Hahaha, nimepiga sana jolowe na kaka zangu, kuna vindege vingine vidogo vya blue, tulikuwa tunavitega kwa ungo na chenga za mchele sijui vyaitwaje.
Yule chizi, bwana tulikuwa wadogo about 12 na akawa anatuonesha dushe lake, we were just naughty girls.
huu uzi ni noma, mpaka kandege jambazi kakumbukwa! nilimsikia sana huyu ingawa kwa sura sikuwahi kumfahamu.
Ngubalu,Mfhulu,Nsalase,Ntondwa,Mikoma,Makuuwa,nk.bila kusahau uyoga wa porini kibao!
Mwanagu Hiyo familia ya Dk Kobelo walichoka sn Alafu alizaa matoto machizi!
Yalikua yakilewa mipombe yanamrudi mama Yao Wa Kirusi na kushiriki nae!
Teh Teh Teh teh!
Mkuu Lukansola humu JF kuna watu Wa mboka kibao! Bado watakuja na story kibao sn! Huyu Kandege alikua jambazi kubwa sn lenye makundi! Na ninafikiri alikufa kwenye ile oparesheni ya Wajeshi miaka ya 80 mwishoni pale walipowaua majambazi Wengi kule Kiloleni!
Ntuzu ngoja nikusahihishe kidogo.
Dr.Kobello alisomea Russia mambo ya Utabibu(MD) na akaoa mwanamke wa kizungu ambaye alizaa naye watoto watatu wa kiume na wote walikuwa Half-Cast na alirudi na kuishi Tabora akiwa na mkewe na watoto watatu.
Mama huyo wa Kizungu alikuwa mtaratibu na muungwana sana tofauti kabisa na mumewe Dr.Kobello ambaye alikuwa Mlevi Mbwa, mwenye dharau, malaya nk.
Watoto wake hawakuzaliwa machizi bali walikuwa na akili sana hususani mtoto wake wa Pili(Steven).
Lakini baadaye watoto wawili(Mtoto wa kwanza na wa pili(Steven)) walikuja kuharibika kabisa na kuwa kama machizi, Pombe, bangi na Unga vikiwa ndio chanzo kikubwa.
Kifupi Famili hii yote imeteketea kwa wote kufariki dunia kwa kipindi kifupi na amebaki mtoto mmoja ambaye ndio wa mwisho kuzaliwa.
Ni sad story nikiisimulia humu kwa kina hii familia namna ilivyopotea

nina hakika pia wengi tunaweza kufahamiana kabisa humu, Hongera kwa huu uzi Ntuzu, kweli nimekumbuka mengi sana.
Aposele naikumbuka ingawa nimesahau ilikuwa wapi, mama mpuguso naye vipi? anakumbukwa? na wale wahindi kina mukesh na sailesh je? walikuwa na garage. mukesh alikuwa anaendesha pikipiki ndo ilikuwa icon yake. nani anakumbuka bizeta hotel?
Mkuu Ntuzu
Inalekea wewe ulikua unakaa National House, Vipi kuna jamaa naitwa John Shija bado yuko mboka Nation ? na famila ya kina Simbakalia bado ipo Tabora ?
Kulikuwa na kampuni ya KISAMVUU(Tajiri wa Kaliua), KAZUGE, NAAMANSII etc sure wameanza kutengeneza barabara hadi december last year ulikuwa unatoka tabora hadi Usoke n lami tupu BT MADARAJA ni yamawazo sanaSiku ya jtano usiku bendi ya tabora jazz ilikua inatoa burudani pale unyanyembe social hall karibu na soko kuu mida ya saa nne usiku utasikia ukiw mitaa ya Chemchem near Kwa wanaume Milambo School nyimbo zinasikika "Ooooh najuta ....nifanye nini sasa....pole kaka mimi ni bado msichana....!"
Kulikua na mabasi ya kwenda Urambo yana carrier juu, road ikiwa ni vumbi nasikia siku hizi ni lami enz hizo stend mpya haijafunguliwa na mh Ben Mkapa aliyekuja kuifungua baadae sna akiwa anatembelea mkongojo kipindi hicho.
Redio za FM ilikua hakuna had baadae sana ikaja RFA na hizi za CG FM na VOT, voice of Tabora zikafuata.
Ukitembea njiani unaangukiwa na maembe aliyoacha Mwarabu ile njia ya karibu na NMB kwa nyuma imejaa miembe njiani
Kulikuwa na kampuni ya KISAMVUU(Tajiri wa Kaliua), KAZUGE, NAAMANSII etc sure wameanza kutengeneza barabara hadi december last year ulikuwa unatoka tabora hadi Usoke n lami tupu BT MADARAJA ni yamawazo sana
wapiii ripota wetu wa RTD BENIIIIIIIIIIIII KIKOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!! kutoka tabora mimi n Beniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii Kiko wa redio tanzania!!!huyu jamaa aliwahi ripoti kuhusu majambazi yaliyoteka basi la Anam kutoka Urambo kuja tbr ambako wasafiri waliamlishwa kupanda juu ya carrier ya bus then kulikuwa na askari 1 akaruka kutoka kwenye carrier ""mithili ya digidigi""(huyu n B kikooo)
nani anamkumbuka delhi kisesa? watoto wa mzee kisesa nadhani alikuwa doctor huyu mzee alikuwa anaishi karibu na round about ya bomani jirani na dr kasele (dentist). huyu mtoto ndo nilikuwa najifunzia kutongoza hivi yuko wapi jamani!