Kwa wale waliowahi kutunza siri nzito kwa muda mrefu tukutane hapa

Kwa wale waliowahi kutunza siri nzito kwa muda mrefu tukutane hapa

Kuna siri nyingine ninazo hadi nikianza kuziwaza naogopa mwenyewe.
Watu wamekua wakijiamini Sana wakikaa na Mimi kuongea mambo yao.
Nyingine nashindwa kuzibeba hadi nakua Kama mgonjwa ila ndo inakua siri tena nashindwa kuzitoa.
Kuna muda natamani ni mwambie MTU asiongee au kufanya kitu mbele yangu sababu ananipa mzigo wa kuanza kufikiria ila nakaa tu.

Wengine nawaulizaga hivi unajiamini nini kufanya/kuongea hiki mbele yangu.
Naomba nikutafute uniadithie angalau 2 au 3 ili nikupunguzie mzigo.
 
Siri nyiingi saana nlishaambiwa,tatizo nakosa uvumilivu,nakereka saaana moyoni[emoji3]hadi nasema
Nlisha itwa mmbeya,msabasi chakubimbi[emoji17]Lkn kwangu naona sawa tu
Kwenye vikao vinavyofanywa kwa siri,wakiniona tu wananifukuza[emoji17]
Unaendaga kuwasimulia rafiki zako au[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ngoja nikuitie warumi nae hawezi tujza siri
 
Mim siwezi kutunza siri, memory ya kuhifadhi data ya kichwa changu kina mambo ya msingi sana ya kuhifadhi..

Siri kesho yake unakuta nimesha sema..

Mim nilisha wahi kumwona mama na mtoto wake wa kike wanamfukia kitoto kichanga.. Usiku hawakuniona kesho yake mapema nikaenda kulisanua..

Nikaja nikumwona msichana mmoja jirani alikuwa akiishi na mdogo wake wa kike dada mtu alikuwa ni fundi wa kushona alikuwa mjamzito ila hakuna aliekuwa anafahamu hakuwa anatoka nje ya nyumba hadi siku anajifungulia nyumbani mdogo wake yupo shuleni, mtoto akamtupa chooni nikashtuka nikalisanua

Kuna jamaa mmoja alikuwa na grosary yake ya kuuza pombe, ilikuwa karibu na kituo kikubwa cha polis, kumbe nyuma yake mchizi alikuwa anauza madawa ya kulevya, wacha nije nilisanue, kumbe pimbi alikuwa na connection na askari wa pale akaja kunshtukia wacha ale sahani moja na mim, wacha nilisanue karibia kituo kizima cha polis walihamishwa na ule mkoa nikahama mazima
Hapa ulifanya vizurii tena ulitakiwa uwaambie pale pale wanaomfukia mtoto ili kuokoa maisha ya mtoto,au ungepiga kelele
 
Hapa ulifanya vizurii tena ulitakiwa uwaambie pale pale wanaomfukia mtoto ili kuokoa maisha ya mtoto,au ungepiga kelele
Mtoto alikuwa amesha fariki tayari, mtoto wa week moja,

Ila kesi iliendeshwa kiajabu ajabu, mara upelelezi hujakamilika mara upuuzi mtupu, watu walidakwa sana wa majirani sijui ile kesi ilikuja kufia wapi
 
Binadamu katika mazingira mbali mbali,ukumbana na majanga mbali mbali ambayo mengine ni hatari kabisa,
Kuna waliowahi kushuhudia mtu kiauawa na kukaa kimya
Kuna waliowahi kuona mtu anamloga mwingine wakatunza siri,
Kuna waliowahi kuona mwenzao anaibiwa wakakaa kimya,
Kuna waliowahi kushuhudia mtu anabakwa wakakaa kimya,
Kuna waliowahi shuhudia mtu au mke wa mtu anatembea na mwanaume mwingine wakakaa kimya,

Mi siri yangu ambayo sitakuja kuisema ni kamba nilimfumania mjomba mkubwa akiwa anatembea na mke wa mjomba mdogo alafu wakajua kwamba nimejua sikuwahi kuisema ilikanusha, yapata miaka 20 sasa,
Leo kuna rafiki yangu amenambia kwamba akiwa mdogo alimuua mtu akiwa Croatia mwaka 1994 , na hakuna aliyejua,

Mwingine (dr) akasema kuwa amewahi kumuinject mgonjwa UKIMWI kupitia syringe, na akakaa kimya maana alilipwa Hela ya kutosha


Najua na wee una siri umetunza tudokeze
Sio siri tena iyo
 
Kuna mshkaji wangu alipigika kishenzi akawa weechat ,kumbe kuna mzungu anatafta wanaume wa kuwabandua ilikuwa mwaka 2014/5 kitu kama hicho , sasa jamaa alikuwa kapigika hana hela, katika kuchati weechat akamuona mzungu men, akamwambia nataka nyuma nakupa dollar 200 jamaa hakuchelewa, sasa siku moja nikamuomba simu yake yangu iliisha chaji, katika kupekuwa nikakuta meseji ya makubaliano ya kubanduliwa, nilishangaa sana nikaziangalia tena na tena, baadae kumrudishia simu yake na wala sijawahi kumwambia mtu yeyote yule, hata yeye sikumwambia kama nimejuaa ila nilimshusha value tokea siku hiyo nikahama na chumba nkazuga shangazi kaniita
What the FCCUK!
 
Back
Top Bottom