Agizo la kuoa mke zaidi ya mmoja sio realistic ndio maana hata namba zinagoma.
SIO AGIZO, ni Ruhusa. Kuwa ‘objective’ uuelewe vyema Uislam. Ukishaelewa kua SI AGIZO bali ni Ruksa huu uzi unapoteza maana.
Namba zinagoma kweli? Hebu kuwa ‘Objective’ tufunge huu mjadala.
Maeneo mengi utakuta wanawake ni wengi kuliko wanaume ‘with exception of few areas’ na sababu ziko dhahiri.
Wasaikolojia leo wanatwambia ‘Men tends to be more aggressive than women’ na ndiyo maana wengi wako magerezani ukilinganisha na wanaume.
Vita zikitokea wengi wa wanaokufa ni wanaume, kama wewe ni mfuatiliaji utagundua hata wakati wa vita ya Urusi na Ukraine Wanawake na watoto waliruhusiwa kuondoka Ukraine huku Wanaume wakilzimishwa kubaki kupigana.
Ulevi na uraibu wa madawa ya kulevya huwaathiri sana wanaume kuliko wanawake, na wataalam wanatueleza kuwa Wanaume wako kwenye hatari kubwa kuingia kwenye uraibu kuliko wanawake.
Uwiano wa kujinyonga ni mkubwa kwa wanaume kuliko wanawake. Yaani kuna nafasi kubwa kwa ME kujinyonga kuliko KE.
Sasa namba zinagoma wapi? Au niambie ni mkoa gani Tanzania wanaume wamekosa wake wa kuoa kisa Waislam wameoa wake wengi?
Hilo jambo lingekuwa sahihi basi wanawake wangekuwa wanalifurahia. Haiwezekani Allah aruhusu kitu wakati huohuo aweke ndani ya mioyo ya wanawake chuki pale jambo hilo la heri linapotokea.
Unasema mungu kaweka chuki kwa KE juu ya ndoa hizi, ni kweli wapo baadhi ya KE wasiopenda kuolewa hivi na pia wapo wanaopenda kuolewa namna hii.
Na ushahidi wa hili ni mwingi watu wangapi na wengine mashuhuri wana wake wengi?
Hapo zamani babu zetu walioa wake wangapi?
(Ukisoma historia hata kidogo hili haliwezi gumu kuelewa)
Kama ni mfuatiliaji utaona namna jamii zetu zilivyo hivi sasa, mtu ana mke mmoja na michepuko kadhaa. Na hapa michepuko hii haina haki yoyote kwa mume kisheria ila watakapozaa.
Sasa ipi bora, mtu huyu kumwozesha wake wengine kihalali na kuwapa wake hao haki zao kamili kama wake na hadhi zao ktk jamii au kuendelea kuwadunisha kwa kuwa michepuko wasio na haki wala hadhi kijamii?
Agizo hilo limepuuzwa na modern society ndio maana hapajatokea upungufu wa wanawake.
Narudia tena, kuwa ‘Objective’ ili uelewe kitu kidogo sana.
KUOA WAKE WANNE SIO AGIZO, NI RUHUSA!
Maana msingi wa uzi wako uko hapa, ukielewa kuwa SI AGIZO utaelewa vingine.
Wapi pamesemwa aoe zaidi ya mke mmoja?
Unaona sasa? Biblia haijawa wazi kwenye hilo Quran imetueleza wazi kuwa “…. Oa mmoja tu…”
Biblia haijasema kitu kuhusu idadi ya wake wa kuoa, na pia haijasema mtu aoe mmoja, hayo ni mawazo ya wakuu wa kanisa tu ambayo hayana mshikamano na Biblia takatifu.
Unamjua Ibrahimu? Baba wa iman alikuwa na wake wangapi?
Unamjua mtu mfalme mwenye busara pengine kuliko wote, Mfalme Suleyman alikuwa na wake wangapi?
Na uzuri mifano iko mingi sana, sasa wewe unamzidi utukufu Suleyman? Au Ibrahimu? Kiasi ujiharamishie kuoa wake wengi?
Au ni wapi kwenye biblia imekatazwa mtu kuoa wake wengi?
Vipi kuhusu Jacob, Esau, Lamek, Abijah, Gideon.
Ukitaka kulijua hili vyema msome Father Adrian Hastings kwenye kitabu chake “Christian marriages in Africa” uupate ukweli wa madai yako dhalili ati Biblia imesema mtu aoe mke mmoja.
(Acha uvivu msome Father Adrian kweli)
Bible ipo clear, kama mtu amekuwa mzinifu unaruhusiwa kutengana naye. Na ukiona kukaa mwenyewe kumekuchosha basi rudi kwa mtu wako myatengeneze. Hakuna sababu nyingine yoyote iliyoruhusiwa.
Vizuri, maana imeonesha kuwa ‘progressive’ kidogo.
Kwahiyo mwenza akikutukania wazazi wako, akawa hapendi ndugu zako, mchawi muuaji ila si mzinifu huwezi kumwacha?
Hivi unajua unachokisema ? Unajua ‘complexity’ ya ndoa? au unakariri vifungu na kuvimeza kama vilivyo wala hufikiri?
Sasa practicality ni jambo la wanadamu tu.
Nakuuliza tena, unajua unachokiongea mkuu?
Hivi ulete sheria ambazo hazipo ‘practical’ jamii itastawi vipi?
Sheria ya ndoa hata hapa tz inamruhusu mkristo kuivunja kupitia mahakama lakini haimaanishi kwamba ndoa imevunjwa mbinguni. Biblia itaheshimika milele kwasababu imeweka msingi kwenye upendo wa kweli na msamaha.
Mkuu jipe muda soma tena ukristo, usome vizuri na usome Uislam vizuri kisha uje uandike vitu vyenye mantiki nami ‘i will be more than happy to discuss spirituality with you’