Kwa style ya Uongozi wa Lissu, Heche na Mnyika, Mapandikizi CHADEMA wataaibika na kufeli vibaya sana

watapigwa sana kama burukenge na walinzi binafsi wa heche ee gentleman? :pedroP:
Mtatunga sana Bongomovie mwaka huu. Tena mchukueni kabisa Lamata awatengenezee script nzuri ila jueni tu kuwa ufedhuli wenu wote hautafanikiwa.
 
Mimi ni CCM! Na nimekuwa msiri kwa miaka mingi. Ila kwa hapa tulipofikia kama Taifa, nadhani mabadiliko hayakwepeki. Haiwezekani chama kilichomilikiwa na wafanyakazi pamoja na wakulima, leo hii kimilikiwe na kikundi cha watu wachache pekee! Tena watu wasio hata na chembe ya uadilifu na pia uzalendo kwa nchi yao.

Mwanasheria wangu binafsi na Wakili Msomi ephen_, tafadhali naomba uhakikishe simu yako iko hewani muda wote. Nimechomoa betri huku.
Mimi mwenyewe naogopa🏃
 
Mzee wangu ameniona nimevaa kofia ya chadema ananitishia kunifukuza nyumban mnishauri jaman 🤔
 
Kiundwe kitengo maalum ndani ya CHADEMA kiongozwe na John Pambalu na Mdude Nyagali ili kupambana na mapandikizi ndani ya CHADEMA kiitwe Usalama wa CHADEMA.
Hakuna haja. Nyakati zishawatupa mkono mapandikizi wote.
 
Amani iwe nanyi Wanabodi,

Kwa miaka mingi sana tangu kuanzishwa mfumo wa vyama vingi, moja ya mbinu ambayo imekuwa ikitumiwa na CHAMA CHA MAPINDUZI ili kuendelea kubaki mabarakani ni kununua Viongozi wa vyama vya Upinzani na kuwatumia kama Mapandikizi yao.

Viongozi hawa wa vyama hivi vya upinzani wamekuwa wanaajiriwa kabisa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo TISS kwa ajili ya kufanya kazi hizo za kipumbavu za kuhakikisha nchi yetu haipati Sera mbadala na Chama mbadala kitakachochukua nafasi ya CCM.

Watu hawa wamekuwa wakiwekwa kwenye payroll ya watumishi Umma na kulipwa fedha zinazotokana na kodi za Wananchi kwa ajili ya kufanya kazi hizo za kijinga na kishetani hasa kuzuia Wananchi wa Tanzania kupata maendeleo ya kweli kupitia vyama mbadala.

Kwa miaka mingi sana, CCM walitumia mbinu hii kwa CHADEMA na walifanikiwa kuweka watu wengi sana CHADEMA kwa ajili ya kuhakikisha Chama hiki hakiwi imara na kuwa mbadala kwa Watanzania. Albert Msando, Petrobas Katambi, Vicent Mashinji na Tumaini Makene ni mfano wa baadhi ya watu tu ambao waliajiriwa na mfumo kwa sababu za kisiasa hasa kuwa Mapandikizi ndani ya CHADEMA na kuhakikisha Chama hiki hakitulii na kushika Madaraka. Hawa walipotoka bado watu wengi sana waliendelea kuwa waajiriwa wa mfumo wa kishetani wa CCM ndani ya Chadema.

Kuibuka kwa Tundu Lissu na John Heche kushika madaraka ndani ya Chadema imeelezwa kuwa ni sehemu ya mkakati wa watu wachache wenye akili huko TISS ambao wameamua kuisafisha nchi yetu dhidi ya upuuzi na ufedhuli wa CCM.

Kwa bahati mbaya sana, CCM na wajinga wao wachache wanaowatumia huko TISS wanafikiri wanaweza kuwatumia mapandikizi ambao kwa sasa hawana chao CHADEMA kutokana na Uongozi wa Lissu na Heche kuleta mifarakano na mitafaruko ndani ya CHADEMA.

Mategemeo ya CCM na wajinga wao waliopo TISS ni CHADEMA kupanick na kushindwa kujikita kwenye ajenda ya Msingi ya No Reform No Election ambayo kiuhalisia imebuniwa ili kulikomboa Taifa hili na kuzikwa kabisa kutokana na ujinga na upuuzi uliosababisha na CCM ambao umeliangamizq tayari Taifa kwa sehemu kubwa sana.

Mategemeo ya CCM na wajinga wachache ni kuwatumia hawa mamluki kuleta tension na vita ya madaraka ndani ya CHADEMA ili kumfanya msajili au Mahakama waingilie kati na kuweka hawa mapandikizi kwenye Uongozi wa CHADEMA na hatimaye CCM iendelee kuifisadi hii nchi bila kukoma.

Wasichojua CCM ni kwamba CHADEMA ipo chini ya watu makini na wanaotumia akili sana kipindi hiki. Hawa Mamluki wote sio kwamba wamekaliwq kimya ila kiuhalisia hatua zote za kisheria zinavhukuliwa dhidi yao na kwa hatua zinazochukuliwa hawatakuwa na nafasi ya kushinda Mahali popote pale kwenye jicho la Sheria.

Kutokana na ubobevu uliotukuka wa Sheria wa Lissu hawa mapandikizi ambao wote sasa wanajulikana sio tu CHADEMA hadi na wananchi wengi wanapewa maonyo na barua za kujieleza huku umma ukijulishwa hatua tajwa kiasi ambacho kamwe hawawezi kuja kusema walionewq pale watakapochukuliwa hatua stahiki.

Jambo kubwa zaidi linalotokea sasa ni kwamba, Wananchi wa Tanzania sasa wameanza kupevuka kwa kasi ya kutisha kiasi cha kutopelekeshwa tena na propaganda za kijinga pamoja na siasa za uzandiki zina,ofanywa na CCM na Mapandikizi wao.

Mfano mzuri wa haya ni namna umma wa Watanzania ulivyosema wazi kuhusu kutumiwa kwa Katibu wa Bawacha Mkoani Njombe aliyetengeneza tukio la kupigwa na walinzi wa Heche ili kuwatoa wananchi kwenye ajenda ya maana ya No Reform No Election.

Nawaonea huruma sana CCM. Wakati haupo upande wenu. Kubalini tu kuwa hakuna marefu yasiyo na ncha na kwa sasa hakuna mbinu chafu mtakayofanya dhidi ya CHADEMA ya Lissu na Heche itakayofanikiwa.

Mungu atawaadhibu vibaya sana.
Mambo ya intel ni ya ajabu sana. Unawezahisi hao ndio watetezi na walinzi wa chama, unakuja kushtuka baada ya miaka kumi ijayo kuwa, Lissu ilikuwa ni "projekti"! Usiichezee CCM hata siku moja!
 
Nakwambiaje sema wote lakini sio aliyepigwa risasi 17 na Magufuli na kupata ulemavu wa kudumu TUNDU ANTIPAS LISSU.
 
Wataaibika vibaya sana. Siasa za utapeli na upandikizi haziwezi fanikiwa tena kwenye kizazi hiki cha sayansi na teknolojia.
Huyo dada wamtakalisha sana hapo hospitali ili kusaka kiki za kisiasa. Na uzuri cdm hawajapoteza muda kujibizana na hizo mbinu outdated. Ni juu ya ccm kupangiana zamu ya kukaa na mgonjwa wao waliyempa script ya kijinga. Wahakikishe anapona na wampe kadi ya ccm, ndani ya cdm kashtukiwa.
 
Mambo ya intel ni ya ajabu sana. Unawezahisi hao ndio watetezi na walinzi wa chama, unakuja kushtuka baada ya miaka kumi ijayo kuwa, Lissu ilikuwa ni "projekti"! Usiichezee CCM hata siku moja!
Ccm haina ujanja huo usitake kuwapa sifa wasiyokuwa nayo. Wangekuwa na ujanja huo wasingeendelea kutegemea vyombo vya dola na mbinu za kizee hivyo.
 
Amani iwe nanyi Wanabodi,

Kwa miaka mingi sana tangu kuanzishwa mfumo wa vyama vingi, moja ya mbinu ambayo imekuwa ikitumiwa na CHAMA CHA MAPINDUZI ili kuendelea kubaki mabarakani ni kununua Viongozi wa vyama vya Upinzani na kuwatumia kama Mapandikizi yao.

Viongozi hawa wa vyama hivi vya upinzani wamekuwa wanaajiriwa kabisa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo TISS kwa ajili ya kufanya kazi hizo za kipumbavu za kuhakikisha nchi yetu haipati Sera mbadala na Chama mbadala kitakachochukua nafasi ya CCM.

Watu hawa wamekuwa wakiwekwa kwenye payroll ya watumishi Umma na kulipwa fedha zinazotokana na kodi za Wananchi kwa ajili ya kufanya kazi hizo za kijinga na kishetani hasa kuzuia Wananchi wa Tanzania kupata maendeleo ya kweli kupitia vyama mbadala.

Kwa miaka mingi sana, CCM walitumia mbinu hii kwa CHADEMA na walifanikiwa kuweka watu wengi sana CHADEMA kwa ajili ya kuhakikisha Chama hiki hakiwi imara na kuwa mbadala kwa Watanzania. Albert Msando, Petrobas Katambi, Vicent Mashinji na Tumaini Makene ni mfano wa baadhi ya watu tu ambao waliajiriwa na mfumo kwa sababu za kisiasa hasa kuwa Mapandikizi ndani ya CHADEMA na kuhakikisha Chama hiki hakitulii na kushika Madaraka. Hawa walipotoka bado watu wengi sana waliendelea kuwa waajiriwa wa mfumo wa kishetani wa CCM ndani ya Chadema.

Kuibuka kwa Tundu Lissu na John Heche kushika madaraka ndani ya Chadema imeelezwa kuwa ni sehemu ya mkakati wa watu wachache wenye akili huko TISS ambao wameamua kuisafisha nchi yetu dhidi ya upuuzi na ufedhuli wa CCM.

Kwa bahati mbaya sana, CCM na wajinga wao wachache wanaowatumia huko TISS wanafikiri wanaweza kuwatumia mapandikizi ambao kwa sasa hawana chao CHADEMA kutokana na Uongozi wa Lissu na Heche kuleta mifarakano na mitafaruko ndani ya CHADEMA.

Mategemeo ya CCM na wajinga wao waliopo TISS ni CHADEMA kupanick na kushindwa kujikita kwenye ajenda ya Msingi ya No Reform No Election ambayo kiuhalisia imebuniwa ili kulikomboa Taifa hili na kuzikwa kabisa kutokana na ujinga na upuuzi uliosababisha na CCM ambao umeliangamizq tayari Taifa kwa sehemu kubwa sana.

Mategemeo ya CCM na wajinga wachache ni kuwatumia hawa mamluki kuleta tension na vita ya madaraka ndani ya CHADEMA ili kumfanya msajili au Mahakama waingilie kati na kuweka hawa mapandikizi kwenye Uongozi wa CHADEMA na hatimaye CCM iendelee kuifisadi hii nchi bila kukoma.

Wasichojua CCM ni kwamba CHADEMA ipo chini ya watu makini na wanaotumia akili sana kipindi hiki. Hawa Mamluki wote sio kwamba wamekaliwq kimya ila kiuhalisia hatua zote za kisheria zinavhukuliwa dhidi yao na kwa hatua zinazochukuliwa hawatakuwa na nafasi ya kushinda Mahali popote pale kwenye jicho la Sheria.

Kutokana na ubobevu uliotukuka wa Sheria wa Lissu hawa mapandikizi ambao wote sasa wanajulikana sio tu CHADEMA hadi na wananchi wengi wanapewa maonyo na barua za kujieleza huku umma ukijulishwa hatua tajwa kiasi ambacho kamwe hawawezi kuja kusema walionewq pale watakapochukuliwa hatua stahiki.

Jambo kubwa zaidi linalotokea sasa ni kwamba, Wananchi wa Tanzania sasa wameanza kupevuka kwa kasi ya kutisha kiasi cha kutopelekeshwa tena na propaganda za kijinga pamoja na siasa za uzandiki zina,ofanywa na CCM na Mapandikizi wao.

Mfano mzuri wa haya ni namna umma wa Watanzania ulivyosema wazi kuhusu kutumiwa kwa Katibu wa Bawacha Mkoani Njombe aliyetengeneza tukio la kupigwa na walinzi wa Heche ili kuwatoa wananchi kwenye ajenda ya maana ya No Reform No Election.

Nawaonea huruma sana CCM. Wakati haupo upande wenu. Kubalini tu kuwa hakuna marefu yasiyo na ncha na kwa sasa hakuna mbinu chafu mtakayofanya dhidi ya CHADEMA ya Lissu na Heche itakayofanikiwa.

Mungu atawaadhibu vibaya sana.
Usije ukashangaa ukasikia LISSU NA HECHE mmoja wapo ni pandikizi
 
Mimi ni CCM! Na nimekuwa msiri kwa miaka mingi. Ila kwa hapa tulipofikia kama Taifa, nadhani mabadiliko hayakwepeki. Haiwezekani chama kilichomilikiwa na wafanyakazi pamoja na wakulima, leo hii kimilikiwe na kikundi cha watu wachache pekee! Tena watu wasio hata na chembe ya uadilifu na pia uzalendo kwa nchi yao.

Mwanasheria wangu binafsi na Wakili Msomi ephen_, tafadhali naomba uhakikishe simu yako iko hewani muda wote. Nimechomoa betri huku.
Kama mm nilivyochomoa waya wa betri duuuuuuu kumbe tupo wengi
 
Kamanda unaijua ccm au unaisikia tu kinywani mwa sugu, heche na lissu?!!!
Mbona tayari mtu yupo humo na anapiga kazi vizuri tu 😄😄😄😄

It's too late. Mwezi novemba 2025 nirejeshe tena kwenye comment hii nikufafanulie...
Huyo ni mzee hataweza kufikisha zote engine atayasahau
 
Ccm haina ujanja huo usitake kuwapa sifa wasiyokuwa nayo. Wangekuwa na ujanja huo wasingeendelea kutegemea vyombo vya dola na mbinu za kizee hivyo.
CCM bado ipo madarakani kwasababu wanajua wanafanya nini na Intel yao ni ya hali ya juu kiweza kuamini na kuielewa.
 
Back
Top Bottom