Kwa tamko la leo la Rais Samia, 'legacy' ya yule jamaa imezikwa rasmi

Kwa tamko la leo la Rais Samia, 'legacy' ya yule jamaa imezikwa rasmi

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Rais Samia alikerwa Sana na ubabe, ukatili, lugha kali na kuwadhalilisha watu kwenye majukwaa. Hakupenda pia dhulma za kisiasa.

Ndiyo maana leo ameamua kuikata rasmi utepe wa haki na uungwana. Kwa tamko hili jeneza la legacy Sasa imepigiliwa misumari ya kijerumani.
 
Sababu za Lema na Lisu kujibanza kwa wazungu zinadhidi kumalizwa, mikutano ya siasa imeruhusiwa, madai yote ya Lisu yamelipwa, kesi yenye kila aina ya ushahidi ya gaidi wa kuuwa viongozi wa serikali imefutwa.
Ngoja tuone kiki mpya watakayokuja nao .
 
Mhe rais Samia alikerwa Sana na ubabe, ukaliti, lugha kali na kuwadhalilosha watu kwenye majukwaa. Hakupenda pia dhulma za kisiasa.

Ndiyo maana leo ameamua kuikata rasmi utepe wa haki na uungwana.

Kwa tamko hili jeneza la legacy Sasa imepigiliwa misumari ya kijerumani.
Na hizo SGR,JNHP,ATCL,Masoko,Stendi kubwa kubwa,kutimua vyeti fake kama wewe na mengineyo ndio legacy yake!

Mama Legacy yake ni Bibi Tozo na Nyasafari [emoji22]!

Tatizo ni kwamba legacy ya Jembe JPM haifutiki kamwe!

Hata wewe muandishi unalielewa hilo na ndio maana mko kijiweni mpaka saa hii.
 
Watanzania ni shida sana. Yaani mama karuhusu mikutano ya hadhara, ambayo ilizuiliwa kinyume na Katiba ya Nchi, lakini watu wanaona kama Hisani fulani hivi.

Kwa maoni yangu, hapa hakuna chochote kilichoongezwa.
 
Watanzania ni shida sana. Yaani mama karuhusu mikutano ya hadhara, ambayo ilizuiliwa kinyume na Katiba ya Nchi, lakini watu wanaona kama Hisani fulani hivi.
Jini jiwe alivunja katiba. Mama hakupendezwa na jambo hili.

Ili asiwaudhi sukuma gang akatafuta janja ya kuondoa upuuzi huu kwa kutengeneza "fumbo" la maridhiano.

Sukuma gang mmepigwa chenga hatari
 
Hakuna Legacy iliopotea hapo ni kwamba Upinzani na CDM wameuvaa mkenge wa CCM. Kwanza huyo unaesema legacy yake imepigwa ukiangalia kwa jicho la tatu ndie alikua anauinua upinzani. Lakini kwa sasa kwa utawala huu wa Hangaya Upinzani kwishney, wameangukia pua, mikutano ya kupangiwa cha kuongea ni kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa.
 
Back
Top Bottom