na watu kufika kwenye maeneo hayo kwa usalama, uharaka na bila shida yoyote na hata mboga mboga pamoja nafaka zita safirishwa kwa muda mfupi kuliko sasa.
Kwa sababu kwenye uchumi wowote ili ukuwe tunatakiwa tujitahidi kupunguza muda wa usafirishaji wa rasilimali ama utengenezaji wa vitu kwa namna hiyo tutaifanya Tanzania kuwa nchi ambayo iko makini na haraka kwenye sekta na swala la uchukuzi.
(iv) Ya nne itashangaza lakini itasaidia tuwekeze kwenye ujenzi wa shule vyuo vikubwa hospitali za hadhi ya juu kwenye kutibu magonjwa na hata kuwekeza kwenye tafiti za kidunia sababu hakuna nchi ilio endelea kwa kushabikia mpira miziki na mengine kwa kiwango kinachozidi utafiti yaani researches, nchi zinazo endelea ni kutokana na sera nzuri za kwenye utafiti either science, uchumi na siasa tusome duniani nchi nyingine zina fanya nini na sisi tunaweza changia nini hii itaweza vutia wana zuoni wengi kuja Tanzania na kusoma mfano tunaona nchi ya afrika kusini ukiachana na miundombinu ila watu wengi wanatamani pia kwenda kusoma huko ukienda ulaya na Asia ndio usiseme, kila mwana wa Afrika anapatamani.
@ Kwenye sera ya ujenzi wa shule yaani vyuo vikubwa tujitahidi kila mkoa uwe na chuo chenye hadhi kama ya chuo kikuu dar es salaam ama zaidi hii itachangia pia uinuaji wa uchumi kwenye mikoa iliokuwa haionekani na pia itafanya wanafunzi wanaomaliza mikoa husika kusoma vyuo vikuu na vikubwa kwa kila mkoa ambao atakuwepo na wengine wanaweza pia kuomba nafasi ya kusoma kwenye hivyo vyuo lakini la muhimu hapa itaamsha shughuli za kiuchumi kwa kila mkoa wa Tanganyika na Zanzibar.
(b) Na kwenye hospitali kufanyike vivyo hivyo kwa sasa tunaweza anza na mikoa yenye idadi nyingi ya watu na ipo angalau vizuri kiuchumi kuendeleza hospitali zao mkoa ziwe kama muhimbili au kujenga hospitali kubwa za hadhi ya muhimbili au zaidi zenye vifaa na wataalamu wazuri ili kusaidia jamii za eneo husika kwenye nyanja tofauti. Hii itafanya nchi kuto endelea upande mmoja tuu tutajijuta kila mkoa wa Tanzania kuna fursa kutokana na upatikanaji wa vitu muhimu
(c) Kujijenga imara na kiteknolojia zaidi kwenye swala la ulinzi cha kwanza imani irudushwe kwa wananchi juu ya vyombo vyetu vya usalama, pili inawezekana kila mkoa kukawa na mfumo wa vinasa picha yaani kamera za matukio ambazo zita unganishwa na vituo vidofompaka vikubwa vya kila kata wilaya, mkoa na hata nchi kwa namna hii nawahakikishia kama suala la watu kwenda Serengeti, Zanzibar Udizungwa Kilimanjaro wata miminika mpaka tuweke sheria kali kama baadhi ya nchi kama China
Sababu tutakuwa tuko vizuri sehemu zote muhimu hili la ulinzi naimani wenye nafasi wanaweza liboresha zaidi na tuka aminika sababu hili ni kati ya changamoto kwa nchi zetu za afrika Tanzania tukitatua basi tutakuwa na ugeni usiokuwa na idadi kati ya 6Million hata 10Million kwa mwaka na itashangaza.
Kwa namna hii nadhani tunaweza peleka taifa letu mbele zaidi ila inahitaji watu wenye upendo wa kweli kwa nchi yetu. Tukumbuke tunaweza tukala kila kitu na kuiporoka Tanzania na hata kuona watu wake hawastahili mazuri ama wana stahili lakini sio kwa kiwango kikubwa, ila usije ukasahau hii ardhi ndio itakayo kupokea siku ikikuhitaji utajisikiaje umefanya mambo ambayo hukuweza kuondoka nayo wakati yalikuwa kwenye uwezo wako tuipende Tanzania tuipende afrika naelewa ni ngumu kwa sera zote kufanyika kutokana na vikwazo vingi vitakavyoweza kuinuka lakini tujitahidi hakuna Tanzania nyingine zaidi ya hii tunaweza kimbilia ulaya kula na kukaa ila kama ulitokea kwenye uso wa Tanzania basi kumbuka kuna siku utataka ukurudishe ardhini kwake utakumbukwa kwa lipi juubya taifa lako?