The Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 11,099
- 13,709
Niseme wazi. Hata wakati wa utawala wa chama kimoja, ilikuwa nadra kwa mgombea urais kushinda karibia aslimia mia. Hii ilitokea hata wakati ambapo mgombea husika alikuwa akigombea na kivuli kama ilivyokuwa kwa Mwalimu Julius Nyerere na waliofuatia kabla ya kuanzisha mfumo wa vyama vingi ambao umekosa maana katika baadhi ya nchi kama vile Equatorial Guinea, Kameruni, Rwanda, Tanzania, na Uganda.
Kwa kuangalia 'ushindi' wa kishindo na kichawa wa Samia, naweza kusema kuwa anakubalika kuliko marais wote ulimwenguni kwa sasa. Tumpe maua yake basi. Samia hoyeee! Uchawa hoyeee! Ushindi wa kimiujiza na kishindo hoyeee!