Kwa wale ambao hamna maelewano mazuri na wazazi wenu

Hili ni tatizo kwa sisi wazazi wa kiume, hata mm nimepitia hili Kuna kipindi nilikosa viatu na shati la shule kuchanika halafu mzee akawa anapiga misele tu Hana time na mm.
Ujue nilijua hili tatizo labda la kutokuelewana na mzee ni la kwangu pekee yangu.. form four nzima nimetumia uniform za washikaji,,, namaliza shule ,, matokeo hayakuwa poa sana mzazi anakwambia toka nyumbani kwangu kwani wewe sio mwanangu nenda kamuulize mama yako baba yako ni nani…..
 
Waafrika tumekua malimbukeni wa dini, mbona wazungu hawana maadili kabisa kwa issue za wazazi wao ila wanazidi kupaa ila sisi tunaojifanya tunajua sana maadili ndio umasikini wa kutisha!!

Biblia mbona imesema kuwa wazazi wasichokoze watoto Bali wawalee katika maadili meaning wakifeli Hilo jukumu obviously laana haiwezi kuwa reliable maana Kila kitu kina Haki na wajibu.

Mfano mzazi wangu alikua hafurahii mafanikio yangu yaani hata nikiwa chuo nikifaulu hawezi nipongeza. Nakumbuka nimepata ajira ya kwanza akanuna hata simu hapokei!! Nakumbuka hata siku naenda interview alininyima nauli na hakupokea simu sema ni vile tu bahati nasibu nikafanyiwa interview kwa simu!!. Na kabla sijapata kazi nlikua nmejiajiri Bado akawa ananikashifu kuwa siwezi fika kokote, nikaanza kuingiza pesa akaanza nifokea kuwa niache hiyo kazi hata kama inanipa Hela ila sio ya mtu mwenye degree!! Hahahah kazi Nako nikapata akanizimia simu!!

Kuna wakati huwa sielewi shida ni nini Hawa wazazi alafu Kuna mpuuzi anasema eti sijui utalaaniwa??

Hapo sijaongelea mama mzazi kabisa ambaye alikua hataki hata nilipiwe ada. Mimi sijawahi mwambia mtu Nina mama Wala kumpost sijui nani kama mama maana nikikumbuka niliyopitia huwa sihesabu kama nina mama. Tukiwa wadogo alikua yupo radhi tulale njaa Ila yeye ashibe!!

So kama Mungu ni mwenye haki kweli sidhani atapokea laana za watu wenye Roho za Giza kama hizo.
 
Huyo bibi na shangazi ni wapare?
 
Dah pole Sana mkuu
 

Nakuelewa brother
 
Pole sana mkuu, inahuzunisha
 
Duh wazazi wengine mizunguo kweli[emoji848]
 
Hahahaha
 
Amezaa huko kwingine?
 
Hii ni kawaida kwa mabinti kuchukiwa na mama zao. Wala usijali sana. Ukitaka nikupe mifano 5 kutoka wanachama wa JF ambao mama zao wa kuwazaa wanawachukia bila sababu, nitakupa
Lete hiyo mifano mkuu
 
Je yeye babaako anakumiss?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…