Kwa sera za namna hii, Tanzania inaweza badilisha hali yake ya kiuchumi na kuwa taifa imara ukanda wa Kusini mwa Afrika ama inahtaji mageuzi zaidi?

Sipingi haya yote unayo eleza humu; lakini una ifanya mada yako kuwa ngumu sana kwa kuisambaza namna unavyo fanya wewe. Yaani imeenea kila mahali; ni vigumu kwa anaye kusoma ku'focus' kwenye nini hasa kinatakiwa kipewe uzito zaidi na kwa wakati gani.

Kama nilivyo eleza, hhi ni moja ya mada nzito sana, ambayo kama tungekuwa makini, hii ndiyo mada ambayo ingekuwa juu zaidi katika majadiliano humu. Lakini angalia ilivyo hadi sasa.

Kuepuka na mimi nisiwe nazungumza mambo kijumla jumla; hapo juu nilisema tu kwa kifupi; kuhusu "UMUHIMU WA MTAJI WA WATU" (Human Capital).
Hakuna nchi inayo weza kuendelea kama mtaji wake huu muhimu upo shaghalabaghala kama ilivyo hapa kwetu. Na si hivyo tu, ili kuupanga vizuri mtaji huo ni lazima pawepo na sera mahsusi za kuuwezesha, yaani "UONGOZI" unao elewa unafanya nini (Uongozi Bora).
Huwezi kuwa na uongozi uso kuwa na dira yoyote ya maana juu ya nchi, halafu utegemee maendeleo ndani ya nchi hiyo

Na haya ya "Geographical Location" kama ulivyo yaweka, na mali asili zote zilizomo ndani ya nchi hii, kama ardhi, madini, utalii, n.k.; yote haya ni sehemu ya 'ARDHI', kama alivyo yaainisha Mwalimu Nyerere katika msemo wake ule mashuhuri:"Ili Tuendelee Tunahitaji Mambo makuu Matatu": Uongozi Bora; Watu, na Ardhi...

Haya yote ya Teknolojia, viwanda, n.k.; yote yanaingia katika moja wapo ya hizo nguzo tatu.

Sasa basi: hapa kwetu sasa hivi ingefaa sana viongozi wetu wakarudi kwenye misingi ya kuwawezesha vijana wetu hawa sasa hivi kupata elimu ya kisasa kabisa inayo weza kupatikana sehemu yoyote duniani, ili waweze kuwa na ujuzi wa haya ya Teknolojia tunayo ihitaji sasa hivi na mambo mengine muhimu. Elimu isipuuzwe hata kidogo.

Uongozi wetu tulio nao sasa sioni ni jinsi gani unaweza kuliinua taifa hili, hata ukiwapa miaka mia moja ijayo; Tanzania haitakuwa mbali sana na ilivyo Haiti.

Swala la Korea Kusini bado hujalipa jibu sahihi, ni hayo hayo ya kurashia tu kama ilivyo kawaida yetu.
 
Wow, well narrated, nimependa ulivyo shuka kuanzia kichwa nini la msingi na hitimisho.

Nitalifanyia kazi kuhusu mpangilio na kuhusu south korea pia nimeeleza japo nimejumuisha kwa ujumla na kuto chambua kitu kimoja baada ya kingine.

Kuhusu swala la wasomi na wenye ujuzi wa mambo baadhi ya kulisaidia taifa nilishawahi lifikisha sehemu muitikio ulikuwepo tatizo ni namna ya kuliwasilisha kutokana na mambo yanavyo enda kwa sasa watanzania tukiweza muda kwenye teknolojia na maendeleo waliopewa dhamana wangeweza onesha zaidi kwenye hayo maswala.

Tatizo ni kwamba nguvu yetu itakapo lalia kiongozi hana budi nae kuonesha nini watu wanataka waone lakini naimani itafika wakati watu watafunguka ila itakuwa muda umeshaenda japo tukiwahi tunaweza kuelekezea upepo huko kwenye mapinduzi ya kiuchumi.
 
Ardhi tunawauzia Waarabu, aiseee Tanzania ina laaana niamini tafadhali
 
Mada nzuri Sana hii, kwa kuongeza at least kwa upande Wangu, hasa hapo kwenye Human capital, nashauri shule zetu zibadilishwe kabisa (total reform) kutoka kwenye ufaulu Hadi kwenye skills development!

Wakati nasoma primary, I think darasa la TATU au la nne, tayari nilikua na tuta la spinach, mchicha n.k. Kaka Zangu walikua na mabanda ya sungura, Kaka Yangu mmojawapo alikuja kutengeneza Banda zuri Sana la Kuku!

Tulikua na mafundi -technicians wazuri Sana WA kidato cha nne..... Leo hamna kitu
 
Ardhi tunawauzia Waarabu, aiseee Tanzania ina laaana niamini tafadhali
Kama iko hivi basi ni swala la kutulia nadhani, kinacho kosekana hapa waliopewa dhamana wana shindwa kaa chini na wenye maarifa ya hivyo vitu na kuangalia namna mambo yalivyo kwa kina na umbali

Aidha kwa namna nyingine ya kipato chetu kuwa cha kusuasua basi hatuna namna zaidi ykufanya hivyo ili kuendeleza mambo mengine ya nchi inabidi hilo lifanyike, sababu wanaweza kuikumbatia na haizalishi wala kuleta kitu, wanaona si mara mia waikodishe ili iingize chochote kitu?

Lakini hapa inabidi iwepo dira ya muda mrefu kwa taifa ili yasijirudie
 
Jiandae kuchukua form ya ubunge, uko vizur
 
Ni kweli kabisa tatizo nimeandika kwa mtindo ambao una hitaji mtu anae penda kusoma na awe na back up ya nini kinacho endelea na matamanio ya wapi tunapohitaji kuwepo.

Pamoja na uwezo wa kuhoji na kujenga hoja ambayo inaweza kuwa na suluhisho.

Naamini hamtaichoka kuisoma na kutoa ufafanuzi utakao saidia Tanzania yetu
 
Lakini hapa inabidi iwepo dira ya muda mrefu kwa taifa ili yasijirudie
Tuondoe madaraka kutoka kwa MTU, kiongozi asiwe na final say kwenye mustakabali wa maisha ya watu na Wajukuu zetu. Mfano wa Ngorongoro, yaliyotokea Ngorongoro "yamemalizwa" kwa salam kutoka kwa MTU mmoja "aliyetuma" wawakilishi wake.

Tanzania ni mbingu inayoishi Jehanam
 
Sawa buana Rijali Jandoni
 
Mchango Wangu mwingine ni Ujenzi madhubuti WA miundombinu, tukiweza kuimarisha miundombinu hasa kwenye mazingira ambayo ni potential Zaidi tutakua tumepunguza gharama.

Kwa mfano, barabara ya Uvinza (Kigoma) kupitia Mpanda( Katavi) Hadi Sumbawanga (Rukwa) kama ingepewa kipaumbele basi Tanzania kwa ukanda ule ingeweza kulisha vizuri sana Nchi za Rwanda, Burundi, Zambia na Congo bila Shaka LAKINI huwezi kuamini ninavyoandika hapa Ujenzi umesimama kwakua mkandarasi hajalipwa, ule WA kibaoni nao pia unasuasua Hadi sasa hakuna kitu. Unajiuliza hivi kipaumbele cha Nchi Yao yetu ni nini hasa??
 
Jiandae kuchukua form ya ubunge, uko vizur
Hahahaha wakati wa MUNGU ukifika Attack, kwa upande niliopo napenda uwepo mfumo mzuri ambao unaweza thamini maslahi mapana ya Taifa, kwa namna hiyo hautokuwa na namna zaidi ya kuifanya nchi ifike mbele japo isiwe publicity ila sera ziwe nzito na za chini kwa chini lakini impact waone waliopo ndani ya nchi

Sababu haya mambo ya kujinasua yanahitaji mkakati madhubuti.
Wapo wanaofaidika kutokana na matatizo ya watu umaskini, ujinga, na vita sasa ukiamsha jamii kwa upande mwingine umeamsha hasira, na hii inatakiwa kukaa mezani kama usuluhisho utapatikana kwa namna hiyo basi itabidi kazi ianzee na mifumo ya ndani ilindane kwa maslahi ya taifa
 
Nadhani tatizo sio sera maana sera nzuri zipo ila shida ni vipaombele.Kipi kianze na kipi kifuate na Kwa Ukubwa gani na maamuzi ya uthubutu.

Pili shida kubwa nyingine ni kukosa strategic thinking kiasi kwamba tunaenda enda tuu bila malengo yanayopimika Wala kujipima.
 
Basi hili pia ni changamoto kama lina fanyika kwa namna, nadhanj kuna sehemu inatakiwa ikaliwe chini ili nadala ya mtu mmoja kubebeshwa kila kitu inatakiwa chain nzima ijue nini cha kufanga kabla taarifa haijafika juu kwenye kichwa

Nadhani pia wanao toa maamuzi juu ya uwekaji wa miradi wanatambua na kulichambua jambo kabla halijatokea mazingira yapoje na baada ya kutangazwa yatakuaje na likisha fanyika hali itakuwa kwa namna gani.

Nadhani inahitajika iwe kwa namna hiyo na naimani wanatekeleza kwa mtindo huo kinyume na hapo itaonekana hata kwa kila jema wenye dhamana wakipanga kufanya basi wananchi wataona kana kwamba kuna baya juu yao na hili huenda lina changiwa na namna maamuzi yanapo fanywa hata kama ni jambo jema kwa uchumi lakini lazima liangaliwe lina madhara gani duniani hakuna kitu kinacho fanya kazi kwa ufanisi wa asilimia 100% lazima kuna asilimia za madhara kutokana na uendeshwaji wa jambo fulani.

Kwa namna hiyo lazima mikakati iwepo kabla ya kulisema na baada ili kuona muitikio

Hakuna kitu kinaweza muweka mwenye dhamana kwenye mawazo kama kuwa na nia nzuri lakini wananchi wasikuelewe sababu ya maswaibu yaliyo wakuta kipindi cha nyuma ni ngumu kuwaeleza kwamba hili la sasa ni kweli sababu wana makovu ambayo wanaogopa kutoneshwa
 
Naimani wanaliona, kwa sasa nchi inahitaji dira inayo eleweka na malengo makubwa, kuna baadhi ya nchi wanakaa vikao vya kila baada ya muda kuweka malengo makubwa na madogo ya nchi, nadhani na kwetu inabidi liwepo hili.

Tufike wakati tetesi na habari za aliepewa dhamana kula hela ya uma isiwepo hiyo inakata morali na imani ya wananchi kwenye mfumo mzima.

Kama hapo umeshaona kazi haiendelei fikra lazima zije hela imeliwa ama hazipo na hii inapelekea haylta mwananchi kutokuwa mstari wa mbele kwenye kuinua uchumi wa nchi na kutojali nchi yake
 
🤔🤔🤔
Tz tutajua kula na sikutafuta,alieonyesha njia ni jiwe pekee ndio maana uchumi ulikua kwa haraka sana , baada ya mola kumchukua nchi imerudi kule alikosema huku hatufiki,walimuita mvunja haki za binadamu kwakua upigaji ulibanwa but sasa slogani yetu ni Mkalitazame na hili
 
Kabisa hili la kukosa la kukosa mpangilio wa kipi kianze kipi kifuate tuhitimishe lipi na tuanze na lipi awamu ya pili ndioa tatizo.

Na kwenye kipaombele ni tatizo kubwa sana tunatoa muda mwingi kwenye mambo yasio na tija kubwa kwa taifa hili pia linatokana na uelewa kwa upande wa elimu ya wananchi hapa sio elimu ya madegree hapana elimu ya mambo na namna gani maisha yanatakiwa yawe bora kwa watu.

Na kuhusu swala la mkakati yaani strategy (strategic plan) ni zito sababu tukiwa makini hizi shida za maji umeme barabara ni mambo yanaongelewa bungeni tokea 2004 tuiweke hii range lakini ni zaidi ilitakiwa kwa mwaka 2024 miaka ishirinj baadae tumeshatoka huko.

Tupo kwenye hoja ya namna gantaifa a linaweza kujilinda kiteknolojia kama hali yakidunia ikiwa mbaya Zaidi ni kwa namna gani tunaweza ongeza ufanisi wa viwanda vya ndani ili kukabiliana na ushindani wa viwanda vya nnje.

That's how it should be hahahaha mpaka nahitimisha kwa kingereza

Taifa linahitaji watu wenye nia iliyo nyooka wenye upendo wa kweli na weledi wa kujua tuna takiwa tuwe wapi.
 
Nakuonea huruma unaandika mambo mazito sana yanayotaka watu wenye uwezo kuyapangia mikakati.

Hao vijana waliopo hapo leo wanaotakiwa kushika nchi kesho the future is not just bleak but darker.

Uhalisia ni kwamba hawana uwezo kabisa.

Mfano mdogo nilikuwa sielewi tatizo la extent ya foreign exchange ukifanya biashara Tanzania as an importer kupata.

Salaleh kupata hela ni shida, sasa waziri mwenyewe anakwambia sio shida. Hila ni tatizo kubwa sana kwa sasa.

Kwa importers wenye akili timamu faida yao lazima waidai kwa malipo ya dollar ili ku-mitigate inflation risk ya currency devaluation.

Maana ukipanga bei na mtu ya kiasi fulani biashara ya million 50 tu hadi akupatie hiyo bila ya kukubaliana fixed rate importer una loose. Hiyo hela kwake kuikusanya kupata dollar, pound au euro ni mtihani.

Hali ya foreign Tanzania ni mbaya sana, mimi mwenyewe nimejionea. Sijui waagizaji wa mafuta na large quantities za essential commodities wanapitia mtihani gani.

Halafu hapo hapo unaona Irene uwoya anaringishia $10000 ambazo hana shida nazo za biashara.

Huyo mama na serikali ya watu wasiojali sidhani kama wanaelewa ukubwa wa tatizo, yaani hali ni mbaya sana kwenye foreign. Halafu waziri analeta siasa.

Foreign exchange Tanzania hali ni mbaya.

Hiyo mipango yako mingine ya akili mleta mada kwa maendeleo ya taifa sahau sio kwa watu ni zero.

Pole, muhimu ni kuwakumbusha tu lakini kwa mapoyoyo ya kufukia hizo hazma zako sahau.

Aisee mungu anajuwa hawa waagizaji wa essential commodities hela wanatoa wapi.

Hali ni mbaya sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…