Kwa ulimwengu huu wa sasa Fani ya Procurement bado inafundishwa vyuoni kwa sababu gani?

Kwa ulimwengu huu wa sasa Fani ya Procurement bado inafundishwa vyuoni kwa sababu gani?

Mkuu, mimi niliwahi kufanya kazi katika construction industry kwa muda fulani. Nilichoshuhudia kwa muda wote huo ni kwamba, watu wa kidato cha nne na sio ndio wanafanya hizo kazi za manunuzi na sio graduates. Kwa mazingira ya Tanzania hiyo kozi ipunguze udahili wa wanafunzi.
Mkuu mbona Kuna mkunga ambaye hajui kusoma Wala kuandika na anazalisha vizuri je taaluma ya ukunga ifutwe?
 
Sio serikali ya Tanzania tu, Duniani kote 80% na zaidi ya bajeti inahusu matumizi ile je watu wanasoma ili kwenda kuajiriwa serikalini wafanye manunuzi?

Mtu aliesoma manunuzi akijiajiri anafanya kazi gani?
Kwenye manunuzi unafundisha vitu kama negotiation, tender, stores management, pricing sasa mtu mwenye ujuzi wa hivyo vitu hapo juu anashindwaje kujiajiri.
 
Sio kila kozi iliundwa ili mtu ajiajiri zingine zipo specific kwa ajili ya ku run organization
Katika Karne ya sasa lengo number moja la graduates wetu linapaswa kuwa kujiajiri. Endapo mtu atapata fursa ya kuajiriwa iwe kwa bahati mbaya sana, lakini the main target must be self employment.
 
Mkunga anaweza akajiajiri kwa taaluma yake hiyo. Sasa graduate wa degree ya procurement anawezaje kujiajiri akimaliza chuo?
mantiki yako ilikuwa kama kijana wa form four anaweza kufanya manunuzi basi hakuna aja ya kuwepo kozi ya procurement. Mimi nikakupa mfano Kuna wakunga ambao hawajui kusoma Wala kuandika wanaweza kusimamia zoezi la mjamzito kujifungua swali langu likawa je kozi za ukunga zifutwe.?

Back to your reply ni kuwa swala kujiajiri yoyote yule anaweza kujiajiri tena Kwa alisomea procurement ana advantage sababu kasomea negotiation skills, Tender, stores handling kwa hiyo ni maamuzi ya mhitimu kuchagua nini cha kufanya maana alichosomea ni applicable kwenye business nyingi.
 
Katika Karne ya sasa lengo number moja la graduates wetu linapaswa kuwa kujiajiri. Endapo mtu atapata fursa ya kuajiriwa iwe kwa bahati mbaya sana, lakini the main target must be self employment.
Sasa kila mtu akijiajiri Nani ataajiriwa? Na kwani huwezi chukua maarifa ukaenda kuyatumia kwenye fani nyingine kabisa?

By the way procurement inafundisha mpaka entrepreneurship
 
mantiki yako ilikuwa kama kijana wa form four anaweza kufanya manunuzi basi hakuna aja ya kuwepo kozi ya procurement. Mimi nikakupa mfano Kuna wakunga ambao hawajui kusoma Wala kuandika wanaweza kusimamia zoezi la mjamzito kujifungua swali langu likawa je kozi za ukunga zifutwe.?

Back to your reply ni kuwa swala kujiajiri yoyote yule anaweza kujiajiri tena Kwa alisomea procurement ana advantage sababu kasomea negotiation skills, Tender, stores handling kwa hiyo ni maamuzi ya mhitimu kuchagua nini cha kufanya maana alichosomea ni applicable kwenye business nyingi.
Exactly procurement inafundisha mpaka strategic Management, humo utakutana na mambo ya SWOT analysis ambayo kimsingi ndio moyo wa biashara yoyote ile duniani
 
Kwa hiyo mtoto wa mlala hoi aliesoma petroleum engineering na civili engineering anajiajiri vipi
Hili pia ni tatizo ambalo "policy makers" watu wanapaswa kulitolea ufafanuzi kaka mkubwa. Sisi waafrika sisi tuna matatizo sana. Tanzania kuna reserve gani ya petroleum mpaka kuwashawishi watoto wa walala hoi kusomea hizo kozi. Nchi za Afrika zinapaswa kwanza kutatua balaa la njaa kabla ya kuwaza hizo petroleum kama wazungu na waarabu. Wale suala la njaa walikwisha limaliza zamani sana ndio maana wanawaza mambo mazito mazito muda wote.
 
Sasa kila mtu akijiajiri Nani ataajiriwa? Na kwani huwezi chukua maarifa ukaenda
Mkuu, unaweza kuyachukua maarifa kutoka wapi kisha ukayatumia wapi kwa mfano? Alafu kama suala ni kupata maarifa tu, kwanini kusiwe na kozi tatu tu za kupatia maarifa? Kwanini kuna lundo la kozi?
 
Exactly procurement inafundisha mpaka strategic Management, humo utakutana na mambo ya SWOT analysis ambayo kimsingi ndio moyo wa biashara yoyote ile duniani
Mkuu, kama hizo SWOT na strategic management hazimuwezeshi fresh graduate kujiajiri, it's nothing.
 
Mkuu, unaweza kuyachukua maarifa kutoka wapi kisha ukayatumia wapi kwa mfano? Alafu kama suala ni kupata maarifa tu, kwanini kusiwe na kozi tatu tu za kupatia maarifa? Kwanini kuna lundo la kozi?
Dah Kaka ningekutajia vitu ambavyo mtu wa procurement anasoma utashangaa
 
By the way procurement inafundisha mpaka entrepreneurship
At least hiyo entrepreneurship mngeiondoka kutoka ndani ya procurement kisha ikawa bachelor degree ya kujitegemea hapo ingekuwa na mantiki kidogo. Kwa mfano bachelor degree in Agriculture and Entrepreneurship au Bachelor Degree in mobile device repair and Entrepreneurship.
 
Back
Top Bottom