Kwa wale tuliowahi kwenda kwa waganga wa kienyeji, tukutane hapa

leta chozi la simba,mkojo wa nyenyere na njiwa aliyefiwa na mumewe...!!!
hapo ndipo utabloo.... ukihuliza unavipataje..?.hapo sasa ndio njia nyeupeee ya kpigwaaa....
 
Sitoi jibu la moja kwa moja kuwa nimewahi ama sijawahi...ila waganga wapo na uganga upo...africa tulikuwa na mila za kiganga...wazungu wakaziboresha...tulitumia miti shamba wao wakatuletea madawa lakini waliyaboresha kutoka kwenye miti shamba kuwa madawa...ila matibabu ni yale yale....ata mambo ya giza pia yapo....
 
Jirani yetu binti wao alisumbuliwa na maradhi, walihangaika hospitali zote , yule dada ilikuwa akisafiri to the moon ni ugonjwa wakupoteza fahamu.

Mmoja wa Sangoma alisema binti analogwa na wazazi wake. Wazazi wenyewe waliblow mapigo .
Hahahaha imebidi nicheke kwa sauti!!....
 
Umerudi nyumbani ulipoitwa na mama na ajira umeshaitwa kazini???
 
Niliwahi kwenda kwa sangoma kutaka kubadili roho mbaya ya bwana yule iwe nzuri,akanipa masharti ya kupeleka mbuzi wa kijani mwenye mistari ya njano,bado namtafuta mbuzi
Huyo hawezi kukusaidia. Siunaona kakutuma kitu kisichopatikana! Muulize wa kuchora anafaa?.
 
sasa kama hutakaa ukanyage uko kwanini waulizia mambo ya uko?...ya kaisari muachie kaisari atiii yakheee
 
Kumbe kuna wanaume nao huwa wanaroga??
Mapenzi mamaa.
Usiombe yakakukuta.
Mpinzani wangu alikuwa ana hela.Mimi sina.alaf demu kanimwaga.nilikuwa nikiwaona wapo wawili roho inauma kweliii.nikaona hapa msaada ni nguvu za Giza.nilifanikiwa kumrudisha.ila sikumpenda kama mwanzo.maana nilijua ule upendo hautoki moyoni mwake.ni dawa tu zimempumbaza.muda wowote anaweza kuondoka.na ndicho kilichotokea.
 
Maisha haya kila mtu ana Siri zake nilishawahi kwenda mdogo wangu alikuwa Mgonjwa hospitality wenyewe walishauri tuanfalie njia nyingine. Ndiyo tulienda huko
Mlifanikiwa baada ya kufuata njia nyingine.?
 
Nilipelekwa na mganga mtoni maeneo ya Msambiazi kwenye zile kona,mganga akaita mamba mtoni akaniambia nimkalie kichwani,wakati akifanya hivyo alikuwa amenishika nisikimbie.
Yaliyotekea ...nilijikuta kibenderani (polisi)nahojiwa kwa kosa la kushambulia na kutaka ku uwa
 
Hahahaaa huyo kweli sangoma
 
Mapenzi yalinipeleka huko nilipopigwa chini nikageuza mteja nikihakishiwa atarudi nikasubiria jibu sikufanikiwa aliolewa huko jumla, toka hapo sina imani tena na watu hao,na niliapa sitogusa wala kukanyaga kwa mganga,nikukumbuke nimeliwa hela nyingi na sikupata msaada,ila sipingi wala kudharau mambo ya waganga kwa wanaoamini sababu ile ni imani kila MTU anavoamini.Me naamini ktk laws of nature ,naamini ktk positive thinking.
 
We jamaa mshenzi, hahahahah sema mnawaoneaga sana wadada na wamama!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…