Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Kwa kifupi sana.tupe walau kwa uchache mkuu.
Maishani mwangu sikuwahi kuona mwanamke wa Kizungu akinyanyaswa kwa kila hali na mumewe tena mume wa kiafrika. Lakini Kwa Dr.Kobello nimeshudia.
Pamoja na kusoma sana na kuwa Daktari wa Binadamu, Kobello hakuwa mfano wa kuigwa, alikuwa karibu kila siku jioni utamkumta Bar, Glocery nk akinywa Bia mpaka mapovu ya Bia kufunika ndevu na mwisho alikuwa akirudi nyumbani na kumpiga na kumdhalilisha mkewe tena mbele ya watoto wake wa watatu wakiume ambao mwisho wa siku wawili kati yao walikuwa wakimfanyia hivyo hivyo mama yao na mwisho anasemekana walikuwa wakimbaka pia.
Ni zaidi ya Laana.
Dr.Kobello alikuja kufariki 1990s, kisha mkewe akiteswa sana na watoto wake wawili wakifuata tabia za baba yao naye Huyo mama akafariki baada ya muda mfupi, Akafuata mtoto wa kwanza ambaye alikuwa Teja naye akafariki na Mwisho akafuata mtoto wa Pili(Steven) naye akafariki inasemekana kwa kuuwawa baada ya kuiba na
kukamatwa.
Mtoto wa Mwisho ndiye pekee aliyebakia ambapo ndugu zake wa mbali kutoka Dar walikuja na kumchukua.