Kwa wale ambao hamna maelewano mazuri na wazazi wenu

Watoto wanaopendwa ndo huwa wanaharibika
 
Ubinafsi tu, mimi baba amelelewa na wazazi wawili na babu na bibi wanajali hasa , sasa kama umelelewa vizur roho ya kumtelekeza mtoto unatoa wapi kama si ubinafsi,
Mi nasema mtu ukikoroga ukazaa na mtu mkatibuana effect usihamishe kwa watoto,
Umejuaje kama baba kukutelekeza? Ukute mama ndo kakunyima nafasi ya kumjua
 
[emoji16][emoji16][emoji16] mkuu elezea kidogo
 
Analewa?
 
Hivi kwanini wababa huwa wanawazingua watoto wa kiume[emoji16][emoji16]
 
Mkuu kwani uliwakosea nini? Baba na mama wote wakuchukie?au ulikuwa mtukutu?
 
OK mkuu
 
[emoji16][emoji16][emoji16] mkuu elezea kidogo
Mkuu kuna mambo hata nikikuambia unaweza ukapinga kabisa kwamba mzazi anaweza kufanya hivi kwa mwanae tena wa kumzaa. Ni mambo ya ajabu sana yani. Mimi naweza hata kumaliza mwaka bila kuwasiliana na Mzazi wala ndugu yeyote,kwanza hakuna anaejua mahala nilipo.
 
Again hapo hauongelei mfumo dume. Kuwa muelewa. Mfumo dume ni mfumo unaomtambua kama baba kiongozi wa familia na mama msaidizi wake.

It means wote wanashirikiana. So kama mwanaume analeta ubabe hiyo sio structure ya mfumo dume bali hilo ni tatizo binafsi la muhusika.
 
Kama umelelewa vizuri huwezi elewa vile watu wanapitia. Nimesoma visa vingi hapa nikamshukuru Mungu kwamba sikuwahi pitia waliyoyapitia. Familia yetu haina ugomvi hata chembe tunaishi peace sana.
Pole kwa wate wanaopitia changamoto na wazazi wao.
 
Mleta mada soma waefeso imeandika "ninyi kina baba msiwachokoze watoto wenu"... Mungu aliona upuuzi wa wazazi kujigeuza miungu kisa kwenye amri zake tumeamrishwa kuwatii wazazi. Mimi binafsi sina tatizo na wazazi wangu maana mapema sana nilishagundua kasoro nikaamua nisamehe kabisa kiroho safi na kwenda nao kijanja. Wakati natoka home kuja Dar kusaka LIFE sikua hata na nauli. Mzee mimi nilishamfuta kwenye ishu za kumwomba hela tangu niko Advance. Nakumbuka niliomba mama anikopeshe nauli nitamlipa baada ya wiki 1. Na kweli wiki ilivyopita akakumbusha deni ikabidi nilipe. Kimsingi nilikuwa na sababu nyingi sana za kuwapotezea wazazi ila nikawaza mambo mengi mno na kuamua kupotezea. Watu wote hawako sawa. Wazazi wengi sana wanalalamika kutelekezwa ila ukichunguza chanzo ni wao wenyewe.
 
Baba Yako na baba yangu ni mapacha... mwambie baba Yako ana pacha wake Ambae ni baba angu...!
 
Baba Yako na baba yangu ni mapacha... mwambie baba Yako ana pacha wake Ambae ni baba angu...!
Tuwapotezee tu maana wanatia hasira. Mimi nimeamua tu kwenda naye kijanja maana bado kuna mambo ya kifamilia anahitajika. Na kama Mungu ashatubariki hakuna haja ya kupambana na mzazi ila muhimu tu ajue misimamo yako kuwa HUTAKI MAMBO YA KIFALA KWA SASA.
 
Ila naomba maelekezo unaishije nae kijanja...Mimi nashindwa kabisa kujizuia najikuta sitaki kabisa mawasiliano yoyote na yeye...ebu nifundishe unavyo ishi na mzazi wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…