Kwa style ya Uongozi wa Lissu, Heche na Mnyika, Mapandikizi CHADEMA wataaibika na kufeli vibaya sana

Amani iwe nanyi Wanabodi,

Kwa miaka mingi sana tangu kuanzishwa mfumo wa vyama vingi, moja ya mbinu ambayo imekuwa ikitumiwa na CHAMA CHA MAPINDUZI ili kuendelea kubaki mabarakani ni kununua Viongozi wa vyama vya Upinzani na kuwatumia kama Mapandikizi yao.

Viongozi hawa wa vyama hivi vya upinzani wamekuwa wanaajiriwa kabisa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo TISS kwa ajili ya kufanya kazi hizo za kipumbavu za kuhakikisha nchi yetu haipati Sera mbadala na Chama mbadala kitakachochukua nafasi ya CCM.

Watu hawa wamekuwa wakiwekwa kwenye payroll ya watumishi Umma na kulipwa fedha zinazotokana na kodi za Wananchi kwa ajili ya kufanya kazi hizo za kijinga na kishetani hasa kuzuia Wananchi wa Tanzania kupata maendeleo ya kweli kupitia vyama mbadala.

Kwa miaka mingi sana, CCM walitumia mbinu hii kwa CHADEMA na walifanikiwa kuweka watu wengi sana CHADEMA kwa ajili ya kuhakikisha Chama hiki hakiwi imara na kuwa mbadala kwa Watanzania. Albert Msando, Petrobas Katambi, Vicent Mashinji na Tumaini Makene ni mfano wa baadhi ya watu tu ambao waliajiriwa na mfumo kwa sababu za kisiasa hasa kuwa Mapandikizi ndani ya CHADEMA na kuhakikisha Chama hiki hakitulii na kushika Madaraka. Hawa walipotoka bado watu wengi sana waliendelea kuwa waajiriwa wa mfumo wa kishetani wa CCM ndani ya Chadema.

Kuibuka kwa Tundu Lissu na John Heche kushika madaraka ndani ya Chadema imeelezwa kuwa ni sehemu ya mkakati wa watu wachache wenye akili huko TISS ambao wameamua kuisafisha nchi yetu dhidi ya upuuzi na ufedhuli wa CCM.

Kwa bahati mbaya sana, CCM na wajinga wao wachache wanaowatumia huko TISS wanafikiri wanaweza kuwatumia mapandikizi ambao kwa sasa hawana chao CHADEMA kutokana na Uongozi wa Lissu na Heche kuleta mifarakano na mitafaruko ndani ya CHADEMA.

Mategemeo ya CCM na wajinga wao waliopo TISS ni CHADEMA kupanick na kushindwa kujikita kwenye ajenda ya Msingi ya No Reform No Election ambayo kiuhalisia imebuniwa ili kulikomboa Taifa hili na kuzikwa kabisa kutokana na ujinga na upuuzi uliosababisha na CCM ambao umeliangamizq tayari Taifa kwa sehemu kubwa sana.

Mategemeo ya CCM na wajinga wachache ni kuwatumia hawa mamluki kuleta tension na vita ya madaraka ndani ya CHADEMA ili kumfanya msajili au Mahakama waingilie kati na kuweka hawa mapandikizi kwenye Uongozi wa CHADEMA na hatimaye CCM iendelee kuifisadi hii nchi bila kukoma.

Wasichojua CCM ni kwamba CHADEMA ipo chini ya watu makini na wanaotumia akili sana kipindi hiki. Hawa Mamluki wote sio kwamba wamekaliwq kimya ila kiuhalisia hatua zote za kisheria zinavhukuliwa dhidi yao na kwa hatua zinazochukuliwa hawatakuwa na nafasi ya kushinda Mahali popote pale kwenye jicho la Sheria.

Kutokana na ubobevu uliotukuka wa Sheria wa Lissu hawa mapandikizi ambao wote sasa wanajulikana sio tu CHADEMA hadi na wananchi wengi wanapewa maonyo na barua za kujieleza huku umma ukijulishwa hatua tajwa kiasi ambacho kamwe hawawezi kuja kusema walionewq pale watakapochukuliwa hatua stahiki.

Jambo kubwa zaidi linalotokea sasa ni kwamba, Wananchi wa Tanzania sasa wameanza kupevuka kwa kasi ya kutisha kiasi cha kutopelekeshwa tena na propaganda za kijinga pamoja na siasa za uzandiki zina,ofanywa na CCM na Mapandikizi wao.

Mfano mzuri wa haya ni namna umma wa Watanzania ulivyosema wazi kuhusu kutumiwa kwa Katibu wa Bawacha Mkoani Njombe aliyetengeneza tukio la kupigwa na walinzi wa Heche ili kuwatoa wananchi kwenye ajenda ya maana ya No Reform No Election.

Nawaonea huruma sana CCM. Wakati haupo upande wenu. Kubalini tu kuwa hakuna marefu yasiyo na ncha na kwa sasa hakuna mbinu chafu mtakayofanya dhidi ya CHADEMA ya Lissu na Heche itakayofanikiwa.

Mungu atawaadhibu vibaya sana.
Nahisi hujuma kufanyika siku No reforms na election ikifika Kanda ya Victoria kule kwa Wenje.
 
CCM iacheni jamani, watu mnakufuru sana kuisemea kila baya kwa CCM, ila mnajisahau sana bila CCM Imara hata uhuru wa kutukana na kuisemea yote mabaya msingepata, leo mna amani, uhuru wa kuandika utakavyo, unapata mambo mengi sana ya huduma za kijamii sbb ya CCM, ila bado mnaitukana, bila CCM Imara leo tungekuwa kama DRC, au Rwanda au Burundi au CAR au Kenya au Uganda, au Somalia au Sudan au Zimbabwe au Senegal au Ivory Coast, au Libya au Egypt au Burkina Fasso etc

Hizo nchi zote za Kiafrika hamjafika, hali yao ni ngumu mno, kiuchumi na kisiasa, hali ya wananchi ni ngumu mnoooo, hakuna uhuru wa mawazo na wengine wanapigana kila siku na kuuana, amani hawana, ila sbb yote hamjui mtu una amka unashika simu yako au laptop unaanza kuitukana CCM, ebu tembeeni kidogo nchi za jirani za Afrika tu, ukirudi hapa Tanzania utanyamaza na kufunga mdomo wako.

CCM pole sana kwa kila baya unalosemwa, CCM tunaomba iendelee kuilinda nchi yetu na kuhakikisha Amani, Uhuru, Maendeleo ya watu wetu na Tunu zote za Taifa letu zinalindwa kwa hali na mali.

Mungu mbariki Rais wetu mpendwa, Mungu Ibariki Tanzania 🙏
 
Amani iwe nanyi Wanabodi,

Kwa miaka mingi sana tangu kuanzishwa mfumo wa vyama vingi, moja ya mbinu ambayo imekuwa ikitumiwa na CHAMA CHA MAPINDUZI ili kuendelea kubaki mabarakani ni kununua Viongozi wa vyama vya Upinzani na kuwatumia kama Mapandikizi yao.

Viongozi hawa wa vyama hivi vya upinzani wamekuwa wanaajiriwa kabisa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo TISS kwa ajili ya kufanya kazi hizo za kipumbavu za kuhakikisha nchi yetu haipati Sera mbadala na Chama mbadala kitakachochukua nafasi ya CCM.

Watu hawa wamekuwa wakiwekwa kwenye payroll ya watumishi Umma na kulipwa fedha zinazotokana na kodi za Wananchi kwa ajili ya kufanya kazi hizo za kijinga na kishetani hasa kuzuia Wananchi wa Tanzania kupata maendeleo ya kweli kupitia vyama mbadala.

Kwa miaka mingi sana, CCM walitumia mbinu hii kwa CHADEMA na walifanikiwa kuweka watu wengi sana CHADEMA kwa ajili ya kuhakikisha Chama hiki hakiwi imara na kuwa mbadala kwa Watanzania. Albert Msando, Petrobas Katambi, Vicent Mashinji na Tumaini Makene ni mfano wa baadhi ya watu tu ambao waliajiriwa na mfumo kwa sababu za kisiasa hasa kuwa Mapandikizi ndani ya CHADEMA na kuhakikisha Chama hiki hakitulii na kushika Madaraka. Hawa walipotoka bado watu wengi sana waliendelea kuwa waajiriwa wa mfumo wa kishetani wa CCM ndani ya Chadema.

Kuibuka kwa Tundu Lissu na John Heche kushika madaraka ndani ya Chadema imeelezwa kuwa ni sehemu ya mkakati wa watu wachache wenye akili huko TISS ambao wameamua kuisafisha nchi yetu dhidi ya upuuzi na ufedhuli wa CCM.

Kwa bahati mbaya sana, CCM na wajinga wao wachache wanaowatumia huko TISS wanafikiri wanaweza kuwatumia mapandikizi ambao kwa sasa hawana chao CHADEMA kutokana na Uongozi wa Lissu na Heche kuleta mifarakano na mitafaruko ndani ya CHADEMA.

Mategemeo ya CCM na wajinga wao waliopo TISS ni CHADEMA kupanick na kushindwa kujikita kwenye ajenda ya Msingi ya No Reform No Election ambayo kiuhalisia imebuniwa ili kulikomboa Taifa hili na kuzikwa kabisa kutokana na ujinga na upuuzi uliosababisha na CCM ambao umeliangamizq tayari Taifa kwa sehemu kubwa sana.

Mategemeo ya CCM na wajinga wachache ni kuwatumia hawa mamluki kuleta tension na vita ya madaraka ndani ya CHADEMA ili kumfanya msajili au Mahakama waingilie kati na kuweka hawa mapandikizi kwenye Uongozi wa CHADEMA na hatimaye CCM iendelee kuifisadi hii nchi bila kukoma.

Wasichojua CCM ni kwamba CHADEMA ipo chini ya watu makini na wanaotumia akili sana kipindi hiki. Hawa Mamluki wote sio kwamba wamekaliwq kimya ila kiuhalisia hatua zote za kisheria zinavhukuliwa dhidi yao na kwa hatua zinazochukuliwa hawatakuwa na nafasi ya kushinda Mahali popote pale kwenye jicho la Sheria.

Kutokana na ubobevu uliotukuka wa Sheria wa Lissu hawa mapandikizi ambao wote sasa wanajulikana sio tu CHADEMA hadi na wananchi wengi wanapewa maonyo na barua za kujieleza huku umma ukijulishwa hatua tajwa kiasi ambacho kamwe hawawezi kuja kusema walionewq pale watakapochukuliwa hatua stahiki.

Jambo kubwa zaidi linalotokea sasa ni kwamba, Wananchi wa Tanzania sasa wameanza kupevuka kwa kasi ya kutisha kiasi cha kutopelekeshwa tena na propaganda za kijinga pamoja na siasa za uzandiki zina,ofanywa na CCM na Mapandikizi wao.

Mfano mzuri wa haya ni namna umma wa Watanzania ulivyosema wazi kuhusu kutumiwa kwa Katibu wa Bawacha Mkoani Njombe aliyetengeneza tukio la kupigwa na walinzi wa Heche ili kuwatoa wananchi kwenye ajenda ya maana ya No Reform No Election.

Nawaonea huruma sana CCM. Wakati haupo upande wenu. Kubalini tu kuwa hakuna marefu yasiyo na ncha na kwa sasa hakuna mbinu chafu mtakayofanya dhidi ya CHADEMA ya Lissu na Heche itakayofanikiwa.

Mungu atawaadhibu vibaya sana.
Hawatoboi
 
Ilianza Lissu alipotangaza nia ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti, hawakutegemea Mbowe kupata upinzani, hawakutegemea Lissu angeshinda.

Sasa ni milio kila kona, baada ya mda wataona maisha katika mwanga bora.
 
Back
Top Bottom