Kwa sisi wanaume tuliooa, ukiacha tendo la ndoa, mke wako anakusaidia kwa lipi?

Kwa sisi wanaume tuliooa, ukiacha tendo la ndoa, mke wako anakusaidia kwa lipi?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Wengi tulikuwa tunatamani kuoa, tukiamini baada ya kuoa maisha yatakuwa full starehe na hakutakuwa na migogoro.

Wapo waliofanikiwa kwa kupata watu sahihi, mpaka wakikaribia kuzeeka sura zao zinakuwa zinafanana.

Pia wapo waliokosa watu sahihi, na kujikuta wameingia kwenye ndoa yenye changamoto; ambao ukikutana nao njiani, sura zao zimekuwa nzito na zimejaa majukumu mazito na ghadhabu za kuingia kwenye ndoa.

Na wengi tunaoteseka kwenye hizi ndoa ni wanaume, sema huwa tunavumilia ndio maana ata takwimu zinaonyesha wanaume wanakufa haraka kuliko wanawake.

Sasa tujiulize swali; Kwa sisi wanaume tulio oa, ukiacha tendo la ndoa, mke wako anakusaidia kwa lipi?​
 
Binafsi Mke wangu ni Msaidizi wangu kwenye mambo mengi, mathalani;

Ananisaidia kusimamia baadhi ya miradi tuliyoanzisha pamoja (Nafanya hivi Kwa kujua kwamba nitawahi kufa kabla yake, hivyo Jukumu la kulea watoto litabaki kwake).

Anasaidia malezi ya watoto wetu

Anasaidia kunipa Utulivu wa mwili na akili
 
Back
Top Bottom