Kwa wale waliozaliwa na waliowahi kuishi Tabora, tukumbushane vituko vya Mboka

Kwa wale waliozaliwa na waliowahi kuishi Tabora, tukumbushane vituko vya Mboka

[
quote_icon.png
By Zanzibar-ASP
Kuna Matunda huenda yako Tabora tu, kwa mfano Ntalali, Mbuguswa, Mamtonga nk.

Nilijaribu kuyatafuta mikoa mingine lakini sikufanikiwa.]

haya matunda niliyakuta kisiwa cha ukerewe, ntalali na mbuguswa, mantonga ni tabora tu sijaona pengine, na kulikuwa na samaki wanapatikana mto ugala wanaitwa wamejazia tumboni, jina limenitoka kama unawakumbuka nikumbushe basi, na sie tuliokaa vijijini urambo kuna mboga inaitwa nsansa, michembe na matobolwa, yani kule vijijini killa kitu ni natural

Wanaitwa KuKuRu!

Ha ha ha haaaaaaa! Mambo ya Tbr Jamani hayo!

Samaki mzuri Lkn miba mingi sn!
 
Km ulikua unakaa Cheyo,Kitete,Gongoni, Kanyenye miaka ile ya 90 lazima Utakua ulisikia habari zao!

Kulikua na Dr pale Kitete Hospital alikua Maarufu Dr Kobello! Hujapata sikia Hilo jina?

kobelo alikuwa na kihospital chake bachu kwa ajili ya abotion nasikia Enzi hizo anatoa mimba wanawake kitoto kinatoka hai anakykabidhi uuwe mwenyewe....alikuwa chizi yule Baba.............Enzi hizo Tabora moses kulola anajaza watu viwanja vya uyui born again wa Enzi hizo.....nimekumbuka unyama wa Dr kobelo roho imeuma sana aisee.mkewe alikuwa kama chizi jamani
 
Kwa sana tu, duh. Wewe ulikuwa nyumba zipi?

Karibu na wale waburushi ndugu wa Rostam Aziz wakina kasel-kandis! Huku opposite na geti kuu la kuingilia kazima sekondari.Kwetu ni mtaa wa nyuma ya hao waburushi.Ingawa pia nilikuwa nikiishi national housing karibu na game ya wanyama wakati mwingine.
 
kaka Ntuzu, hasa, nilikuwa nawapenda sana hawa samaki, ukifika msimu wake nilikuwa nawala sana, nakumbuka na asali mbichi ya kutokea uyowa kule ulyankulu ndani kabisa, karibia na shinyanga,
 
kaka znz asp umenikumbusha mbali sana manake watoto wa dr. kisengi walikuwa ni hatari, wale jamaa walikuwa ni zege halilali, kwa kweli walikamua vibaya mno uhazili, new comer yoyote atatoa tu, na enzi zile waliokuwa wanamiliki magari walikuwa ni wachache, mie nilikuwa milambo, siku akili imechoka naingia zangu pale jirani na uhazili kulikuwa na vioski ( mkwakwani) nikitizama mabinti wanaoingia na kutoka roho yangu inasuuzika narudi zangu milambo sekondari manake kule tulikuwa madume tu, nikijisikia kurefresh naenda hapo mkwakwani nakumbuka ndio jina la vioski vya pale getini uhazili

Mkuu unachanganya. Watoto wote wa Dr. Kisenge hawana makuu. Ni watu very humble and down to earth. Huyo Andrew ndiye alikuwa na marafiki zake. Kundi lake hilo ukadhani wote ni watoto wa Dr. Kisenge. Huyu Andrew ndiye alikuwa anaitwa Raisi wa Kariakoo mwenye kampuni yake ya Andrew Traders akiimbwa sana kwenye mabendi na radio kipindi hicho Ngwasuma, Twanga Pepeta na Dj mmoja wa Radio One simtaji jina
 
Au Wewe ndio ulikamatwa kwenye mabweni ya Uhazili!

Teh Teh Teh Teh! Nakutania Mkuu!

Mambo ya mboka mengi sn Mkuu! Yani Bado watakuja watu humu na story nyingi sn za kila kona na kila kitu!
Ila Nahisi kabisa kumbe tunafahamiana!

kaka znz asp umenikumbusha mbali sana manake watoto wa dr. kisengi walikuwa ni hatari, wale jamaa walikuwa ni zege halilali, kwa kweli walikamua vibaya mno uhazili, new comer yoyote atatoa tu, na enzi zile waliokuwa wanamiliki magari walikuwa ni wachache, mie nilikuwa milambo, siku akili imechoka naingia zangu pale jirani na uhazili kulikuwa na vioski ( mkwakwani) nikitizama mabinti wanaoingia na kutoka roho yangu inasuuzika narudi zangu milambo sekondari manake kule tulikuwa madume tu, nikijisikia kurefresh naenda hapo mkwakwani nakumbuka ndio jina la vioski vya pale getini uhazili

Mkuu unachanganya. Watoto wote wa Dr. Kisenge hawana makuu. Ni watu very humble and down to earth. Huyo Andrew ndiye alikuwa na marafiki zake. Kundi lake hilo ukadhani wote ni watoto wa Dr. Kisenge. Huyu Andrew ndiye alikuwa anaitwa Raisi wa Kariakoo mwenye kampuni yake ya Andrew Traders akiimbwa sana kwenye mabendi na radio kipindi hicho Ngwasuma, Twanga Pepeta na Dj mmoja wa Radio One simtaji jina
 
kaka Ntuzu, hasa, nilikuwa nawapenda sana hawa samaki, ukifika msimu wake nilikuwa nawala sana, nakumbuka na asali mbichi ya kutokea uyowa kule ulyankulu ndani kabisa, karibia na shinyanga,

Hujawahi kula Nyama ya Nyati? Maana Uko Ulyankulu ndanindani ndio zilikua zinatoka!
 
Ntabaye namfahamu alikuwa jirani yetu. Ninachokumbuka, tulienda kwake kusali jumuiya akatutoa baru, kuwa hamuhitaji Yesu wetu. Lkn Mungu si ntabaye, mumewe Mungu alivyomchukua, akaanzaje kusali.
Kaunga. Kama Ntabaye (The Advocate) alikuwa jirani yenu ina maana umeishi maeneo ya Kazima au Railway college. Maana hiyo familia naifahamu. Na mimi nilikuwa jirani nao.

Aisee na ITEGAMATWI pia, isije ikawa tulicheza kombolela. Sitaki kuwafahamu aisee. LOL
 
Last edited by a moderator:
Kweli unamkumbuka mwita waibe na mwembe kunyonga, unakumbuka mgurunde cup fainal 1994? kuna wachezaji km KIMTI, GOLIATH MWAKIPESILE, METHOD, na wengine kipindi kile ALLY MAYAI alikuwa UYUI, mihayo alikuwapo VICTO KILOWOKO.

Chini ya Mwalimu Omari! Mihayo walikua na kadada hivi miaka Hiyo kwenye netball na Basketball kanaitwa Pewa keupe hivi na mwingine Joyce Masamalo! Unawakumbuka?

Hawa walikua hodari sn kwenye michezo!
 
Haswa. Nimekuwa nikimwita Dr.Aziz kwa jina la Dr.Mohamed kwa kuwa mmoja wa watoto wake alikuwa akiiitwa Mohamed ambaye nilifahamiana naye kwa karibu sana.

Dr.Azizi sawa na Dr. Othman na Dr.Kisenge ndio madaktari waliokuwa na Zahanati zao binafsi wakiziendesha wao wenyewe binafsi mjini Tabora.

Dr.Aziz alifariki mwaka jana mwezi wa April jijini Mwanza baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Huyu Daktari angekuwa mbali sana kimaisha kama angepangilia maisha yake vizuri.
Ndio Daktari pekee enzi hizo Tabora sikuwahi kumwona akiwa Bar, Glocery nk akinywa pombe. Alikuwa muungwana sana na aliyependa kuonekana kijana na mtanashati japokuwa tayari kiumri alikuwa mtu wa makamo.
Tatizo lake kubwa ni Ndoa za mitaala, rasmi nilikuwa najua ana wake wawili lakini alikuwa ana watoto wengi sana na wote walikuwa wanamtegemea kiuchumi.
Nimesoma nao kazima wale vijana. Inasikitisha sana maana walikuwa bright.
 
Chini ya Mwalimu Omari! Mihayo walikua na kadada hivi miaka Hiyo kwenye netball na Basketball kanaitwa Pewa keupe hivi na mwingine Joyce Masamalo! Unawakumbuka?

Hawa walikua hodari sn kwenye michezo!

Pewa jina lina ring a bell; kazima tulikiwa na one Joyce mzuri sana kwa basket lkn aliweza hata football. Kungekuwa na soka ya kike kama sasa angekuwa star.
 
Karibu na wale waburushi ndugu wa Rostam Aziz wakina kasel-kandis! Huku opposite na geti kuu la kuingilia kazima sekondari.Kwetu ni mtaa wa nyuma ya hao waburushi.

Kaselkandis ni binamu zake Rostam. Hiyo mitas unayoisema kulikuwa na mtu anaitwa Amin Imkana. Alikuwa anacheza mpira ni balaa. Ex Uyui huyo. Alipo kuja Dar mpira akaacha. Tabora ilitoa vipaji vingi sana hasa football na basketball.
Kama sikosei wewe ulikuwa jirani na Jaji Kwikima then alikuwa ni Advocate
 
[Kweli unamkumbuka mwita waibe na mwembe kunyonga, unakumbuka mgurunde cup fainal 1994? kuna wachezaji km KIMTI, GOLIATH MWAKIPESILE, METHOD, na wengine kipindi kile ALLY MAYAI alikuwa UYUI, mihayo alikuwapo VICTO KILOWOKO.]

kaka mshino nawakumbuka wote naona anayesikika ni ally mayai tu wengine sijui walipo, Goliathi alikuwa ni rafiki yangu sana na nimesoma na mdogo wake hapo hapo milambo akiitwa tuntufye mwakipesile, jamaa alikuwa ni pande la mtu, kama goliathi wa kwenye biblia,

Kilowoko ni Askari magereza mbeya! Alichezea timu Yao kule wakampa na kazi!
 
Jamani Makrina Ntabaye! Hako ndo kalikua katoto Ka Mwisho kwa Ntabaye!
Na ndiye aliyekuwa mzuri kuliko wote, sijui yuko wapi?
Nilikutana na binti ntabaye mmoja Dar, sikumbuki ni yupi ila sio Macrina.
 
Karibu na wale waburushi ndugu wa Rostam Aziz wakina kasel-kandis! Huku opposite na geti kuu la kuingilia kazima sekondari.Kwetu ni mtaa wa nyuma ya hao waburushi.

Kaselkandis ni binamu zake Rostam. Hiyo mitas unayoisema kulikuwa na mtu anaitwa Amin Imkana. Alikuwa anacheza mpira ni balaa. Ex Uyui huyo. Alipo kuja Dar mpira akaacha. Tabora ilitoa vipaji vingi sana hasa football na basketball.
Kama sikosei wewe ulikuwa jirani na Jaji Kwikima then alikuwa ni Advocate

Nimekula sana cheuros (sina uhakika na spelling) za waburushi wale. Kibinti chao kimoja nilisoma nacho.
Nawakumbuka pia watoto wa Kwikima kina Saada???? sijui wako wapi?
 
Ntuzu ngoja nikusahihishe kidogo.
Dr.Kobello alisomea Russia mambo ya Utabibu(MD) na akaoa mwanamke wa kizungu ambaye alizaa naye watoto watatu wa kiume na wote walikuwa Half-Cast na alirudi na kuishi Tabora akiwa na mkewe na watoto watatu.

Mama huyo wa Kizungu alikuwa mtaratibu na muungwana sana tofauti kabisa na mumewe Dr.Kobello ambaye alikuwa Mlevi Mbwa, mwenye dharau, malaya nk.
Watoto wake hawakuzaliwa machizi bali walikuwa na akili sana hususani mtoto wake wa Pili(Steven).

Lakini baadaye watoto wawili(Mtoto wa kwanza na wa pili(Steven)) walikuja kuharibika kabisa na kuwa kama machizi, Pombe, bangi na Unga vikiwa ndio chanzo kikubwa.
Kifupi Famili hii yote imeteketea kwa wote kufariki dunia kwa kipindi kifupi na amebaki mtoto mmoja ambaye ndio wa mwisho kuzaliwa.

Ni sad story nikiisimulia humu kwa kina hii familia namna ilivyopotea
Ntuzu please ebu tupe story kidgo ya famlia ya Dr Kobello!
 
Aisee na ITEGAMATWI pia, isije ikawa tulicheza kombolela. Sitaki kuwafahamu aisee. LOL

Kaunga hatukucheza wote. Binafsi miaka hiyo nilishakuwa A Level karibu namaliza Secondary Education.
 
Back
Top Bottom