Mh Rais ameagiza apelekewe ripoti ya kina nani waliyomteka na kumuua Mzee Meddy Kibao.....Kama Polisi wakishindwa basi tutakuwa hatuna jeshi kabisa ,kama issue ndogo kama hiyo wakishindwa vipi issue kubwa?
Kuwapata watekaji ni simple sana uki-envolve wataalam wa Cyber na watalam wa mitandao ya simu ,yaani ndani ya 3hrs tu unawapata watekaji wote maana walikuwa wanatumia simu means waliacha traces.
Hatua ya za kufanya:-
1. Kitengo cha Cyber Crime Central hapo na TCRA wakachukue real time triplets muda ambao bus likiwa linatoka Stand ,hapa manifesto waakikishe ilikuwa filled na yule mtekaji aliyekuwa ndani au abiria wahojiwe kujua yule mtekaji aliyekuwa ndani alipandia wapi,kama alipandia mwanzoni basi Watu wa Cyber/TCRA wachukue cells/sites dumps ambayo itakuwa na namba zote zilizokuwa covered maeneo ya magufuli stand.
2.Kisha wachukue tena Cells/Sites dump bus lilipotekwa hapo MJAPAN/TEGETA Complex ,hapa itacover sites zinazozunguka Tegeta/Bahari beach/Wazo/Boko/Ununio...Hapo inamaanisha hii dump ya pili itakuwa na numba zilizotoka mbezi+zilizopo maeneo hayo ya bus lilipotekwa.
3.Hatua ya tatu ni kufanya VLOOKUP -Hapo ni Microsoft Excel tu ,imatch numbers zilizokuwa Maguful stand na numbers zilizokuwa Tegeta wakati bus linatekwa ,hapa zitakazomatch ni zile ambazo zimetoka magufuli,hii inaamisha ndiyo watakuwa abiria wote waliotoka stand ya magufuli.
4.Baada ya watekaji kumchukua Meddy Kibao means bus likaendelea na safari na watekaji wakaondoka kuelekea Ununio then hapo wachunguzi wachukue cells/sites dump nyingine baada ya watekaji na bus kuondoka,then wafanye tena VLOOPUP ,hapa itamatch numbers zilizotoka magufuli/abiria ambao waliokuwa wanaenda tanga lakini baada ya bus kuondoka still zikasoma eneo hilo hilo la tegeta/boko/ununio/bahari beach ,hizo number zitakazomatch nidyo zitakuwa za hao watekaji maana ndiyo waliotoka magufuli na wakaishia tegeta/ununio/bahari beach.