Kwa wale ambao hamna maelewano mazuri na wazazi wenu

Dawa ya moto moto.
Ujinga na upumbavu wa kukumbatia nge vimewaua wengi sana.
Mzazi mshenzi kaa naye mbali.
Mimi father simpendi.
Kati ya watoto wake 3 ambao tulimaliza la saba siku moja Mimi pekee aliniombea nifeli na cha ajabu ni Mimi pekee nikatoboa tena shule ya vipaji maalumu.
 
Mkuu kwani kutokuelewana na heshima mbona ni vitu viwili tofauti... Kutokuelewana ni hali ya ninyi wawili kutokwenda njia moja ila heshima ni tabia.

Unaweza usielewane na kiongozi wako ila kutokana na nafasi yake ukatii maelekezo (ukamuheshimu)

Kuelewana na kutokuelewana ni suala la kawaida kwenye maisha, Hata wewe mwenyewe unaweza ukakosa kuelewana na Mungu wako kutokana na kutokuelewa njia zake ila Heshima ikabaki palepale kutokana na ukuu wake.

Kuelewana na Kutokuelewana kunajengwa na hoja na utaratibu wa kuendana kinamna fulani wakati Heshima ni kutokana na tabia na mazingira ya makuzi fulani.
 
Haya Mambo Kama mtu hayajawahi
Kumkuta anaweza akaona watu wanaolalamika basi wanachekesha au wamechanganyikiwa,aisee hakuna kitu inaumiza au kumfanya mtu aone maisha machungu Kama kukosa upendo autakaye mtoto kutoka kwa mzazi wake
 
Ni Mimi mkuu. Siku hizi nimejitenga, Ni mwaka mmoja Sasa hawajui nilipo na Mimi sijui wapo hai au wamekufa and I don't care kwa sababu hakuna atakayeishi milele

Ila kwenye familia kuna mambo yanakera sana ,unatamani hata uzaliwe kwingine kumbe kila sehemu kuna shida,nadhan ni utu na upendo hawana
Toka uache kumshirikisha mambo yamenyooka?
 
Hili ni tatizo kwa sisi wazazi wa kiume, hata mm nimepitia hili Kuna kipindi nilikosa viatu na shati la shule kuchanika halafu mzee akawa anapiga misele tu Hana time na mm.
 
Hili ni tatizo kwa sisi wazazi wa kiume, hata mm nimepitia hili Kuna kipindi nilikosa viatu na shati la shule kuchanika halafu mzee akawa anapiga misele tu Hana time na mm.
Yani hyo kitu iko hata kwa wanyama wengine, madume hatunaga fikra za kusaidia au kusupport familia zetu.

Sent from my TECNO KG7h using JamiiForums mobile app
 
So sad

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Pole sana man,i can feel your pain bro
 
Kupitia uzi huu nimejifunza mambo mengi Sana nilidhan mm pekee ndyo napitia magumu ya familia yangu kumbe tupo wengi Sana

Kikubwa tuchukulie changamoto hizo tulizopitia kurekebisha familia zetu (watotowetu) tiwatendee mema tuwasikilize na tuwashaur vyema


Binafsi mzaz wangu wa kiume alinipa kila kitu kadir ya uwezo wake lakn kitu kimoja pekee udikteta Tena kwangu tuu kutonisikiliza Wala kinishirikisha kwa Jambo lolote badala yake wanasikilizwa watoto wengne na wanakaa nakupanga mambo ya familia mm naambiwa tu

Jambo hili lilinipa msongo wa mawazo Sana ukizingatia mm nilikuwa mtoto mkubwa kat ya wote lakn n mtoto wa nje ya ndoa na nilijipeleka tu kwa baba yangu baada ya shida kuwa nyingi huko nilokokuwa nakaa (kwa Bibi) ujio wangu pale unaonekana uliharibu kanuni na taratibu zao lakn nifanye nn n mm shida zilinikimbiza wakat mzaz wangu anakila kitu alikuwa engineer wa tanroads mkoa X

Hali ya kutengwa kimaamuzi iliendelea had nilipofika chuo pesa za matumizi had nimpigie mdogo wangu ndyo itumwe ukimpigia mzee hapokei simu na akipiga atanilaumu kwanini nilimpigia mda wa kazi ukipiga jion atakuambia yupo na marafk zake nisimsumbue

Amekuja kustaafu mm nipo chuo mwaka wa 4 namalizia akawagawia wanae wote Kia's Cha pesa Kama 5M kwa kila mtu mm sikupata hata shilingi na hii nilikuja kuambiwa na mdogo wangu alikuja kufunga mzgo wa biashara akaniambia wewe pesa yako utafanyia Nini ? Ndipo nikajua kumbe wamepewa pesa

Lakn MUNGU n mwema maisha Sasa yanasonga Nina familia yangu najitahid kuilea kwa upendo ili nisije kosea Kama mm nilivyoona nakosewa

Kwa Sasa mzazi wangu anailaumu simshirikishi katika maamuz ya mambo yangu najitenga Sana na familia sipigi simu mara kwa Mara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya Mambo Kama mtu hayajawahi
Kumkuta anaweza akaona watu wanaolalamika basi wanachekesha au wamechanganyikiwa,aisee hakuna kitu inaumiza au kumfanya mtu aone maisha machungu Kama kukosa upendo autakaye mtoto kutoka kwa mzazi wake
Ukiacha yote aliyowahi kunifanyia ikiwa ni pamoja na haki ya kumjua baba lkn hii kauli ( NATAKA KUAGIZA GARI LINGINE KWA SASA HVYO SIWEZI KUKUTUMIA MATUMIZI HUKO CHUONI )ndio ilinfanya nione ilikua bahati mbaya sana yeye kunizaa ingawaje hata upendo wa kinafki nimeushindwa.

Yan una mzazi si fukara lkn unaishi maisha ya kuomba omba yeye yupo busy kuhangaika kulinda ndoa yake and worse yeye ni mama, boalra angekua baba huenda ningempa excuse kalishwa limbwa na mke wake sasa mama nae kapewa limbwata na mume wake aisee wazazi ni mtihan mkubwa

ITS SEVEN YEARS NOW NAONA VEMA KUKAA MBALI NAYE, YANI MZAZI ANAKUCHUKIA MPAKA HUELEWI ULIKOSEA NINi
 
Nimeipenda hii! Huu ndiyo ukweli, kwanini umtegemee mtoto atakayekurudi? Lazima mtoto atakuwa na kiyongo kwa vile ulimrudi akiwa mtoto ili kumrekebisha
 
Hii ni kawaida kwa mabinti kuchukiwa na mama zao. Wala usijali sana. Ukitaka nikupe mifano 5 kutoka wanachama wa JF ambao mama zao wa kuwazaa wanawachukia bila sababu, nitakupa
 
Aisee.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…