Uchaguzi 2020 Kwa Umati ule 'Kiduchu' wa kampeni ya Bernard Membe tena 'Kwao' Mkoani Lindi ni bora tu angeungana na Tundu Lissu na awe Mgombea Mwenza wake

Uchaguzi 2020 Kwa Umati ule 'Kiduchu' wa kampeni ya Bernard Membe tena 'Kwao' Mkoani Lindi ni bora tu angeungana na Tundu Lissu na awe Mgombea Mwenza wake

Membe hawezi siasa za majukwaani.Sio mtu mwenye maneno mengi,propaganda na fitina zakisiasa tena za upinzani.Kibaya zaidi yuko kwenye chama ambacho ndo kinajijenga.Kosa ambalo membe alilifanya ni kuridhika kuishi ndani ya Ccm na alishindwa kujua kua umaarufu wake ulibebwa na Ccm.alipaswa asome alama za nyakati mapema aanze kujijenga mwenyewe mapema akiwa bado ndani ya chama kama alivyofanya Magu.Magu alikua mjanja kujijenga mwenyewe mapema ndo maana sasa hivi chama ndo kinawajibika kwake badala yeye kuwajibika kwa chama.Kwahiyo umaarufu wa Magu ndio unaokibeba chama,yaani ukimchomoa magu kwenye hicho chama ccm inakua na wakati mgumu.Tofauti na Membe ukimchomoa kwenye vyama nisawa na ndege asiye na manyoya.
 
Mbinu nzuri sana imetumika,tayari pande mbili zimevolunteer ili kuizamisha majini ile pande nyingine ya pili,mchezo utaisha hivyo
 
Membe hawezi siasa za majukwaani.Sio mtu mwenye maneno mengi,propaganda na fitina zakisiasa tena za upinzani.Kibaya zaidi yuko kwenye chama ambacho ndo kinajijenga.Kosa ambalo membe alilifanya ni kuridhika kuishi ndani ya Ccm na alishindwa kujua kua umaarufu wake ulibebwa na Ccm.alipaswa asome alama za nyakati mapema aanze kujijenga mwenyewe mapema akiwa bado ndani ya chama kama alivyofanya Magu.Magu alikua mjanja kujijenga mwenyewe mapema ndo maana sasa hivi chama ndo kinawajibika kwake badala yeye kuwajibika kwa chama.Kwahiyo umaarufu wa Magu ndio unaokibeba chama,yaani ukimchomoa magu kwenye hicho chama ccm inakua na wakati mgumu.Tofauti na Membe ukimchomoa kwenye vyama nisawa na ndege asiye na manyoya.
Membe angetakiwa asubiri 2025 agombee ndan ya ccm, nguvu yake iko ndani ya ccm na sio nje
 
Chadema walihabgaika kumpata maalimu Seif na nkundi lake ili kujiimalisha zanzibar lakini anaonekana kuna agenda au malengo genge la mwalimu seif wanavyo ambapo wameona ndani ya Chadema malengo yao yatakuwa dissolved kama sio udini basi muungano other wise tungetoa chama kikubwa cha siasa kama ccm hivyo ndoto yakuwa na vyama viwili vya siasa ingetimia
Kwa sababu tumeshaanza kupenya Zanzibar inshallah azma yetu itatimia tu.

Muda utasema naamini uchaguzi huu tutakuwa na wabunge kutoka Zanzibar hata viti maalumu.
 
Hivi hujui hata mgombea mwenza anatakiwa awe na sifa zipi?halafu unajiona upo sahihi...
 
Membe alituaminisha kuwa kuna makada watano wabobezi from CCM wapo behind the scene, lakn mpak sa hv ni hollaa anafight alone agaist a well organised CCM.

Tatizo la CCM huwa wana umoja Sana linapokuja suala la uchaguz , umoja ni silaha kubwa Sana kweye masuala yyte ya kivita, hii infanya mifumo yote ya nchi inaelekezwa kuifavour CCM , kuanzia vyombo vya usalama, asasi za kiraia , matajiri wakubwa , mashirika binafs na ya uma, katika mazingira haya ni ngumu Sana kutoboa kwa mpinzan.

Kwa sasa mwamko wa upigaji kura ni kama haupo hasa maeneo ya mijini watu kama Wana harakat zao za maisha tofaut na 2015 , hii inaonyesha CCM wanashinda asubhi tuu, ...... Kama ni suala la nyomi hakuna anayeweza vunja rekodi ya Lowassa

Umoja wa ccm hauletwi kwasababu ya umoja wa kisiasa, bali madaraka ya mwenyekiti wake ambaye ni mkuu wa vyombo vya dola. Hivyo kila mtu anayetegemea kufanya siasa kwa mbeleko ya vyombo vya dola na taasisi za kimamlaka ni lazima awe ccm. Kutokana na uhusiano wa vyombo vya dola na taasisi za kimamlaka, ni rahisi makundi mbalimbali kama wafanyabiashara nk kwa kutaka au kulazimishwa, ni lazima waiunge mkono ccm ili kubaki salama baada ya uchaguzi.

Halafu acha upotoshaji wa kijinga, nyomi ya 2015 haikuwa kwasababu ya Lowassa, bali ilikuwa ni hamasa ya kisiasa iliyojengwa na Dr. Slaa mara baada ya uchaguzi wa 2010-2015. Hata watu kujiandikisha ilikuwa ni kwamba mgombea wa ccm atakuwa Lowassa ili watu wamchinje, hapo ndio kitambulisho cha kura kiliitwa kichinjio. Haya yanayomkuta Membe, hata Lowassa yangemkuta, tena mabaya sana, iwapo angeenda chama tofauti na cdm. Alaaniwe Mbowe na genge lake kwa kuchukua vipande 30 vya fedha vya Lowassa, na kumpa huyo mzee muhuni nafasi ya kugombea cdm.
 
Wewe nyumbu kweli, hujui hata sheria ya uchaguzi. Mgombea mwenza anatoka sehem moja ya Muungano na mgombea urais?

Ndio maana mpo kushangilia tu ujinga mnaolishwa na mgombea urais wenu na kuamini atashinda mropokaji yule

Mpaka hivi leo nawaza na ninamtafuta huyu Mtu ( Mtanzania ) aliyemdanganya kabisa wazi wazi Bernard Membe kuwa ana 'Mvuto' wa 'Kisiasa' na kwamba 'akigombea' Urais nchini Tanzania kwa Kushindana na 'Mwamba wa Chato' Rais Dkt. John Magufuli na CCM yake (yangu) anaweza 'Kumshinda' na kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kama kuna Mtu aliyeona Mkutano wake wa Kampeni Bernard Membe tena Mkoani Kwake kabisa(Chimbukoni) huko Lindi na kwa ule Umati 'Kiduchu' alioupata ni kheri tu angejiunga na CHADEMA au kungekuwa na Makubaliano 'Maalum' baina ya CHADEMA na ACT-Wazalendo ili Yeye ( Membe ) awe Mgombea Mwenza wa Tundu Lissu kidogo kungekuwa na 'Ushindani' wa uhakika wa Kisiasa.

Watanzania siyo Mangumbaru na Mapopoma yaani 'Wamchague' Mtu ambaye hata Kwao tu 'hakubaliki' kivile na wala hana 'Mvuto' ule wa Kisiasa.
 
Haya mambo ya umati yana faida zake kisiasa lakini ukweli yana danganya sana wanasiasa. kwenye miji na majiji ukichambua umati, unaweza pata waliojiandikisha kupiga kura ni watu wachache sana.
Umati hai ni umati wa vijijini.
 
Membe anasumbuliwa na “ego” anajiona kama vile alidhulumiwa nafasi ya urais iliyokuwa ni haki yake mwaka 2015.

Pia alijiandaa kwa kuchangisha pesa nyingi za nje hivyo imembidi aingie kwenye kugombea urais ili waliompa hizo pesa waone zikifanyiwa kazi wakati huu wa kampeni.
 
Haya mambo ya umati yana faida zake kisiasa lakini ukweli yana danganya sana wanasiasa. kwenye miji na majiji ukichambua umati, unaweza pata waliojiandikisha kupiga kura ni watu wachache sana.
Umati hai ni umati wa vijijini.

Umati unadanganya wagombea. Pale wengine ni wezi wa simu, wengine pale ni sehemu za kupata wachumba, wengine wanakwenda kushangaashangaa kila wanachokiona.
 
Membe angetakiwa asubiri 2025 agombee ndan ya ccm, nguvu yake iko ndani ya ccm na sio nje
2025 kwa CCM atawekwa muislam ( anaweza kutokea Zanzibar pis akiwepo ).
Tatizo humu kumejaa sana vitoto vya mwaka 2000
 
Umati unadanganya wagombea. Pale wengine ni wezi wa simu, wengine pale ni sehemu za kupata wachumba, wengine wanakwenda kushangaashangaa kila wanachokiona.
Hilo ni kweli mkuu na kuna wengine wanapenda kukusanyika sehemu yenye watu wengi na wengine wanachukulia ni sehemu ya kwenda kujichanganya wengine ngoja na mimi nikashangae maana sina kazi ya kufanya.
 
Back
Top Bottom