Kwa wale waliopunguzwa kazini (USAID na wengine)

Inategemea uko wapi!! Debe ina kilo 20, ukicheza vizuri hadi kwa 30 unapata, mmezoea kununua zile za korie au mama alaska
Na hapa ndo ndoa nyingi zitavunjika. kuna watu wagumu sana kubadilika hata kama mazingira yamebadilika. mama akishaona umepoteza kazi anaanza kukitembeza uko nje au anakula kona mazima.
 
Mzee Kichuguu hongera.wewe haujapunguzwa bila shaka.chapa kazi.
 
Asante mkuu
 
Ni kweli, discipline ya hali ya juu ndo inahitajika, ukicheza kidogo umeyumba
 
Jamaa yangu kitengo cha HIV TAKWIM wameambiwa warudi kazini. Kuna mambo mengi watu wanapats taarifa magazetini, na wengine walifurahia wenzao kutemeshwa mzigo na trump.
 
Au mambuzi eti
Direct hires wote wamekua placed kwenye administrative leave, tena ni 90 days miezi mitatu tu, na kitita. Wale ambao ni special function tena wakutumwa si waajiriwa direct wengi wanaendelea na kazi, kama kusambaza dawa au kusambaza vyakula, au zile tasks tofauti.
Sasa kama wewe ni muajiriwa wa mkataba wa USAID na upo upo, unataka kuchomoa hela nssf, uumjinga sana. Na ushauri wako kwa watu wa vitumbua sijui mchele kilo moja, embu acha hizo basi.
Marekani inaangalia uwezekano wakuweka ofisi hiyo vizuri na si retrenchment. Embu katafute waajiriwa ambao ni wachache sana kwa bongo. Sidhani jf watakuwepo. Wakueleze. Na uache story hizi. Kuna mmoja anaitwa salma madini yupo instagram follow kwa bongo hapo. Ana gari lina jina lake kabisa anaishi goba. Nenda akueleze.
 
Mpaka 30 unanunua, mwezi wa 5 kuweni makini nunueni mpunga muweke ndani, ukiagiza pale Isaka kahama na uziri pale magari mengi yanapita, usafiri ni rahisi.
Sitawafundisha kila kitu
😹😹😹 Kwahiyo tutoke dar tukasubiri mpunga shambani tena Mwanza ili tupate kwa bei ndogo.!! Ujue wewe unachekesha.!!

Hizo nauli na gharama za kusafirisha debe la mpunga kutoka Mwanza kuja dar, unajua utakuwa umepata madebe mangapi ya mchele? 😹

Mbona unatuletea hesabu za kitoto mkuu, hebu wewe kukubali tu umepuyanga..!! Hakuna wa kukuchapa hapa wote watu wazima.!!
 
Yaani huna hela alafu ukatafute grade 1??? Ila wanawake mnarudisha nyuma maendeleo, tena huo sio wenye chenga kwa taarifa yako, huo dukani kwa mangi unauzwa 1700 kwa kg, ww unanunua jumla
Yaani hapo kama ni mume umeoa,hakyanani lazima upitie changamoto, wanawake wengi sana watazinguana na waume zao kuhusu kuji-adjust waendane na kipato kilichopo.Bodaboda,dereva bajaji na wengine,wakae vizuri kusaidia hizi familia.
 
Mdogo wangu, amka usingizini acha kujipa moyo, ofisi zimefungwa hiyo ndio fact, rudi kwenye uhalisia, kubali hali yako, acha kujificha kwenye keyboard
 

Mie sijawahi kwenda mkoani kununua nnaagiza,
Ishi na watu vizuri ndg,
Mimi nina marafiki wengi tu wanasafiri kila siku,
wengine safari za kazi,
wengine binafsi, nina marafiki wengi tu madereva wa maroli
Ishi na watu vizuri
 
Mie sijawahi kwenda mkoani kununua nnaagiza,
Ishi na watu vizuri ndg,
Mimi nina marafiki wengi tu wanasafiri kila siku,
wengine safari za kazi,
wengine binafsi, nina marafiki wengi tu madereva wa maroli
Ishi na watu vizuri
Ilitakiwa uelezee pia kwenye hiyo mchele debe 35 unatakiwa kuishi na watu vizuri, uwe na marafiki madereva malori na wasafiri ili kusiwe na gharama za nauli..!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…