Mikopo Consultant
JF-Expert Member
- Oct 28, 2024
- 529
- 1,150
Siasa ni mazungumzo kati ya pande mbili zenye mirengo inayokinzana, kwa lengo la kutafuta masuala kadhaa ya kuwaunganisha pamoja na hivyo kutatua migogoro.
Tanzania hakuna vikundi vya watu wanaobeba silaha (waasi) kukabiliana na serikali, bali kuna vyama vya kisiasa. Hii maana yake ni kwamba njia ya kutumia polisi wenye mitutu ya bunduki na vyombo vingine vya usalama kukabiliana na wapinzani, sio sahihi.
Kwa maneno ya Tundu Lissu hapo majuzi, kwenye ile hotuba yake ambayo mimi naiita ni funga kazi, iliyowafumba midomo mpaka wale vitatange, amesema kwamba Rais Samia aliwakatalia kutekeleza maridhiano.
Na mimi ndio hoja yangu kwamba, ikiwa kweli Rais Samia aliwakatalia CHADEMA baada ya kuwa nao kwenye mazungumzo marefu basi alifanya makosa makubwa sana ambayo yanaenda kuwa na madhara ya moja kwa moja kwenye yatayojiri kwenye majukwaa ya kisiasa mwaka 2025 na ambayo yameanza kujiri kwa kasi.
Ni kama sasa gari la CHADEMA limewaka kwa speed kali lakini wamekuja na Ajenda ya kuuzuia uchaguzi ambayo kwa aina ya uongozi mpya wa CHADEMA inaonekana wapo tayari kabisa kulala ulalo ulalo, kitu ambacho kinafanya huu mwaka kuwa wa kipekee sana.
Kwakuwa sasahivi huko duniani pamechafuka na wameingia madarakani viongozi waliochafukwa, CCM na Samia waondoe kabisa mawazo ya kutaka kupora uchaguzi na kutawala nchi kwa ujanja ujanja.
Samia na CCM wakubali kulamba matapishi yao ya kushindwa kukubaliana na Mbowe, mazungumzo na upinzani hayakwepeki kwa sasa kwa mustakabali wa amani ya hii nchi. Hoja za Tundu Lissu zina mashiko kwa kila mtu mwenye akili.
Na muwe makini CCM nawatahadharisha, msiende na masarumbesa ya fedha na vito vya thamani, anachukia rushwa huyoo!.
Zasubuhi