ki2c
JF-Expert Member
- Jan 17, 2016
- 7,719
- 14,506
Mmmmh....! labda na overrate nguvu ya IGP bila kujua zaidi.Mkuu ki2c Siro hana mnyororo wowote wa kuweza kum save pale anapokumbana na rungu la boss wake. Kumbuka jeshi la polisi ni kubwa, na lina makamanda wengine ambao huenda wanakubalika ndan ya jeshi hilo zaidi ya vile anavyokubalika Siro. Raisi ni mkuu wa nchi, ni amiri jeshi mkuu na boss wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama. Kwa maana hiyo ana mkono wake katika kila idara ya usalama nchini (watu wake wa kumpa taarifa nyeti kimya kimya). Kwahiyo Siro anaweza kuona amezungukwa na makamanda ambao yeye anahisi ndio backup wake wa kumpambania pale anapofikwa na tatizo, kumbe nyuma ya pazia hao hao makamanda anaowategemea ndio wanaopeleka taarifa zake kwa boss wao (raisi) Kinachomsaidia Siro ni aina ya raisi. Amekuta raisi Samia sio mtu wa kukimbilia kukurupuka kisa tu kasikia mtu anamuongelea mafumbo katika radio, tv au chombo chochote cha habari. Laiti kama raisi Samia angekuwa mtu wa kuchukua hatua kwa kila sauti anayoisikia inamsema yeye, au kumhukumu kila anaelalamika kama ilivyo kwa Siro, basi angekuwa ashafunga na kufukuza wengi ndan ya serikali, chama na uraiani. Maana wenye kulalamika ni wengi na sauti za kejeli dhidi yake anazisikia na kuzipuuza. Kuna makamanda wa polisi walikuwa wazito na wenyeji ndani ya jeshi hilo kama vile kina Mahita, Mwema nk. Lkn leo hawapo na maisha yanaendelea kama kawa. Hata mkuu mungine wa polisi Ernest Mangu juzikati alitumbuliwa na hakuna alie mkwamisha mtumbuaji. Kwahiyo jamaa amepata bahati ya kuongea mambo yake chini ya uongozi wa raisi mvumilivu na mstahamilivu. Lkn angekuwa ni yule wa kutumia nguvu zake moja kwa moja basi Siro angeisha na angeshangaa wanaompa mpa support wangemkimbia. Maana hakuna ambae angekubali kuupoteza ugali wake kwa ajili ya muungine.