Kwa takwimu hizi za sensa hapa Tanzania na duniani, agizo la Quran kuoa mpaka wanawake wanne halitekelezeki

Kwa takwimu hizi za sensa hapa Tanzania na duniani, agizo la Quran kuoa mpaka wanawake wanne halitekelezeki

Umeelewa nilichoandika mkuu? Hebu soma tena

Ukisoma Quran vizuri Allah hajalazimisha mtu kuoa wake wanne, na kwakuwa hajalazimishwa mtu hivyo usitarajie kuona kila mtu anaoa wanne.”

Na kwa watakaofanya hivyo wanapewa sharti la kuwa na uwezo wa kufanya uadilifu baina ya wakeze.
Ukishatoa ruhusa ya jambo fulani kutokea unatakiwa kuweka mazingira ya hilo jambo kutokea. Ina maana Allah amesahau kwamba alitoa hilo agizo ndio maana anaumba wanaume wengi kuliko wanawake hapa duniani?
Dah, hapo ni wapi tumeambiwa tuoe mke mmoja? Na tusioe wake wengi mkuu?
Wapi hapo amesema uoe zaidi ya mke mmoja? Ipo clear, mwanaume ataambatana na mke wake na hakuna talaka.
 
Kwahiyo hiyo surplus ndio inatakiwa angalau wanaume laki tano wa kiislamu wajipatie wake wanne halafu wengine wabakie hivyo? Kumbe quran iliandika agizo kwa ajili ya wachache? Na hii ni kwa Tanzania peke yake.

Mbona umeziepuka takwimu za dunia nzima zinazoonesha wanaume ni wengi zaidi?
Na sio wanaume wote wanaume wote wanaoa wake wanne.
 
Nikweli kabisa wakiwaruhusu mbona makanisa kila kona watayaona.
Ethiopia waliwahi kupiga marufuku wakristo hivyo ikawa inaaminika kwamba hawapo tena.

Baada ya miaka mingi wakaja kuruhusu wakashangaa sana ndani ya wiki moja mfumo wote wa ukristo ulikuwa in place kuanzia maaskofu, wachungaji, wainjilisti na wazee wa kanisa.

Kumbe kwa miaka yote walikuwepo kimyakimya. Utashangaa siku Saudi Arabia, Iran, Yemen, nk wakiweka uhuru kukawa na wakristo wengi kuliko sehemu nyingine duniani.
 
Ukishatoa ruhusa ya jambo fulani kutokea unatakiwa kuweka mazingira ya hilo jambo kutokea. Ina maana Allah amesahau kwamba alitoa hilo agizo ndio maana anaumba wanaume wengi kuliko wanawake hapa duniani?
Unaelewa ninachojaribu kukueleza kweli?

Kuoa wake wanne si amri, ni ruhusa kwa watakaoweza. Na toka ruhusa hiyo imetolewa miaka 1400 iliyopita ushawi sikia kesi kuwa kuna mahali Wanawake hawatoshi kwa sababu kuna Waislamu wameoa wake wengi?

Wapi hapo amesema uoe zaidi ya mke mmoja? Ipo clear, mwanaume ataambatana na mke wake na hakuna talaka.
Sasa hapo wapi imekatazwa kuoa mke zaidi ya mmoja?

Halafu suala la talaka wewe umesema “hakuna talaka” kwa akili ya kawaida isiyohitaji Digirii unadhani ‘is it practical?’

Wewe ndiye unaefanya watu waitukane Biblia takatifu.
 
Kumbe kwa miaka yote walikuwepo kimyakimya. Utashangaa siku Saudi Arabia, Iran, Yemen, nk wakiweka uhuru kukawa na wakristo wengi kuliko sehemu nyingine duniani.
Una takwimu mkuu?

Kwa mujibu wa tafiti iliyofanywa na ‘Pew Research Center’ mwaka 2017 iliitaja Uislamu kuwa ni Dini inayokua kwa kasi zaidi.

Mwaka ule waislamu walikadiriwa kuwa Bilioni 1.8 duniani ila inatazamiwa idadi hiyo kuongezeka na kufikia Bilioni 3 ifikapo 2060 ambapo ni ongezeko la zaidi ya 70% Huku wakristo wanatazamiwa kuongezeka kwa asilimia 34% tu.

Na wakati huo watu watatu kati ya kumi watakuwa ni Waislam duniani.

Kama hauna takwimu maneno yako yanakuwa ‘mere speculation’ na inapaswa kuwa ninaibu kuyaandika katika jukwaa kama hili.
 
Hivi unakijua unachokisema au unabahatisha?

Kwa Marekani pekee ‘Federal Bureau of Prison’ walitoa ripoti iliyoonesha kuwa 93% ya wafungwa wao ni wanaume na wanawake ni 7% pekee.

Kwa duniani inakadiriwa kuwa (hii ni takwimu ya muda mrefu kidogo lakini itatusaidia walau kupata picha, ni ya 2010) kati ya Wafungwa 16 basi 15 ni wanaume na mwanamke ni mmoja tu, hiyo ni DUNIANI.

Nakuuliza tena unajua unachokisema au unabahatisha? Championship
Niambie duniani kuna wafungwa wangapi ili tuone kama idadi hiyo itakuwa kubwa na significant ukifananisha na uwepo wa wanaume bilioni 3+ na wanawake bilioni 3+
 
Yule mungu wa lugha moja tu ana maagizo ya hovyo sana pamoja na mtume wake
Mimi huwa ninaanini Muhammad alikuwa jamaa aliyetaka umaarufu hivyo akatunga stori nyingi nyingi na kuanzisha dini na matokeo yake ndio sasa errors kibao zinaonekana.
 
Una takwimu mkuu?

Kwa mujibu wa tafiti iliyofanywa na ‘Pew Research Center’ mwaka 2017 iliitaja Uislamu kuwa ni Dini inayokua kwa kasi zaidi.

Mwaka ule waislamu walikadiriwa kuwa Bilioni 1.8 duniani ila inatazamiwa idadi hiyo kuongezeka na kufikia Bilioni 3 ifikapo 2060 ambapo ni ongezeko la zaidi ya 70% Huku wakristo wanatazamiwa kuongezeka kwa asilimia 34% tu.

Na wakati huo watu watatu kati ya kumi watakuwa ni Waislam duniani.
Nawe unaamin?? kadri miaka inavyokwenda hizi dini zitakosa kabisa wafuasi.
 
Kuna mambo yanafikirisha pale baadhi ya vitabu vya kale kutoa maelekezo ambayo yanapingana na uhalisia wa dunia.

Tanzania (mwaka 2022)
Wanawake 31,687,990
Wanaume 30,053,130

Duniani (mwaka 2021)
Wanaume: 3,970,238,390 (bilioni 3.97 sawa na asilimia 50.42%)
Wanawake: 3,904,727,342 (bilioni 3.905 sawa na asilimia 49.58%)

Kwahiyo hapa duniani, kwa kila wanawake 100 wanaozaliwa kuna wanaume 106 wanazaliwa. Wanaume ni wengi kuliko wanawake kwa mujibu wa takwimu zinazotambulika.

Wanaume wakiamua kuoa wake wanne kama Quran inavyoruhusu basi itabidi hao wanawake wawe wa shirikisho kwa wanaume. Hii haikubaliki katika jamii nyingi ulimwenguni.

Allah atakuwa alitoa agizo hili bila kuifahamu dunia maana tungetegemea wanawake wawe wengi sana kuliko wanaume. Tunaweza kuhitimisha kwamba hakuifahamu dunia.
Unatakiwa ujue wanaume wanakufa vitani,hawana nguvu za kiume na Pia Sio wanaume wote wataweza kuoa wake zaidi ya 1,Ruhusa ya kuoa wake wengi inawahitaji wale tu wenye vigezo sio kila anayevaa suruali,hivyo Kwa idadi yetu wanaume Bado agizo la Quran lipo sahihi asilimia 100% Hadi ninavyoandika muda huu.
 
Unaelewa ninachojaribu kukueleza kweli?

Kuoa wake wanne si amri, ni ruhusa kwa watakaoweza. Na toka ruhusa hiyo imetolewa miaka 1400 iliyopita ushawi sikia kesi kuwa kuna mahali Wanawake hawatoshi kwa sababu kuna Waislamu wameoa wake wengi?
Agizo la kuoa mke zaidi ya mmoja sio realistic ndio maana hata namba zinagoma. Hilo jambo lingekuwa sahihi basi wanawake wangekuwa wanalifurahia. Haiwezekani Allah aruhusu kitu wakati huohuo aweke ndani ya mioyo ya wanawake chuki pale jambo hilo la heri linapotokea.

Agizo hilo limepuuzwa na modern society ndio maana hapajatokea upungufu wa wanawake.
Sasa hapo wapi imekatazwa kuoa mke zaidi ya mmoja?

Halafu suala la talaka wewe umesema “hakuna talaka” kwa akili ya kawaida isiyohitaji Digirii unadhani ‘is it practical?’

Wewe ndiye unaefanya watu waitukane Biblia takatifu.
Wapi pamesemwa aoe zaidi ya mke mmoja? Biblia ipo clear, kama mtu amekuwa mzinifu unaruhusiwa kutengana naye. Na ukiona kukaa mwenyewe kumekuchosha basi rudi kwa mtu wako myatengeneze. Hakuna sababu nyingine yoyote iliyoruhusiwa.

Sasa practicality ni jambo la wanadamu tu. Sheria ya ndoa hata hapa tz inamruhusu mkristo kuivunja kupitia mahakama lakini haimaanishi kwamba ndoa imevunjwa mbinguni. Biblia itaheshimika milele kwasababu imeweka msingi kwenye upendo wa kweli na msamaha.
 
Una takwimu mkuu?

Kwa mujibu wa tafiti iliyofanywa na ‘Pew Research Center’ mwaka 2017 iliitaja Uislamu kuwa ni Dini inayokua kwa kasi zaidi.

Mwaka ule waislamu walikadiriwa kuwa Bilioni 1.8 duniani ila inatazamiwa idadi hiyo kuongezeka na kufikia Bilioni 3 ifikapo 2060 ambapo ni ongezeko la zaidi ya 70% Huku wakristo wanatazamiwa kuongezeka kwa asilimia 34% tu.

Na wakati huo watu watatu kati ya kumi watakuwa ni Waislam duniani.

Kama hauna takwimu maneno yako yanakuwa ‘mere speculation’ na inapaswa kuwa ninaibu kuyaandika katika jukwaa kama hili.
Uislamu unaongezeka kwenye nchi ya ufaransa na sababu zinaeleweka. Pia waislamu wanakuwa wengi kwasababu wanazaliana sana. Ukristo halisi wa wale ambao ni wafuasi wa mafundisho ya Bwana Yesu Kristo katika biblia (acha huu wa dini kama ukatoliki nk) unaendelea kukua kimyakimya na unao wafuasi imara.

Ila ukiangalia kwa ukaribu zaidi siioni sustainability ya ukuaji wa uislamu kwa miaka ijayo kwasababu jamii za sasa zinaepuka sana kuzingatia imani za dini au angalau asilimia kubwa ya wanaoitwa waamini ni watu ambao hawajasimama imara kwenye hizo imani.

Hata hivyo kinabii inatarajiwa uislamu na ukatoliki utakuja kuungana na kutengeneza dini moja maalumu kwa ajili ya ulimwengu wote hivyo kwangu mimi makundi haya mawili lazima yataendelea kukua na kuwa integrated.
 
Unatakiwa ujue wanaume wanakufa vitani,hawana nguvu za kiume na Pia Sio wanaume wote wataweza kuoa wake zaidi ya 1,Ruhusa ya kuoa wake wengi inawahitaji wale tu wenye vigezo sio kila anayevaa suruali,hivyo Kwa idadi yetu wanaume Bado agizo la Quran lipo sahihi asilimia 100% Hadi ninavyoandika muda huu.
Idadi ya wanaume kwa takwimu za mwaka 2021 hapa duniani zimewazidi wanawake kwa milioni 60+ hivyo hayo makundi maalumu umeyataja hapo yanaweza kujazwa na watu hao.

Kwahiyo bado haijawa clear kwanini Allah ameshindwa kuumba angalau wanawake wengi zaidi ya wanaume ili ruhusa yake iweze kutekelezwa.
 
Una takwimu mkuu?

Kwa mujibu wa tafiti iliyofanywa na ‘Pew Research Center’ mwaka 2017 iliitaja Uislamu kuwa ni Dini inayokua kwa kasi zaidi.

Mwaka ule waislamu walikadiriwa kuwa Bilioni 1.8 duniani ila inatazamiwa idadi hiyo kuongezeka na kufikia Bilioni 3 ifikapo 2060 ambapo ni ongezeko la zaidi ya 70% Huku wakristo wanatazamiwa kuongezeka kwa asilimia 34% tu.

Na wakati huo watu watatu kati ya kumi watakuwa ni Waislam duniani.
Sisi wakristo Mungu wetu aamini kwenye wingi nikutolee mfano middle east Israel ni nchi ndogo sana lakin ilishapigana vita na nchi tano za kiarabu na ikazishinda kwetu wingi sio hoja
 
Sisi wakristo Mungu wetu aamini kwenye wingi nikutolee mfano middle east Israel ni nchi ndogo sana lakin ilishapigana vita na nchi tano za kiarabu na ikazishinda kwetu wingi sio hoja
Mkuu ile hoja ilikuwa inajibu madai ya waislamu kukimbilia ukristo.

Ila kukujibu ni kuwa Mungu ni kweli hajali wingi, anajali haki tu!
 
Kuna mambo yanafikirisha pale baadhi ya vitabu vya kale kutoa maelekezo ambayo yanapingana na uhalisia wa dunia.

Tanzania (mwaka 2022)
Wanawake 31,687,990
Wanaume 30,053,130

Duniani (mwaka 2021)
Wanaume: 3,970,238,390 (bilioni 3.97 sawa na asilimia 50.42%)
Wanawake: 3,904,727,342 (bilioni 3.905 sawa na asilimia 49.58%)

Kwahiyo hapa duniani, kwa kila wanawake 100 wanaozaliwa kuna wanaume 106 wanazaliwa. Wanaume ni wengi kuliko wanawake kwa mujibu wa takwimu zinazotambulika.

Wanaume wakiamua kuoa wake wanne kama Quran inavyoruhusu basi itabidi hao wanawake wawe wa shirikisho kwa wanaume. Hii haikubaliki katika jamii nyingi ulimwenguni.

Allah atakuwa alitoa agizo hili bila kuifahamu dunia maana tungetegemea wanawake wawe wengi sana kuliko wanaume. Tunaweza kuhitimisha kwamba hakuifahamu dunia.
Sensa ni zinadhaminiwa na wazungu lazima hesabu itoke kama wanavyotaka wao ili iwe rahisi kuleta mambo ya gender equity na mambo yao ya magasho
 
Uislamu unaongezeka kwenye nchi ya ufaransa na sababu zinaeleweka. Pia waislamu wanakuwa wengi kwasababu wanazaliana sana. Ukristo halisi wa wale ambao ni wafuasi wa mafundisho ya Bwana Yesu Kristo katika biblia (acha huu wa dini kama ukatoliki nk) unaendelea kukua kimyakimya na unao wafuasi imara.

Ila ukiangalia kwa ukaribu zaidi siioni sustainability ya ukuaji wa uislamu kwa miaka ijayo kwasababu jamii za sasa zinaepuka sana kuzingatia imani za dini au angalau asilimia kubwa ya wanaoitwa waamini ni watu ambao hawajasimama imara kwenye hizo imani.

Hata hivyo kinabii inatarajiwa uislamu na ukatoliki utakuja kuungana na kutengeneza dini moja maalumu kwa ajili ya ulimwengu wote hivyo kwangu mimi makundi haya mawili lazima yataendelea kukua na kuwa integrated.
Mkuu kusema Uislam unakua Ufaransa peke yake umefanya tafiti?

Kama hujafanya taarifa hiyo umeitoa wapi?

Halafu hivi unajua kuna wimbi kubwa la watu wanaoacha kujihusisha na dini?

Mkuu hizi hoja ni mawazo yako au ni ‘fact’? Naona hazina uhalisia kwa yanayoendelea Duniani.
 
Agizo la kuoa mke zaidi ya mmoja sio realistic ndio maana hata namba zinagoma.
SIO AGIZO, ni Ruhusa. Kuwa ‘objective’ uuelewe vyema Uislam. Ukishaelewa kua SI AGIZO bali ni Ruksa huu uzi unapoteza maana.

Namba zinagoma kweli? Hebu kuwa ‘Objective’ tufunge huu mjadala.

Maeneo mengi utakuta wanawake ni wengi kuliko wanaume ‘with exception of few areas’ na sababu ziko dhahiri.

Wasaikolojia leo wanatwambia ‘Men tends to be more aggressive than women’ na ndiyo maana wengi wako magerezani ukilinganisha na wanaume.

Vita zikitokea wengi wa wanaokufa ni wanaume, kama wewe ni mfuatiliaji utagundua hata wakati wa vita ya Urusi na Ukraine Wanawake na watoto waliruhusiwa kuondoka Ukraine huku Wanaume wakilzimishwa kubaki kupigana.

Ulevi na uraibu wa madawa ya kulevya huwaathiri sana wanaume kuliko wanawake, na wataalam wanatueleza kuwa Wanaume wako kwenye hatari kubwa kuingia kwenye uraibu kuliko wanawake.

Uwiano wa kujinyonga ni mkubwa kwa wanaume kuliko wanawake. Yaani kuna nafasi kubwa kwa ME kujinyonga kuliko KE.

Sasa namba zinagoma wapi? Au niambie ni mkoa gani Tanzania wanaume wamekosa wake wa kuoa kisa Waislam wameoa wake wengi?

Hilo jambo lingekuwa sahihi basi wanawake wangekuwa wanalifurahia. Haiwezekani Allah aruhusu kitu wakati huohuo aweke ndani ya mioyo ya wanawake chuki pale jambo hilo la heri linapotokea.
Unasema mungu kaweka chuki kwa KE juu ya ndoa hizi, ni kweli wapo baadhi ya KE wasiopenda kuolewa hivi na pia wapo wanaopenda kuolewa namna hii.

Na ushahidi wa hili ni mwingi watu wangapi na wengine mashuhuri wana wake wengi?

Hapo zamani babu zetu walioa wake wangapi?

(Ukisoma historia hata kidogo hili haliwezi gumu kuelewa)

Kama ni mfuatiliaji utaona namna jamii zetu zilivyo hivi sasa, mtu ana mke mmoja na michepuko kadhaa. Na hapa michepuko hii haina haki yoyote kwa mume kisheria ila watakapozaa.

Sasa ipi bora, mtu huyu kumwozesha wake wengine kihalali na kuwapa wake hao haki zao kamili kama wake na hadhi zao ktk jamii au kuendelea kuwadunisha kwa kuwa michepuko wasio na haki wala hadhi kijamii?

Agizo hilo limepuuzwa na modern society ndio maana hapajatokea upungufu wa wanawake.
Narudia tena, kuwa ‘Objective’ ili uelewe kitu kidogo sana. KUOA WAKE WANNE SIO AGIZO, NI RUHUSA!

Maana msingi wa uzi wako uko hapa, ukielewa kuwa SI AGIZO utaelewa vingine.

Wapi pamesemwa aoe zaidi ya mke mmoja?
Unaona sasa? Biblia haijawa wazi kwenye hilo Quran imetueleza wazi kuwa “…. Oa mmoja tu…”

Biblia haijasema kitu kuhusu idadi ya wake wa kuoa, na pia haijasema mtu aoe mmoja, hayo ni mawazo ya wakuu wa kanisa tu ambayo hayana mshikamano na Biblia takatifu.

Unamjua Ibrahimu? Baba wa iman alikuwa na wake wangapi?

Unamjua mtu mfalme mwenye busara pengine kuliko wote, Mfalme Suleyman alikuwa na wake wangapi?

Na uzuri mifano iko mingi sana, sasa wewe unamzidi utukufu Suleyman? Au Ibrahimu? Kiasi ujiharamishie kuoa wake wengi?

Au ni wapi kwenye biblia imekatazwa mtu kuoa wake wengi?

Vipi kuhusu Jacob, Esau, Lamek, Abijah, Gideon.

Ukitaka kulijua hili vyema msome Father Adrian Hastings kwenye kitabu chake “Christian marriages in Africa” uupate ukweli wa madai yako dhalili ati Biblia imesema mtu aoe mke mmoja.

(Acha uvivu msome Father Adrian kweli)
Bible ipo clear, kama mtu amekuwa mzinifu unaruhusiwa kutengana naye. Na ukiona kukaa mwenyewe kumekuchosha basi rudi kwa mtu wako myatengeneze. Hakuna sababu nyingine yoyote iliyoruhusiwa.
Vizuri, maana imeonesha kuwa ‘progressive’ kidogo.

Kwahiyo mwenza akikutukania wazazi wako, akawa hapendi ndugu zako, mchawi muuaji ila si mzinifu huwezi kumwacha?

Hivi unajua unachokisema ? Unajua ‘complexity’ ya ndoa? au unakariri vifungu na kuvimeza kama vilivyo wala hufikiri?

Sasa practicality ni jambo la wanadamu tu.
Nakuuliza tena, unajua unachokiongea mkuu?

Hivi ulete sheria ambazo hazipo ‘practical’ jamii itastawi vipi?

Sheria ya ndoa hata hapa tz inamruhusu mkristo kuivunja kupitia mahakama lakini haimaanishi kwamba ndoa imevunjwa mbinguni. Biblia itaheshimika milele kwasababu imeweka msingi kwenye upendo wa kweli na msamaha.
Mkuu jipe muda soma tena ukristo, usome vizuri na usome Uislam vizuri kisha uje uandike vitu vyenye mantiki nami ‘i will be more than happy to discuss spirituality with you’
 
Back
Top Bottom