Kwa wale waliozaliwa na waliowahi kuishi Tabora, tukumbushane vituko vya Mboka

Kwa wale waliozaliwa na waliowahi kuishi Tabora, tukumbushane vituko vya Mboka

umenikumbusha mbali sana, yani milambo secondary enzi hizo, tulikuwa tunajiita milambo mens, kwenye umiseta au mchakamchaka tukikutana na tabora boys tegemea ngumi kali sana, nawakumbuka warsaw ndo walikuwa mapozeo yetu, nani anamkumbuka mwalimu msemakweli ( Milambo sec), namkumbuka Nehemia msechu mkurugenzi wa NHC kwa sasa na Magesa Mlongo ( Mkuu wa mkoa wa Arusha) wote tulikuwa tunapiga nao ngema, Deusidedit Kibamba ( mambo ya katiba kama sikosei) na kumbukumbuka mwalimu wangu wa chemistry Mr. Kyala, ilikuwa raha sana kipindi kile, na tuligoma mwaka 94 mgomo ulifanikiwa na kumuondoa mkuu wa shule (mr. Msemakweli) enzi zile za Dr. lawrence Gama ( Mungu amlaze mahala pema peponi amin)


Kweli unamkumbuka mwita waibe na mwembe kunyonga, unakumbuka mgurunde cup fainal 1994? kuna wachezaji km KIMTI, GOLIATH MWAKIPESILE, METHOD, na wengine kipindi kile ALLY MAYAI alikuwa UYUI, mihayo alikuwapo VICTO KILOWOKO.
 
kaka Bijou, wewe hujakaa tabora, tuliokaa kule tabora inafahamika kama mboka, ukiwa wilayani watu wakienda tabora mjini utasikia naenda mboka, ni kama watu wa mikoani wakija dar husikii wakisema dar wanasema bongo, sasa ndio na tabora inaitwa jina la mboka enzi na enzi, chanzo sijajua mie nimelikuta na kuliacha
 
[Kweli unamkumbuka mwita waibe na mwembe kunyonga, unakumbuka mgurunde cup fainal 1994? kuna wachezaji km KIMTI, GOLIATH MWAKIPESILE, METHOD, na wengine kipindi kile ALLY MAYAI alikuwa UYUI, mihayo alikuwapo VICTO KILOWOKO.]

kaka mshino nawakumbuka wote naona anayesikika ni ally mayai tu wengine sijui walipo, Goliathi alikuwa ni rafiki yangu sana na nimesoma na mdogo wake hapo hapo milambo akiitwa tuntufye mwakipesile, jamaa alikuwa ni pande la mtu, kama goliathi wa kwenye biblia,
 
Mkuu Uko sahihi kabisa! Mimi sikutaka kuizungumzia sn Hiyo familia ila naifahamu vzr sn!

Wale watoto Wa Kobelo walikua na Akili sn shuleni Lkn walivyokuja kuharibika Yani ilikua hovyo kabisa!

Yule mama Wa Kirusi ukikutana nae sokoni alikua anatia Huruma sn! Hivi Kwanini Warusi hawapendi saidia raia wao wakiwa away?

Mkuu mkewe na Dr. Kobelo si Mrusi ila ni Mhungary na ndiko Dr alikosomea. Baada ya Dr. Kufariki ile family ilisambaratika. Ingawa Dr. alishahama nyumbani kabla baada ya vurugu alizokuwa anamfanyia yule Mama,
watoto wale wa kiume walimpiga baba yao na kumfukuza nyumbani kwake Cheyo. So ni kama laana fulani hivi. Maana baadaye wale wawili wakubwa ni mama yao ndo aliwafunga gereza la Uyui kutokana na vituko vyao. Nawafahamu hawa watoto tokea wako Mwenge Primary wakishikwa mikono kupelekwa shule. Siku nilipopata story yao nilisikitika sana. Walikuja Tanzania wanaongea kihungary hata kingereza walikuwa hawakijui vizuri.
 
Mkuu Uko sahihi kabisa!

Unamkumbuka dr Azizi? Dr Othman?
Haswa. Nimekuwa nikimwita Dr.Aziz kwa jina la Dr.Mohamed kwa kuwa mmoja wa watoto wake alikuwa akiiitwa Mohamed ambaye nilifahamiana naye kwa karibu sana.

Dr.Azizi sawa na Dr. Othman na Dr.Kisenge ndio madaktari waliokuwa na Zahanati zao binafsi wakiziendesha wao wenyewe binafsi mjini Tabora.

Dr.Aziz alifariki mwaka jana mwezi wa April jijini Mwanza baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Huyu Daktari angekuwa mbali sana kimaisha kama angepangilia maisha yake vizuri.
Ndio Daktari pekee enzi hizo Tabora sikuwahi kumwona akiwa Bar, Glocery nk akinywa pombe. Alikuwa muungwana sana na aliyependa kuonekana kijana na mtanashati japokuwa tayari kiumri alikuwa mtu wa makamo.
Tatizo lake kubwa ni Ndoa za mitaala, rasmi nilikuwa najua ana wake wawili lakini alikuwa ana watoto wengi sana na wote walikuwa wanamtegemea kiuchumi.
 
Nilikua nakaa kule juu mlimani Filter!

Namkumbuka sn John Shija mkulu!
Mkuu Ntuzu mbona huyo John Shija yupo Dar miaka tu.
 
Zanzibar -ASP

Yule mtoto wa kwanza wa Dk Kisenge anaitwa Rodrick Kisenge yuko wapi ? Na Dk Kasele bado yuko hai ?

Zanzibar-ASP Dr. Rodrick Kisenge si mtoto wa kwanza. Ni mzaliwa wa tatu. Anatanguliwa na dada zake wawili ambao walishaolewa zamani ndo maana unadhani yeye ni wa kwanza.
 
kaka ntuzu nawakumbuka sana, unamkumbuka na mwalimu machibya, na mwalimu camilius ( kwa sasa angeitwa sharobaro) Rwabukoba, mwalimu njile mbabe anakwambia kubhyula sio kuona, unapakumbuka kwa mama joha jirani na madarasa ya egm



Ticha Rwabukoba ameshakuwa marehemu sasa yapata miaka mi3 au mi4 hivi iliyopita! Baada ya shule za kata kufumuka alihamishwa Milambo na kwenda kuwa mkuu wa shule moja wapo ya kata pale Tabora mjini.
 
Duhh!
Haki ya mama meja na mimi na jamaa wengine tulikuwa tunazichanga halafu tunaingizana pale African hotel.
Nyama choma kwa fujo!

Kuna siku yule Dr kabelo alileta Soo pale! Akaanza kutukana kina dada flani pale. Eti kwa sababu yy ni bingwa wa kuzalisha pale Tbr lazima atakuwa kaishaona zile nyeti za hao kina dada wanaoringa!

Nilimkata kofi mpaka chini! Paka shume yule! Sijui nae bado yuko hai!?

Teh teh teh teh!

Dr. Kobelo kazichomoa sana mimba za wanafunzi Tabora.
Alikuwa anasema kumdu mkewe lazima alewe kwanza. Ila inasikitisha mkewe na watoto wote waliishia kuwa machizi sijui ni bangi au Mungu alimuadhibu kwa kuua vichanga maelfu.
 
Tehtehtehteh... sio mimi bwana, mie nilikuwa mtoto wa geti kali, uncle wangu alikuwa meneja wa RTC Tabaora wakati aunt alikuwa mwl kazima sec, alikuwaje mkali!

Mwalimu nani huyo? Atakuwa alinifundisha aisee.
 
Zanzibar -ASP

Yule mtoto wa kwanza wa Dk Kisenge anaitwa Rodrick Kisenge yuko wapi ? Na Dk Kasele bado yuko hai ?
Dr.Rodrick Kisenge kwa sasa ni daktari Bingwa wa Watoto pale Muhimbili, ni mtu mkubwa sana pale Muhimbili, nimekutana na vijana kadhaa wanaosoma udaktari pale Muhimbili wakisema Dr.Rodrick ni Lecturer wao na mkuu wa idara ya Paediatric pale Muhimbili.

Dr.Kasele mpaka sasa sijui yuko wapi.
 
Umesoma kazima mamii? Utakuwa ulifundishwa na shangazi yangu, alikuwa mwalimu pale kazima secondary

NiPM jina lake basi, au hata useme alifindisha masomo gani na miaka.
 
haaaahhaah Taradadi yule wa Urambo?alikuwa na kama mwarabu fulani na ana manyoya kama nyani nakumbuka cc tulikuwa tunamwita taradadi manyoya alikuwa na sifa ya kungonga wasichana sana kipindi cha UMITASHUMTA
Aah nimecheka mpa basi. Taradadi alikuwa ni mwalimu wa primary school sikimbuki jina. Lakini pia alikuwa ni kocha wa mchezo wa riadhaa. Pia alikuwa ni mwalimu kwenye magwaride ya chipukizi. Siku hizi naona yamekufa. Ila mara ya mwisho nilimsikia kwenye radio kipindi cha michezo akiongea kama Afisa Utamaduni nadhani ni Manispaa ya Tabora kuhusu maandalizi ya mchezo wa riadhaa.
 
Haswa. Nimekuwa nikimwita Dr.Aziz kwa jina la Dr.Mohamed kwa kuwa mmoja wa watoto wake alikuwa akiiitwa Mohamed ambaye nilifahamiana naye kwa karibu sana.

Dr.Azizi sawa na Dr. Othman na Dr.Kisenge ndio madaktari waliokuwa na Zahanati zao binafsi wakiziendesha wao wenyewe binafsi mjini Tabora.

Dr.Aziz alifariki mwaka jana mwezi wa April jijini Mwanza baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Huyu Daktari angekuwa mbali sana kimaisha kama angepangilia maisha yake vizuri.
Ndio Daktari pekee enzi hizo Tabora sikuwahi kumwona akiwa Bar, Glocery nk akinywa pombe. Alikuwa muungwana sana na aliyependa kuonekana kijana na mtanashati japokuwa tayari kiumri alikuwa mtu wa makamo.
Tatizo lake kubwa ni Ndoa za mitaala, rasmi nilikuwa najua ana wake wawili lakini alikuwa ana watoto wengi sana na wote walikuwa wanamtegemea kiuchumi.


Mkuu aliyefikwa na mauti akiwa Mwanza mwaka jana ni Dr Othman yule mzenji aliyelowea Tabora. Dr Aziz ni yule msomali ambaye alikuja kufungua ofisi yake pale Alipokuwepo Dr Mhina baada ya Dr Mhina kuhamia Dar.

Kwenye List ya madaktari waliokuwa na dispensary zao ongezea Dr Mhina na Dr Liwa.
 
Zanzibar -ASP

Yule mtoto wa kwanza wa Dk Kisenge anaitwa Rodrick Kisenge yuko wapi ? Na Dk Kasele bado yuko hai ?

Zanzibar-ASP Dr. Rodrick Kisenge si mtoto wa kwanza. Ni mzaliwa wa tatu. Anatanguliwa na dada zake wawili ambao walishaolewa zamani ndo maana unadhani yeye ni wa kwanza.

Mrigariga uko sawa kabisa.
Dr.Kisenge ana watoto wakubwa wa kwanza wakike. Nafikiri mmoja alikwenda kuloea ughaibuni kati ya ulaya na Amerika.
 
Last edited by a moderator:
Duhh anti kutaja hayo mambo ya geti kali.

Umenikumbusha jamaa yangu mmoja alikuwa na ndege wake kule Cheo karibu na kambi ya jepshi.
Mtoto geti kali kiroho mbaya!

Sasa jamaa siku moja kanipitia nimsindikize. Manake ndege ilimuahidi kukutana nyuma ya nyumba magharibi time!

Basi wakati tunaenda tukakosea step tukapita maeneo ya jeshi!
Weeee!

Kulirukishwa kichura kama hatuna akili nzuri!

Kitokeo cha hapo. Breki ya kwanza isevyaaaa kwenda kutafuta supu ya makongoro! Pale karibu na Mzee makubeli!

Manake miguu ilikuwa inauma kishenzi!

Teh teh teh teh!

Cc manumbu1

aisee umenikumbusha mbali, wenyewe tulikuwa tuna kamtindo ka kumshikisha mtu pembe. Unakubaliana naye lkn hutokei.

Huyo ni Juma Makuberi nini? Yaani those were the days.
 
Last edited by a moderator:
vinaitwa viziizi kuna ndege wengi we acha tu! jolowe,mkongotoro,zonzi,kajole,katyente,dede,tetere,wanya nyanda,chozi,etc.yaani nimewinda na manati,ungo,ulimbo,mkupuo na wavu hadi namaliza form 4!

Yaani unatamani siku zirudi. Nikiwaangalia watoto wetu na maplay station yao nawaonea huruma kweli.
 
Back
Top Bottom