Etwege
JF-Expert Member
- Jul 4, 2018
- 8,105
- 20,307
Tangu zamani watu waliojenga nyumba kabla ya biashara wamekuwa wakiulizwa maswali ya kwa nini wasijenge biashara kubwa kwanza alafu ndio baadae wajenge nyumba, wanaouliza hayo maswali wanadai kujenga ni kuzika pesa!
Dhana ya kwamba ukijenga unazika pesa siku hizi imeshika kasi baada ya motivational speakers kuishikia bango na vijana wengi wameanza kuiamini.
Motivational speakers wasichokielewa ni kwamba
1. Watu wachache sana wanaojenga wakiwa na hela yote ya ujenzi, wengi wanajenga taratibu kwa kudunduliza.
2. Mtu akijenga anaaminika na jamii inayomzunguka na hata mabenki, yani anaweza kukopa hela au kudhaminiwa na mtu kwa haraka sana.
3. Hata ukijenga alafu baadae ikatokea biashara unataka kufanya na huna hela basi nyumba yako ni dhamana yako unaweza kupata mtaji wa hela unayoitaka.
4. Ukiona maisha ya mtu ambaye alikuwa na hela alafu biashara ikafeli kabla hajajenga nyumba na ana familia huwa ni mabaya na stress sana kuliko mtu mwenye nyumba yake alafu hana hela.
5. Motivation speakers mara nyingi hutolea mfano wa vijana wa nchi za Ulaya au Asia kuwa hawajengi nyumba na badala yake hufanya biashara tu, huu mlinganyo siyo Sawa kwa sababu ya utofauti wa sera za nchi, mfano Tanzania serikali haina sera ya makazi nafuu kwa raia wake, badala yake NHC wanajenga vijumba vidogo alafu wanaviuza kwa bei ya juu sana wakisingizia eti hizo ndiyo nyumba za bei nafuu kwa ajili ya wanyonge!!! Wakati Ulaya ni sheria ya nchi mtu binafsi haruhusiwi kujenga, yanajenga makampuni na serikali inasimamia ziwafikie raia kwa bei nafuu.