Kwa wale waliozaliwa na waliowahi kuishi Tabora, tukumbushane vituko vya Mboka

Kwa wale waliozaliwa na waliowahi kuishi Tabora, tukumbushane vituko vya Mboka

Aisee kwanza hilo jina sijawahi kulisikia kwingine kokote, Taradadi; umenikumbusha mbali sana mkuu, for sure huu uzi nimeukubali.

cc Ntuzu

Mwanangu sio Siku zote mijadala mizito tu ya siasa! Lazima tuwe na vitu vyepesi vya kujadili vinavyogusa maisha yetu!
 
Last edited by a moderator:
Very true. Ilikuwa ni huzuni kubwa sana. Nikikumbuka sometimes nahisi machozi kunitoka.

Mkuu jipe Moyo ndivyo wanadamu tulivyo!

Mkuu Nahisi km ulikua jirani na Hiyo familia?
 
Disco la mwanaisungu, tabora hotel.
Basketball kwenye grounds za uhazili.
Nani alisoma mwenge, kipindi cha mwalimu chiboni?

Kaunga mimi nimesoma Uyui Secondary. Nimesikitika umezungumzia basketball halafu ukasahau kuitaja shule yangu. Kama kweli ulisoma Mwenge Primary umeisahauje Uyui Sec?! Kituo cha kuzalisha wachezaji basketball Tanzania? Nani anamkumbuka marehemu hawa Meja na Byera Kaneno (RIP). Ambaye alikuja kuchezea Bees. Uhazili palikuwa na mwalimu pale ambaye alikuwa kocha wa basketball. Jina lake Kansolele... Huyu bwana alikuwa ni giant ktk viwango vyote. Mguu wake alikuwa size 15. Sijawahi kumuona akivaa viatu vya ngozi zaidi ya rubber za Pony na Converse.
 
umenikumbusha mbali sana, yani milambo secondary enzi hizo, tulikuwa tunajiita milambo mens, kwenye umiseta au mchakamchaka tukikutana na tabora boys tegemea ngumi kali sana, nawakumbuka warsaw ndo walikuwa mapozeo yetu, nani anamkumbuka mwalimu msemakweli ( Milambo sec), namkumbuka Nehemia msechu mkurugenzi wa NHC kwa sasa na Magesa Mlongo ( Mkuu wa mkoa wa Arusha) wote tulikuwa tunapiga nao ngema, Deusidedit Kibamba ( mambo ya katiba kama sikosei) na kumbukumbuka mwalimu wangu wa chemistry Mr. Kyala, ilikuwa raha sana kipindi kile, na tuligoma mwaka 94 mgomo ulifanikiwa na kumuondoa mkuu wa shule (mr. Msemakweli) enzi zile za Dr. lawrence Gama ( Mungu amlaze mahala pema peponi amin)
 
*TABORA NA MADAKTARI.
Nikiwa Tabora katika miaka ya 1980s na 1990s nilifanikiwa kufahamu mengi kuhusu Madaktari wa binadamu na maishha yao, kwa kifupi nina wakumbuka hawa zaidi. Dr.Kisenge, Dr.Kobello, Dr.Mohamed.

Kwa mfano Dr.KISENGE
Alikuwa na zahanati yake katikati ya mji pembeni mwa jengo la kampuni ya sigara ikitazamana na Jengo la shirika la Bima(NIC) na benki ya zamani ya CRDB(Benki ya ushirika na maendeleo vijijini).
Alifariki 1994.
Watoto wake watatu wakaja kuwa madaktari Dar, Mmoja Dr.Sabuni(Ni daktari bingwa wa watoto pale Muhimbili), Dr.Peter Kisenge(Ni Daktari bingwa wa Moyo pale Muhimbili) na Dr.George(Ni daktari wa Mifugo, yuko Dar akifanya biashara ya vipuri vya Magari Kariakoo).

Yupo mtoto mwingine wa Dr.Kisenge anaitwa Endrew kwa sasa yupo Dar anakula bata tu, yeye ni kupiga hela na kuponda raha, enzi zile kila mrembo mkali aliyekuwa Uhazili jamaa alikuwa anamsaka kwa udi na uvumba, muda mwingi alikuwa akiendesha Kwa kasi Pikipiki Kubwa XL ya Ofisi(Zahanati), Gari ya Baba yake(Pigot 504) na baadaye alinunua Carina yake Nyekundu ili kusaka warembo, jambo la ajabu ni kuwa marafiki zake aliokuwa nao Tabora na baadhi ya warembo wengi wa Uhazili walikufa kitambo sana kwa Ukimwi lakini huyu jamaa inadaiwa mara zote alipopimwa alikuwa yuko Fit kabisa!!
 
nakumbuka na urambo enzi hizo primary nilikuwa kazaroho kule kaliua, vijiji kama igwisi, Usimbe, imalamakoye, na igagala, ilikuwa raha sana, nikikumbuka nilivyokuwa nakula karanga vibaya sana kuzidi na panya buku, baadae nikaenda malizia shule 1 urambo vijijini inaitwa Songambele, kule nikakutana na matunda yanaitwa mantonga, we acha tu, hukumbuki ka kuna chocolate au mkate, vijijini raha sana, nakumbuka kijiji cha uyogo, jionee mwenyewe, kalemela, na ulyankulu, ila matunda kama mantonga nilikuwa nayapenda sana na sijui kama bado yapo, wtu wa tabora mtujulishe jamani miezi gani yanakuwepo hayo matunda nataka kurudi tabora jamani dah
 
Kwa mnaokumbuka Tabora Boyz miaka ya 70s na Mh. Ma------ meya wa dar es salaam leo kuna bibi alikuwa mpishi pale jikoni akiitwa Khadija Kibadeni.
 
kaka znz asp umenikumbusha mbali sana manake watoto wa dr. kisengi walikuwa ni hatari, wale jamaa walikuwa ni zege halilali, kwa kweli walikamua vibaya mno uhazili, new comer yoyote atatoa tu, na enzi zile waliokuwa wanamiliki magari walikuwa ni wachache, mie nilikuwa milambo, siku akili imechoka naingia zangu pale jirani na uhazili kulikuwa na vioski ( mkwakwani) nikitizama mabinti wanaoingia na kutoka roho yangu inasuuzika narudi zangu milambo sekondari manake kule tulikuwa madume tu, nikijisikia kurefresh naenda hapo mkwakwani nakumbuka ndio jina la vioski vya pale getini uhazili
 
Duh!! Wewe unakumbuka sana shule ya Mazoezi Mwenge. Huyu Mwalimu Chiboni alikuwa headmaster, alikuwa anajua kiingereza kizuri na fasaha sana but alikuwa Mlevi wa Pombe, Alikuwa mwenyeji wa Dodoma(Mgogo) na mara ya mwisho nilimwona 1993 Salanda-Dodoma nikipita na treni akiwa hana chochote.
Pia kulikuwepo na walimu wengine kama:
1/Mwalimu Shigela(Inadaiwa huyu mama alianza kufundisha na Nyerere enzi za Mkoloni, alinifundisha kusoma na kuandika!!)
2/Mwalimu Mihayo.
3/Mwalimu Pongo(Nilisikia huyu mama alikufa kwenye ajali ya Mv Bukoba 1996)
4/Mwalimu Husein.
5/Mwalimu Maduhu.

Sijui kama unakumbuka ile mihogo mizuri ya kupikwa iliyokuwa na Pilipili ikiuzwa wakati wa break?

Mihogo ya Mzee mmoja akiitwa Mzee Jaffari. Nasikia alifariki miaka ya mwanzoni mwa 90 hivi. Then mwanae akaja kuendeleza hiyo biashara. Sasa sijui kama hiyo recipe waliiendeleza maana ile mihogo ina historia ndefu. Inasemekana Mzee huyo alianzia kuuza mihogo hiyo Kazima Sec. wakati huo Uyui Sec haijajengwa bado. So ni miaka mingi sana. Angezaliwa nchi kama America angekufa tajiri maana hiyo mihogo ingekuwa branded na kupewa trademark. Story ya huyu Mzee wa mihogo na ya Col. Saunders mwanzilishi wa KFC zinafanana sana tofauti ni wametoka mabara mawili tofauti.
 
*TABORA NA MADAKTARI.
Nikiwa Tabora katika miaka ya 1980s na 1990s nilifanikiwa kufahamu mengi kuhusu Madaktari wa binadamu na maishha yao, kwa kifupi nina wakumbuka hawa zaidi. Dr.Kisenge, Dr.Kobello, Dr.Mohamed.

Kwa mfano Dr.KISENGE
Alikuwa na zahanati yake katikati ya mji pembeni mwa jengo la kampuni ya sigara ikitazamana na Jengo la shirika la Bima(NIC) na benki ya zamani ya CRDB(Benki ya ushirika na maendeleo vijijini).
Alifariki 1994.
Watoto wake watatu wakaja kuwa madaktari Dar, Mmoja Dr.Sabuni(Ni daktari bingwa wa watoto pale Muhimbili), Dr.Peter Kisenge(Ni Daktari bingwa wa Moyo pale Muhimbili) na Dr.George(Ni daktari wa Mifugo, yuko Dar akifanya biashara ya vipuri vya Magari Kariakoo).

Yupo mtoto mwingine wa Dr.Kisenge anaitwa Endrew kwa sasa yupo Dar anakula bata tu, yeye ni kupiga hela na kuponda raha, enzi zile kila mrembo mkali aliyekuwa Uhazili jamaa alikuwa anamsaka kwa udi na uvumba, muda mwingi alikuwa akiendesha Kwa kasi Pikipiki Kubwa XL ya Ofisi(Zahanati), Gari ya Baba yake(Pigot 504) na baadaye alinunua Carina yake Nyekundu ili kusaka warembo, jambo la ajabu ni kuwa marafiki zake aliokuwa nao Tabora na baadhi ya warembo wengi wa Uhazili walikufa kitambo sana kwa Ukimwi lakini huyu jamaa inadaiwa mara zote alipopimwa alikuwa yuko Fit kabisa!!

Mkuu Uko sahihi kabisa!

Unamkumbuka dr Azizi? Dr Othman?
 
Kuna Matunda huenda yako Tabora tu, kwa mfano Ntalali, Mbuguswa, Mamtonga nk.
Nilijaribu kuyatafuta mikoa mingine lakini sikufanikiwa.

Umesahau nsalansi zinapatikana Itetemia. Wakati bado mapori nasikia siku hizi ni mji umejengeka mpaka kufika karibia na Kipalapala Seminary.
 
Zanzibar -ASP

Yule mtoto wa kwanza wa Dk Kisenge anaitwa Rodrick Kisenge yuko wapi ? Na Dk Kasele bado yuko hai ?
 
umenikumbusha mbali sana, yani milambo secondary enzi hizo, tulikuwa tunajiita milambo mens, kwenye umiseta au mchakamchaka tukikutana na tabora boys tegemea ngumi kali sana, nawakumbuka warsaw ndo walikuwa mapozeo yetu, nani anamkumbuka mwalimu msemakweli ( Milambo sec), namkumbuka Nehemia msechu mkurugenzi wa NHC kwa sasa na Magesa Mlongo ( Mkuu wa mkoa wa Arusha) wote tulikuwa tunapiga nao ngema, Deusidedit Kibamba ( mambo ya katiba kama sikosei) na kumbukumbuka mwalimu wangu wa chemistry Mr. Kyala, ilikuwa raha sana kipindi kile, na tuligoma mwaka 94 mgomo ulifanikiwa na kumuondoa mkuu wa shule (mr. Msemakweli) enzi zile za Dr. lawrence Gama ( Mungu amlaze mahala pema peponi amin)

Yule Mwalimu Wa Frech Wa Milambo alikua mrefu hivi rai Wa Rwanda alikua anaitwa Sijui Ruta! Na marehemu Mabuye!

Mwalimu Omari Yule Wa Mihayo hasa kwenye michezo Unamkumbuka?
 
Asante sana.
Hiyo Familia ya Dr.Kobello ilikuwa familiy friend kwetu.

Aiseee pole sn!

Mkuu Nahisi tunaweza tukawa tunafahamiana kabisa! Maana kwa vijana Wa mboka Wa miaka Hiyo kujuana ilikua Lazima!
 
Wakuu salama?

Nimeona tukumbushane mambo na vituko vya mboka na story kibao za mkoa ule! Na mitaa, matunda ya porini km Magongoti, vijana Wa mboka, Mwanaisungu etc.

Wakuu Mwenye story ya mboka Au Mwenye chochote kile aje tupige porojo kidogo!

natokaea tabora, hiyo Mboka WALA sijawahi kusikia
 
Ntabaye namfahamu alikuwa jirani yetu. Ninachokumbuka, tulienda kwake kusali jumuiya akatutoa baru, kuwa hamuhitaji Yesu wetu. Lkn Mungu si ntabaye, mumewe Mungu alivyomchukua, akaanzaje kusali.
Kaunga. Kama Ntabaye (The Advocate) alikuwa jirani yenu ina maana umeishi maeneo ya Kazima au Railway college. Maana hiyo familia naifahamu. Na mimi nilikuwa jirani nao.
 
waswezi unawakumbuka? nimesoma uyui na gongoni, uhazili nimecheza basketball, disco la muungano mess nimecheza. makokola je, vipi?
Lukansola Uyui ulisoma miaka gani?
 
kaka ntuzu nawakumbuka sana, unamkumbuka na mwalimu machibya, na mwalimu camilius ( kwa sasa angeitwa sharobaro) Rwabukoba, mwalimu njile mbabe anakwambia kubhyula sio kuona, unapakumbuka kwa mama joha jirani na madarasa ya egm
 
[
quote_icon.png
By Zanzibar-ASP
Kuna Matunda huenda yako Tabora tu, kwa mfano Ntalali, Mbuguswa, Mamtonga nk.

Nilijaribu kuyatafuta mikoa mingine lakini sikufanikiwa.]

haya matunda niliyakuta kisiwa cha ukerewe, ntalali na mbuguswa, mantonga ni tabora tu sijaona pengine, na kulikuwa na samaki wanapatikana mto ugala wanaitwa wamejazia tumboni, jina limenitoka kama unawakumbuka nikumbushe basi, na sie tuliokaa vijijini urambo kuna mboga inaitwa nsansa, michembe na matobolwa, yani kule vijijini killa kitu ni natural
 
Back
Top Bottom