Kwa takwimu hizi za sensa hapa Tanzania na duniani, agizo la Quran kuoa mpaka wanawake wanne halitekelezeki

Kwa takwimu hizi za sensa hapa Tanzania na duniani, agizo la Quran kuoa mpaka wanawake wanne halitekelezeki

SIO AGIZO, ni Ruhusa. Kuwa ‘objective’ uuelewe vyema Uislam. Ukishaelewa kua SI AGIZO bali ni Ruksa huu uzi unapoteza maana.

Namba zinagoma kweli? Hebu kuwa ‘Objective’ tufunge huu mjadala.

Maeneo mengi utakuta wanawake ni wengi kuliko wanaume ‘with exception of few areas’ na sababu ziko dhahiri.

Wasaikolojia leo wanatwambia ‘Men tends to be more aggressive than women’ na ndiyo maana wengi wako magerezani ukilinganisha na wanaume.

Vita zikitokea wengi wa wanaokufa ni wanaume, kama wewe ni mfuatiliaji utagundua hata wakati wa vita ya Urusi na Ukraine Wanawake na watoto waliruhusiwa kuondoka Ukraine huku Wanaume wakilzimishwa kubaki kupigana.

Ulevi na uraibu wa madawa ya kulevya huwaathiri sana wanaume kuliko wanawake, na wataalam wanatueleza kuwa Wanaume wako kwenye hatari kubwa kuingia kwenye uraibu kuliko wanawake.

Uwiano wa kujinyonga ni mkubwa kwa wanaume kuliko wanawake. Yaani kuna nafasi kubwa kwa ME kujinyonga kuliko KE.

Sasa namba zinagoma wapi? Au niambie ni mkoa gani Tanzania wanaume wamekosa wake wa kuoa kisa Waislam wameoa wake wengi?

Unasema mungu kaweka chuki kwa KE juu ya ndoa hizi, ni kweli wapo baadhi ya KE wasiopenda kuolewa hivi na pia wapo wanaopenda kuolewa namna hii.

Na ushahidi wa hili ni mwingi watu wangapi na wengine mashuhuri wana wake wengi?

Hapo zamani babu zetu walioa wake wangapi?

(Ukisoma historia hata kidogo hili haliwezi gumu kuelewa)

Kama ni mfuatiliaji utaona namna jamii zetu zilivyo hivi sasa, mtu ana mke mmoja na michepuko kadhaa. Na hapa michepuko hii haina haki yoyote kwa mume kisheria ila watakapozaa.

Sasa ipi bora, mtu huyu kumwozesha wake wengine kihalali na kuwapa wake hao haki zao kamili kama wake na hadhi zao ktk jamii au kuendelea kuwadunisha kwa kuwa michepuko wasio na haki wala hadhi kijamii?

Narudia tena, kuwa ‘Objective’ ili uelewe kitu kidogo sana. KUOA WAKE WANNE SIO AGIZO, NI RUHUSA!

Maana msingi wa uzi wako uko hapa, ukielewa kuwa SI AGIZO utaelewa vingine.

Unaona sasa? Biblia haijawa wazi kwenye hilo Quran imetueleza wazi kuwa “…. Oa mmoja tu…”

Biblia haijasema kitu kuhusu idadi ya wake wa kuoa, na pia haijasema mtu aoe mmoja, hayo ni mawazo ya wakuu wa kanisa tu ambayo hayana mshikamano na Biblia takatifu.

Unamjua Ibrahimu? Baba wa iman alikuwa na wake wangapi?

Unamjua mtu mfalme mwenye busara pengine kuliko wote, Mfalme Suleyman alikuwa na wake wangapi?

Na uzuri mifano iko mingi sana, sasa wewe unamzidi utukufu Suleyman? Au Ibrahimu? Kiasi ujiharamishie kuoa wake wengi?

Au ni wapi kwenye biblia imekatazwa mtu kuoa wake wengi?

Vipi kuhusu Jacob, Esau, Lamek, Abijah, Gideon.

Ukitaka kulijua hili vyema msome Father Adrian Hastings kwenye kitabu chake “Christian marriages in Africa” uupate ukweli wa madai yako dhalili ati Biblia imesema mtu aoe mke mmoja.

(Acha uvivu msome Father Adrian kweli)

Vizuri, maana imeonesha kuwa ‘progressive’ kidogo.

Kwahiyo mwenza akikutukania wazazi wako, akawa hapendi ndugu zako, mchawi muuaji ila si mzinifu huwezi kumwacha?

Hivi unajua unachokisema ? Unajua ‘complexity’ ya ndoa? au unakariri vifungu na kuvimeza kama vilivyo wala hufikiri?

Nakuuliza tena, unajua unachokiongea mkuu?

Hivi ulete sheria ambazo hazipo ‘practical’ jamii itastawi vipi?

Mkuu jipe muda soma tena ukristo, usome vizuri na usome Uislam vizuri kisha uje uandike vitu vyenye mantiki nami ‘i will be more than happy to discuss spirituality with you’
NAKAZIA
 
Waislamu wenzangu wametoa sababu nzuri Sana juu ya kwanini Allah alikuwa sahihi kuruhusu au kutoa RUHUSA ya wanaume kuoa wake wanne.

Ningependa kuongezea mambo mawili matatu

Kuna hoja inasema kama Allah ameridhia hivyo kwanini hajawafanya wanawake kuridhia swala Hilo?

Kwanza wivu ni Swala la asili ambalo tumeumbwa nalo,kwahiyo Kwa mwanamke kutopenda mume kuoa mke mwingine ni Swala la wivu Tu na si vingine

Lakini linatokana na Sisi wanaume wenyewe,tumetengeneza mazingira kwamba tunao mke mwingine kama kumtia adabu mke mkubwa ima Kwa kutokuwa na nidhamu au kutokuwa msikivu,sasa yote yanawafanya automatically kuchukia uke wenza

Na lingine ni kuhamisha mapenzi yote Kwa mke mpya na ni kitu ambacho hakifai katika Dini na tumesisitizwa Sana tufanye uadilifu Kwa wake zetu,ni ukweli usio pingika kuwa huwezi kuwapenda wote Kwa asilimia Mia lkn usimfanye huyo mwingine aonekane hapendwi

Kwahiyo hayo na mengine ndio huwafanya wanawake kuchukia uke wenza.

Lakini wengi wao wanajua Dini inaruhusu hivyo na hawana Shaka nalo.

Kuna mpuuzi mmoja wala sikutaka kumkoti alisema wanaume wameruhusiwa kuoa wake wengi eti kwasababu Tu wanaume walikufa vitani! Huyo ni mpuuzi kwasababu hajui anachokisema.

Kuna sababu zifuatazo ambazo Allah ametupa RUHUSA ya kuoa wake wanne kama tulitaka;

1) kuna wanaume ambao wamejaaliwa matamanio hasa au Wana nguvu hasa za kusex,watu kama hawa mke mmoja hawezi kumhudumia,yaani yeye anahitaji Sana sex kiasi kwamba inakuwa Keri Kwa mke,so mtu kama huyu ili kuepuka zinaa ni Bora akaongeza mke ili asimkosee Allah. Wengi wenu ni mashahidi humu mara nyingi Watu wanaandiza Uzi kuwa unakuta mke Hampi mumewe unyumba Bila sababu maalum,na ndio maana Michepuko inakuwa mingi Sana

2) Kuna vipindi ambavyo wanawake wanapitia ambavyo huchangia kushindwa kumhudumia mumewe ktk swala zima sex,mfano kipindi cha siku zake,au kipindi cha mimba,kuna wengine wakipata mimba Tu wanapata bed rest,na wengine hawajisikii jabisa kusex, hapo mwanaume atahitaji kuwa na mke mwingine ili mambo yaende Sawa.

3) Idadi ya waoaji ni ndogo Sana ukilinganisha na wasio oa,humu ndani si kuna wapuuzi wengi wanasemaga kataa ndoa,au naongopa? Je hawa Akina dada je watasitiriwa na Akina Nani kama sio wanaume marijali .

Hizo ni sababu chache Tu ishi nazo hizo Kwanza Kwa Leo!

Cha kuchekesha zaidi hawa wapuuzi ambao wanakataa kuoa wake wengi ndio wanaongoza Kwa kuwa na Michepuko huko mtaani pumbavu Sana!

Utasikia biblia imekataza kufanya hivyo,wakati hakuna kifungu kinachosema hivyo,Allah ni mmoja na ndio huyo huyo aliyetoa RUHUSA hiyo.

najua kuna wapuuzi watakuja kutoa povu!
 
Waislam wanaongezeka zaidi ufaransa, hiyo ni fact unaweza kupata taarifa zaidi mtandaoni.

Ila pia waislam wanayo tabia ya kuongea sana na kulalamika maeneo wanayokaribishwa ili tamaduni zao zifanywe rasmi hivyo huwa wanasikika sana ingawa ni wachache.
Kudai hivyo haitoshi kuthibitisha kuwa ni kweli, nipe data au chanzo cha taarifa yako mkuu.

Kama huna wakati mwingine usithubutu kusema kitu ambacho huna ushahidi nacho vinginevyo useme wazi kuwa hayo ni maoni yako binafsi.
 
Quran iikamilishe biblia?🤣🤣🤣 Weka link hapa tubonyeze ngapi kupata vichekesho kama hivi?

Maswali ya Robert kule hamjayajibu mkaleta blah blah tupu na kibadilisha mada kama ilivyo kawaida yenu.
Mkuu mpaka unasema haya upo kundi gani kati ya haya?
1. Unaijua Quran tu
2. Unaijua Biblia tu (halafu unatoa ‘commentary’ kuhusu Quran)
3. Unazijua Quran na Biblia

Kama upo kwenye kundi namba tatu, basi unaweza kuendelea kuleta mada za dini hizi mbili, vinginevyo jipe muda jifunze kuhusu dini zote mbili kwa utulivu, zielewe ili hata ukileta mada hapa iwe mada yenye mantiki si ya kishabiki isiyo na uthibitisho inayoonesha wazi mleta mada hajui anachokizungumza mkuu.

Kama Biblia takatifu inavyoeleza kwenye methali 15:14

The mind of the intelligent seeks knowledge, But the mouth of fools feeds on foolishness.”
 
Kile kitabu kinaunda mpaka majini i wish nikisome vzr japo kila nikijitahidi kukisoma sikielewi pia naona kina lugha ngumu sana kuelewa kuliko kukariri
 
Kile kitabu kinaunda mpaka majini i wish nikisome vzr japo kila nikijitahidi kukisoma sikielewi pia naona kina lugha ngumu sana kuelewa kuliko kukariri
Ndio mkuu kinaunda majini makubwa kama meli mkuu

Vipi tukuundie mkuu ufurahi!
 
Ndio mkuu kinaunda majini makubwa kama meli mkuu

Vipi tukuundie mkuu ufurahi!
Yale mazuri ninavyo sikia ila shida yake kuyafuga na upatane nayo! Ila kama ikupendeza niundie ambalo halina dushe wala mkia maana hayachelewi kuku_popo pawa na lisiwe linakunywa damu niwe nalicharge kwa solar maana umeme ni shida na lisiwe linaoga pia likubali kulala kwenye banda la kuku sio ndani kwangu!
 
Ruhusa ya kuoa wake wengi ni jambo linalopendwa na wanaume na lingechukuliwa serious basi Allah angebakia na aibu maana hajaweza kuumba wanawake wa kutosha ili litekelezwe.
Hilo linapendwa maana ni ‘practical and natural’ na ndiyo maana leo hii miaka 1400 tangu ruhusa hiyo itolewe HAKUNA MAHALI WATU WAMEKOSA WAKE ATI KISA WAISLAM WAMEOA WAKE WENGI.

Sijui kama unaelewa madai haya mkuu.

Quran 4
3. Give orphans their wealth ˹when they reach maturity˺, and do not exchange your worthless possessions for their valuables, nor cheat them by mixing their wealth with your own. For this would indeed be a great sin.

4. If you fear you might fail to give orphan women their ˹due˺ rights ˹if you were to marry them˺, then marry other women of your choice—two, three, or four. But if you are afraid you will fail to maintain justice, then ˹content yourselves with˺ one or those ˹bondwomen˺ in your possession. This way you are less likely to commit injustice.

Quran ndiyo kitabu pekee cha dini kilichoweka bayana idadi ya kuoa, na ndiyo kitabu pekee kilichoeleza kuwa mtu aoe mmoja tu.

Biblia takatifu hakuna mahali imeeleza idadi ya kuoa, hiyo inaweza tafsirika kuwa watu waoe kwa idadi yoyote waitakayo. Kitu ambacho ni ‘impractical’

Takwimu za dunia zinapingana na hilo, kuna wanaume milioni 60+ zaidi ya wanawake.
Unajua kwanini mkuu?
Nchi pekee zenye wanaume wengi kuliko wanawake ni Uchina na India.

Kwa Uchina hayo ni matokeo ya ‘One child Policy’ iliyoanzishwa miaka ya 1980 iliyolenga kudhibiti ongezeko la idadi ya watu.

Familia nyingi za kichina kufuatia sera hiyo walihakikisha wanaitumia nafasi hiyo yq kuzaa mtoto mmoja pekee wanaitumia kujipatia mtoto wa kiume, na hii ni kwa sababu kuwa jamii za kichina humthamini mwanaume kuliko mwanamke kama ilivyo kwa jamii nyingi za kiafrika. Kwahiyo ujauzito ulipotungwa wazazi walienda hospitali kujua jinsia na kama ujauzito huo ukigundulika kuwa ni mtoto wa kike basi wanaitoa na kama mtoto wa kiume basi huiacha.

Na ndiyo maana leo hii kuna zaidi ya wanaume milioni 30 kuliko wanawake.

Kwa India wao hali haikuwa hivyo kabisa, tangu miaka ya 1970 jamii familia nyingi zilikuwa zikienda hospitali kujua jinsia ya watoto wao, kama ni wa kike basi mimba iliharibiwa na kama ni wa kiume mimba iliachwa.

Mwaka 2011 shirika la Uingereza la ‘The Lancet’ lilibaini kuwa kwa miaka 30 iliyopita zaidi ya mimba milioni 12 za watoto wa kike zilitolewa.

Na serikali ya India ili kulikabili tatizo hili miaka ya 1990 ilipiga marufuku utoaji wa mimba kwa sababu ya jinsia lakini suala hilo linaendelea mpaka leo.

Leo hii ukiacha vitendo hivyo viovu vinavyofanywa Uchina na India kiasili idadi ya wanawake itaongezeka kuwa kubwa kuliko wanaume na sababu hiyo ndiyo asili na kanuni ya kimaumbile.

Hawa wapo kwenye hiyo category ya wanaume milioni 60+ waliozidi idadi ya wanawake unless ulete takwimu kwamba duniani wafungwa wanazidi hiyo namba.
Mkuu idadi ya wanaume waliozidi wanawake huko india ni zaidi ya milioni 33, na Uchina ni zaidi ya milioni 30.

Ukipiga hesabu hapo utajua hiyo idadi uliyoisema hapo.

Nakushauri, fanya tafiti kidogo kabla hujaleta mada mkuu.

Takwimu za dunia zinapingana na hii hoja yako.
Unajua ‘trend’ ya population mkuu?
Tafadhali hebu soma tena.

Nasikia aibu kuona unaandika madai kama haya, yanaonesha wazi kuwa hauko ‘informed’ na hii ni mbaya kwa taswira ya Ukristo maana watu wataona Wakristo wote hawana taarifa za kutosha.

Jitahidi kufanya tafiti kidogo upate taarifa za kutosha mkuu.

Weka hapa takwimu za hii category
Ripoti ya Umoja wa Mataifa juu ya matumizi ya dawa za kulevya

Research report

Takwimu za dunia kwa sasa zinapingana na hili maana wanaume ni wengi zaidi ya wanawake.
Rejea idadi ya watu wa Uchina na India nimekujibu hapo juu.
Kwa idadi ya wanaume waliopo duniani kwa sasa haiwezekani japo wanawake wakatutosha wote achilia mbali kuwa na mke zaidi ya mmoja.
Haiwezekani vipi mkuu? Mbona wapo waislam wengi na wengine Wakristo waliooa wake zaidi ya mmoja?

Na ni wapi umesikia kuna upungufu wa wanawake ati kisa kuna Waislam na wakristo wameoa wake wengi?

Madai yako hayana uhalisia, unadhania tu.

Huu ni uongo, hakuna mwanamke anataka au anapenda mume wake awe na mwanamke mwingine.
Mkuu umefanya tafiti? Mbona mifano iko mingi.

Mambo kama haya hayahitaji hisia zako binafsi mkuu wapo wanawake wanapenda ndoa hizi.

Hizi takwimu umezitoa wapi. Yaani weakness za watu wachache ndio zimfanye Allah kuruhusu watu waoe wake wengi? Halafu hapohapo Allah ameshindwa kuumba wanawake wengi kuliko wanaume.😂
Siyo kweli,
Lile ni ruhusa ambayo lazima ichangamkiwe lakini sasa Allah kashindwa kuumba wanawake wengi kuliko wanaume.
Siyo kweli, mkuu umesomea nini katika elimu yako?
Acha kuleta upotoshaji wako, biblia imesema Mungu alimuumba mtu mume na mke na hao WAWILI watakuwa mwili mmoja na hivyo mwanaume atawaacha wazazi wake na kuambatana na mkewe. ACHA KULETA UPOTOSHAJI.
Sasa hapo ni wapi imesemwa mtu aoe mke mmoja tu? Au ni wapi imekatazwa watu kuoa wake wengi?

Hebu msome Father Hastang uelewe uzushi huu wa ndoa moja kwenye ukristo umetokea wapi.

Nenda kasome Mathayo 19 kuanzia mstari wa tatu kama nilivyokuwekea post za nyuma uelewe kwanini watu walioa wake wengi agano la kale. Yesu alishaweka maelezo kwamba tangu MWANZO Mungu alimuumba Adam na Eva (hakuumba wanawake wengi kwa ajili ya Adam) na kwamba wakristo wanatakiwa kufuata utaratibu huo wa tangu mwanzo.
Mkuu hivi unaelewa?

Kwenye Biblia nzima hakuna mstari uliosema wanaume waoe mke mmoja tu. Na hakuna mstari unaosema kuoa wake wengi nk dhambi.
Ninamsoma Yesu Kristo katika biblia, sifuatishi opinion za watu wengine wala experience zao.
Hapo unakosea, huwezi itumia biblia kuwa chanzo cha kila kitu, umeonesha ujinga ulio nao.

Na Father Hasting alifanya tafiti objective sio ‘experience’

Soma upate maarifa uache uvivu.
Halafu kama husomi unapata wapi nguvu ya kuleta mada hapa?

Acha ujinga mkuu, unaudhalilisha ukristo.
Ndio maana Yesu Kristo alipomaliza ile sura ya 19 katika kitabu cha Mathayo alisema agizo hilo ni gumu na kwamba sio kila mtu atakuwa na imani ya kulifuata. Ukiwa mkristo lazima ufuate maagizo ya biblia na sio logic zako.
Ni kweli, lakini ni wapi Biblia imesema kuoa wake wengi dhambi?

Hebu nijibu kwanza, nipo na biblia za Tafsiri zote hapa, nasubiri.

Halafu wewe unamzidi Baba yetu Ibrahimu kwa imani? Unamzini Solomon kwa Imani? Wewe ni nani ktk ukristo uharamishe ndoa za wake wengi mkuu?
Mwenza wako akiwa na tabia hizo unapaswa kumuombea na kumuonyesha upendo wa Kristo na hatimaye atabadilika.
Hii ni ‘impractical’ na hujui kuhusu ‘complexity’ za ndoa wala ‘human psychology’
Tunafuata maelekezo ya biblia na sio popular opinion ya society.
Hiyo siyo ‘popular opinion’ hizo ni ‘scientific facts’ sio maoni binafsi, ni majibu ya tafiti mkuu.
Mantiki ni neno la Mungu katika biblia na sio opinion za watu wengine. Nimeisoma hiyo na nimeitumia kukujibu hapa.
Nakuuliza tena ni wapi kwenye biblia imekatazwa kuoa wake wengi?

Tupe mstari

Na ndiyo maana nakushauri ufanye tafiti ujue chanzo cha ndoa moja kwenye ukristo kimetokea wapi na huwezi fanya tafiti kama husomi, maana Yesu hawezi kukupa majibu ya maswali haya ndotoni mkuu.

Soma upate kuujua ukweli.
Msome David Gitari kwenye ‘Church and Polygamy’ kina kurasa 13 tu
Kipate hapa

Kama lugha itakuwa tabu niambie nijitahidi kukifasiri mkuu.
 
Yale mazuri ninavyo sikia ila shida yake kuyafuga na upatane nayo! Ila kama ikupendeza niundie ambalo halina dushe wala mkia maana hayachelewi kuku_popo pawa na lisiwe linakunywa damu niwe nalicharge kwa solar maana umeme ni shida na lisiwe linaoga pia likubali kulala kwenye banda la kuku sio ndani kwangu!
Sawa unalihitaji lini liwe tayar
 
Muda wowote ukisha liweka sawa nifahamishe nitakupa adress! Usije ukalituma na zile scoota za ku_deliver pizza! Bodaboda ni majanga anaweza asifike
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
🤣🤣🤣 Sawa nitazingatia ushauri wako mkuu
 
Hilo linapendwa maana ni ‘practical and natural’ na ndiyo maana leo hii miaka 1400 tangu ruhusa hiyo itolewe HAKUNA MAHALI WATU WAMEKOSA WAKE ATI KISA WAISLAM WAMEOA WAKE WENGI.

Sijui kama unaelewa madai haya mkuu.

Quran 4
3. Give orphans their wealth ˹when they reach maturity˺, and do not exchange your worthless possessions for their valuables, nor cheat them by mixing their wealth with your own. For this would indeed be a great sin.

4. If you fear you might fail to give orphan women their ˹due˺ rights ˹if you were to marry them˺, then marry other women of your choice—two, three, or four. But if you are afraid you will fail to maintain justice, then ˹content yourselves with˺ one or those ˹bondwomen˺ in your possession. This way you are less likely to commit injustice.

Quran ndiyo kitabu pekee cha dini kilichoweka bayana idadi ya kuoa, na ndiyo kitabu pekee kilichoeleza kuwa mtu aoe mmoja tu.

Biblia takatifu hakuna mahali imeeleza idadi ya kuoa, hiyo inaweza tafsirika kuwa watu waoe kwa idadi yoyote waitakayo. Kitu ambacho ni ‘impractical’

Unajua kwanini mkuu?
Nchi pekee zenye wanaume wengi kuliko wanawake ni Uchina na India.

Kwa Uchina hayo ni matokeo ya ‘One child Policy’ iliyoanzishwa miaka ya 1980 iliyolenga kudhibiti ongezeko la idadi ya watu.

Familia nyingi za kichina kufuatia sera hiyo walihakikisha wanaitumia nafasi hiyo yq kuzaa mtoto mmoja pekee wanaitumia kujipatia mtoto wa kiume, na hii ni kwa sababu kuwa jamii za kichina humthamini mwanaume kuliko mwanamke kama ilivyo kwa jamii nyingi za kiafrika. Kwahiyo ujauzito ulipotungwa wazazi walienda hospitali kujua jinsia na kama ujauzito huo ukigundulika kuwa ni mtoto wa kike basi wanaitoa na kama mtoto wa kiume basi huiacha.

Na ndiyo maana leo hii kuna zaidi ya wanaume milioni 30 kuliko wanawake.

Kwa India wao hali haikuwa hivyo kabisa, tangu miaka ya 1970 jamii familia nyingi zilikuwa zikienda hospitali kujua jinsia ya watoto wao, kama ni wa kike basi mimba iliharibiwa na kama ni wa kiume mimba iliachwa.

Mwaka 2011 shirika la Uingereza la ‘The Lancet’ lilibaini kuwa kwa miaka 30 iliyopita zaidi ya mimba milioni 12 za watoto wa kike zilitolewa.

Na serikali ya India ili kulikabili tatizo hili miaka ya 1990 ilipiga marufuku utoaji wa mimba kwa sababu ya jinsia lakini suala hilo linaendelea mpaka leo.

Leo hii ukiacha vitendo hivyo viovu vinavyofanywa Uchina na India kiasili idadi ya wanawake itaongezeka kuwa kubwa kuliko wanaume na sababu hiyo ndiyo asili na kanuni ya kimaumbile.

Mkuu idadi ya wanaume waliozidi wanawake huko india ni zaidi ya milioni 33, na Uchina ni zaidi ya milioni 30.

Ukipiga hesabu hapo utajua hiyo idadi uliyoisema hapo.

Nakushauri, fanya tafiti kidogo kabla hujaleta mada mkuu.

Unajua ‘trend’ ya population mkuu?
Tafadhali hebu soma tena.

Nasikia aibu kuona unaandika madai kama haya, yanaonesha wazi kuwa hauko ‘informed’ na hii ni mbaya kwa taswira ya Ukristo maana watu wataona Wakristo wote hawana taarifa za kutosha.

Jitahidi kufanya tafiti kidogo upate taarifa za kutosha mkuu.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa juu ya matumizi ya dawa za kulevya

Research report

Rejea idadi ya watu wa Uchina na India nimekujibu hapo juu.

Haiwezekani vipi mkuu? Mbona wapo waislam wengi na wengine Wakristo waliooa wake zaidi ya mmoja?

Na ni wapi umesikia kuna upungufu wa wanawake ati kisa kuna Waislam na wakristo wameoa wake wengi?

Madai yako hayana uhalisia, unadhania tu.

Mkuu umefanya tafiti? Mbona mifano iko mingi.

Mambo kama haya hayahitaji hisia zako binafsi mkuu wapo wanawake wanapenda ndoa hizi.

Siyo kweli,

Siyo kweli, mkuu umesomea nini katika elimu yako?

Sasa hapo ni wapi imesemwa mtu aoe mke mmoja tu? Au ni wapi imekatazwa watu kuoa wake wengi?

Hebu msome Father Hastang uelewe uzushi huu wa ndoa moja kwenye ukristo umetokea wapi.

Mkuu hivi unaelewa?

Kwenye Biblia nzima hakuna mstari uliosema wanaume waoe mke mmoja tu. Na hakuna mstari unaosema kuoa wake wengi nk dhambi.

Hapo unakosea, huwezi itumia biblia kuwa chanzo cha kila kitu, umeonesha ujinga ulio nao.

Na Father Hasting alifanya tafiti objective sio ‘experience’

Soma upate maarifa uache uvivu.
Halafu kama husomi unapata wapi nguvu ya kuleta mada hapa?

Acha ujinga mkuu, unaudhalilisha ukristo.

Ni kweli, lakini ni wapi Biblia imesema kuoa wake wengi dhambi?

Hebu nijibu kwanza, nipo na biblia za Tafsiri zote hapa, nasubiri.

Halafu wewe unamzidi Baba yetu Ibrahimu kwa imani? Unamzini Solomon kwa Imani? Wewe ni nani ktk ukristo uharamishe ndoa za wake wengi mkuu?

Hii ni ‘impractical’ na hujui kuhusu ‘complexity’ za ndoa wala ‘human psychology’

Hiyo siyo ‘popular opinion’ hizo ni ‘scientific facts’ sio maoni binafsi, ni majibu ya tafiti mkuu.

Nakuuliza tena ni wapi kwenye biblia imekatazwa kuoa wake wengi?

Tupe mstari

Na ndiyo maana nakushauri ufanye tafiti ujue chanzo cha ndoa moja kwenye ukristo kimetokea wapi na huwezi fanya tafiti kama husomi, maana Yesu hawezi kukupa majibu ya maswali haya ndotoni mkuu.

Soma upate kuujua ukweli.
Msome David Gitari kwenye ‘Church and Polygamy’ kina kurasa 13 tu
Kipate hapa

Kama lugha itakuwa tabu niambie nijitahidi kukifasiri mkuu.
Dunia nzima Wanaume ndo wanaozaliwa wengi kuliko wanawake unalijua hilo
 
Back
Top Bottom