[By Zanzibar-ASP
Kuna Matunda huenda yako Tabora tu, kwa mfano Ntalali, Mbuguswa, Mamtonga nk.
Nilijaribu kuyatafuta mikoa mingine lakini sikufanikiwa.]
haya matunda niliyakuta kisiwa cha ukerewe, ntalali na mbuguswa, mantonga ni tabora tu sijaona pengine, na kulikuwa na samaki wanapatikana mto ugala wanaitwa wamejazia tumboni, jina limenitoka kama unawakumbuka nikumbushe basi, na sie tuliokaa vijijini urambo kuna mboga inaitwa nsansa, michembe na matobolwa, yani kule vijijini killa kitu ni natural
Km ulikua unakaa Cheyo,Kitete,Gongoni, Kanyenye miaka ile ya 90 lazima Utakua ulisikia habari zao!
Kulikua na Dr pale Kitete Hospital alikua Maarufu Dr Kobello! Hujapata sikia Hilo jina?
Kwa sana tu, duh. Wewe ulikuwa nyumba zipi?
kaka znz asp umenikumbusha mbali sana manake watoto wa dr. kisengi walikuwa ni hatari, wale jamaa walikuwa ni zege halilali, kwa kweli walikamua vibaya mno uhazili, new comer yoyote atatoa tu, na enzi zile waliokuwa wanamiliki magari walikuwa ni wachache, mie nilikuwa milambo, siku akili imechoka naingia zangu pale jirani na uhazili kulikuwa na vioski ( mkwakwani) nikitizama mabinti wanaoingia na kutoka roho yangu inasuuzika narudi zangu milambo sekondari manake kule tulikuwa madume tu, nikijisikia kurefresh naenda hapo mkwakwani nakumbuka ndio jina la vioski vya pale getini uhazili
Mkuu unachanganya. Watoto wote wa Dr. Kisenge hawana makuu. Ni watu very humble and down to earth. Huyo Andrew ndiye alikuwa na marafiki zake. Kundi lake hilo ukadhani wote ni watoto wa Dr. Kisenge. Huyu Andrew ndiye alikuwa anaitwa Raisi wa Kariakoo mwenye kampuni yake ya Andrew Traders akiimbwa sana kwenye mabendi na radio kipindi hicho Ngwasuma, Twanga Pepeta na Dj mmoja wa Radio One simtaji jina
kaka Ntuzu, hasa, nilikuwa nawapenda sana hawa samaki, ukifika msimu wake nilikuwa nawala sana, nakumbuka na asali mbichi ya kutokea uyowa kule ulyankulu ndani kabisa, karibia na shinyanga,
Ntabaye namfahamu alikuwa jirani yetu. Ninachokumbuka, tulienda kwake kusali jumuiya akatutoa baru, kuwa hamuhitaji Yesu wetu. Lkn Mungu si ntabaye, mumewe Mungu alivyomchukua, akaanzaje kusali.
Kaunga. Kama Ntabaye (The Advocate) alikuwa jirani yenu ina maana umeishi maeneo ya Kazima au Railway college. Maana hiyo familia naifahamu. Na mimi nilikuwa jirani nao.
Kweli unamkumbuka mwita waibe na mwembe kunyonga, unakumbuka mgurunde cup fainal 1994? kuna wachezaji km KIMTI, GOLIATH MWAKIPESILE, METHOD, na wengine kipindi kile ALLY MAYAI alikuwa UYUI, mihayo alikuwapo VICTO KILOWOKO.
Nimesoma nao kazima wale vijana. Inasikitisha sana maana walikuwa bright.Haswa. Nimekuwa nikimwita Dr.Aziz kwa jina la Dr.Mohamed kwa kuwa mmoja wa watoto wake alikuwa akiiitwa Mohamed ambaye nilifahamiana naye kwa karibu sana.
Dr.Azizi sawa na Dr. Othman na Dr.Kisenge ndio madaktari waliokuwa na Zahanati zao binafsi wakiziendesha wao wenyewe binafsi mjini Tabora.
Dr.Aziz alifariki mwaka jana mwezi wa April jijini Mwanza baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Huyu Daktari angekuwa mbali sana kimaisha kama angepangilia maisha yake vizuri.
Ndio Daktari pekee enzi hizo Tabora sikuwahi kumwona akiwa Bar, Glocery nk akinywa pombe. Alikuwa muungwana sana na aliyependa kuonekana kijana na mtanashati japokuwa tayari kiumri alikuwa mtu wa makamo.
Tatizo lake kubwa ni Ndoa za mitaala, rasmi nilikuwa najua ana wake wawili lakini alikuwa ana watoto wengi sana na wote walikuwa wanamtegemea kiuchumi.
Aisee na ITEGAMATWI pia, isije ikawa tulicheza kombolela. Sitaki kuwafahamu aisee. LOL
Vipi kuhusu story za Fifi?
Chini ya Mwalimu Omari! Mihayo walikua na kadada hivi miaka Hiyo kwenye netball na Basketball kanaitwa Pewa keupe hivi na mwingine Joyce Masamalo! Unawakumbuka?
Hawa walikua hodari sn kwenye michezo!
[Kweli unamkumbuka mwita waibe na mwembe kunyonga, unakumbuka mgurunde cup fainal 1994? kuna wachezaji km KIMTI, GOLIATH MWAKIPESILE, METHOD, na wengine kipindi kile ALLY MAYAI alikuwa UYUI, mihayo alikuwapo VICTO KILOWOKO.]
kaka mshino nawakumbuka wote naona anayesikika ni ally mayai tu wengine sijui walipo, Goliathi alikuwa ni rafiki yangu sana na nimesoma na mdogo wake hapo hapo milambo akiitwa tuntufye mwakipesile, jamaa alikuwa ni pande la mtu, kama goliathi wa kwenye biblia,
Na ndiye aliyekuwa mzuri kuliko wote, sijui yuko wapi?Jamani Makrina Ntabaye! Hako ndo kalikua katoto Ka Mwisho kwa Ntabaye!
Karibu na wale waburushi ndugu wa Rostam Aziz wakina kasel-kandis! Huku opposite na geti kuu la kuingilia kazima sekondari.Kwetu ni mtaa wa nyuma ya hao waburushi.
Kaselkandis ni binamu zake Rostam. Hiyo mitas unayoisema kulikuwa na mtu anaitwa Amin Imkana. Alikuwa anacheza mpira ni balaa. Ex Uyui huyo. Alipo kuja Dar mpira akaacha. Tabora ilitoa vipaji vingi sana hasa football na basketball.
Kama sikosei wewe ulikuwa jirani na Jaji Kwikima then alikuwa ni Advocate
Ntuzu please ebu tupe story kidgo ya famlia ya Dr Kobello!Ntuzu ngoja nikusahihishe kidogo.
Dr.Kobello alisomea Russia mambo ya Utabibu(MD) na akaoa mwanamke wa kizungu ambaye alizaa naye watoto watatu wa kiume na wote walikuwa Half-Cast na alirudi na kuishi Tabora akiwa na mkewe na watoto watatu.
Mama huyo wa Kizungu alikuwa mtaratibu na muungwana sana tofauti kabisa na mumewe Dr.Kobello ambaye alikuwa Mlevi Mbwa, mwenye dharau, malaya nk.
Watoto wake hawakuzaliwa machizi bali walikuwa na akili sana hususani mtoto wake wa Pili(Steven).
Lakini baadaye watoto wawili(Mtoto wa kwanza na wa pili(Steven)) walikuja kuharibika kabisa na kuwa kama machizi, Pombe, bangi na Unga vikiwa ndio chanzo kikubwa.
Kifupi Famili hii yote imeteketea kwa wote kufariki dunia kwa kipindi kifupi na amebaki mtoto mmoja ambaye ndio wa mwisho kuzaliwa.
Ni sad story nikiisimulia humu kwa kina hii familia namna ilivyopotea