*TABORA NA MADAKTARI.
Nikiwa Tabora katika miaka ya 1980s na 1990s nilifanikiwa kufahamu mengi kuhusu Madaktari wa binadamu na maishha yao, kwa kifupi nina wakumbuka hawa zaidi. Dr.Kisenge, Dr.Kobello, Dr.Mohamed.
Kwa mfano Dr.KISENGE
Alikuwa na zahanati yake katikati ya mji pembeni mwa jengo la kampuni ya sigara ikitazamana na Jengo la shirika la Bima(NIC) na benki ya zamani ya CRDB(Benki ya ushirika na maendeleo vijijini).
Alifariki 1994.
Watoto wake watatu wakaja kuwa madaktari Dar, Mmoja Dr.Sabuni(Ni daktari bingwa wa watoto pale Muhimbili), Dr.Peter Kisenge(Ni Daktari bingwa wa Moyo pale Muhimbili) na Dr.George(Ni daktari wa Mifugo, yuko Dar akifanya biashara ya vipuri vya Magari Kariakoo).
Yupo mtoto mwingine wa Dr.Kisenge anaitwa Endrew kwa sasa yupo Dar anakula bata tu, yeye ni kupiga hela na kuponda raha, enzi zile kila mrembo mkali aliyekuwa Uhazili jamaa alikuwa anamsaka kwa udi na uvumba, muda mwingi alikuwa akiendesha Kwa kasi Pikipiki Kubwa XL ya Ofisi(Zahanati), Gari ya Baba yake(Pigot 504) na baadaye alinunua Carina yake Nyekundu ili kusaka warembo, jambo la ajabu ni kuwa marafiki zake aliokuwa nao Tabora na baadhi ya warembo wengi wa Uhazili walikufa kitambo sana kwa Ukimwi lakini huyu jamaa inadaiwa mara zote alipopimwa alikuwa yuko Fit kabisa!!