Kwa wale wanaowacheka watu waliojenga nyumba badala ya kufanya biashara

Kwa wale wanaowacheka watu waliojenga nyumba badala ya kufanya biashara

Huwa NAJIULIZA mbona wahindi na waarabu wamepanga alafu ndo matajiri, nilicho kuja kigundua pesa nyingi tunapoteza kwenye ujenzi ilihali pesa hiyo ukifanyia biashara ya uhakika ikakulipa unatoboa fasta alafu utajenga badae, ila usijenge ukiwa masikini
Matajiri wengi wana mambo zaidi ya haya unayoyafahamu.
 
Jenga hata mimi nimejenga , biashara ni pasua kichwa ...Biashara unaweza kufanya mwaka nzima ila sio kupata faida ni kuokoa mtaji , matajiri wote waoanfanya biashara wana mikopo na hawapati usingizi .

Jenga biashara lazima uwe makini , yaani hauwezi kukaa hapo kwa miaka mitatu lazima ushtue akili ya kujiongeza . Biashara bila ya makazi bado una asilimia kadhaa za kuwa maskini kabisa au kuwa tajiri mkubwa so kama hauamini katika kubeti basi achana na biashara . Nilishawahi kupoteza milion 10 huku nikitegemea kupata faida ya milion 5 kutokana na biashara hiyo , so technically ni bettin ; hii ni baada ya kukaa na kuwazua vizuri .​

Motivational speaker ukiwa na akili hauwezi kuwasikilia , kwanza sio wafanyabiashara ila ni wauza mawazo ya biashara .
 
Umenena vyema
 
Huwa NAJIULIZA mbona wahindi na waarabu wamepanga alafu ndo matajiri, nilicho kuja kigundua pesa nyingi tunapoteza kwenye ujenzi ilihali pesa hiyo ukifanyia biashara ya uhakika ikakulipa unatoboa fasta alafu utajenga badae, ila usijenge ukiwa masikini
Hao wahindi na waarabu wasio watanzania wanaruhusiwa kumiliki ardhi nchini!?
 
Kwani hakuna.wafanyabiashara ngozi nyeusi ambao hawajajenga ? Je ni matajiri kama hao wahindi/waarabu?
Mimi mwenyewe sijajenga na viwanja ninavyo 3 na nilianza ujenzi nikasimama nikaingia kwenye biashara sasa naona mambo yanakwenda na nikitaka kuendelea ujenzi naendelea bila.kuwa na mawazo nachoamini mimi kama uko kwenye biashara ukawa na nizamu ya pesa na mzunguko upo swala la kujenga ni jambo la kawaida
 
Tangu zamani watu waliojenga nyumba kabla ya biashara wamekuwa wakiulizwa maswali ya kwa nini wasijenge biashara kubwa kwanza alafu ndio baadae wajenge nyumba, wanaouliza hayo maswali wanadai kujenga ni kuzika pesa!
Dhana ya kwamba ukijenga unazika pesa siku hizi imeshika kasi baada ya motivational speakers kuishikia bango na vijana wengi wameanza kuiamini.
Motivational speakers wasichokielewa ni kwamba
1. Watu wachache sana wanaojenga wakiwa na hela yote ya ujenzi, wengi wanajenga taratibu kwa kudunduliza.
2. Mtu akijenga anaaminika na jamii inayomzunguka na hata mabenki, yani anaweza kukopa hela au kudhaminiwa na mtu kwa haraka sana.
3. Hata ukijenga alafu baadae ikatokea biashara unataka kufanya na huna hela basi nyumba yako ni dhamana yako unaweza kupata mtaji wa hela unayoitaka.
4. Ukiona maisha ya mtu ambaye alikuwa na hela alafu biashara ikafeli kabla hajajenga nyumba na ana familia huwa ni mabaya na stress sana kuliko mtu mwenye nyumba yake alafu hana hela.
5. Motivation speakers mara nyingi hutolea mfano wa vijana wa nchi za Ulaya au Asia kuwa hawajengi nyumba na badala yake hufanya biashara tu, huu mlinganyo siyo Sawa kwa sababu ya utofauti wa sera za nchi, mfano Tanzania serikali haina sera ya makazi nafuu kwa raia wake, badala yake NHC wanajenga vijumba vidogo alafu wanaviuza kwa bei ya juu sana wakisingizia eti hizo ndiyo nyumba za bei nafuu kwa ajili ya wanyonge!!! Wakati Ulaya ni sheria ya nchi mtu binafsi haruhusiwi kujenga, yanajenga makampuni na serikali inasimamia ziwafikie raia kwa bei nafuu.
Kila mtu afanye anachoweza, fainali uzeeni. Kuna wazee kibao wana majumba huku kitaa....hawana pesa tena, hawana uwezo hata wa kukarabati magofu yao, wanasumbua wapangaji kinoma. biashara ya kuzeeka nayo unayo?
 
Nyumba inaweza kukusaidia kupata mkopo
Mkopo sio msaada. Wewe endelea kusema INAKUSAIDIA. Na by the way, kiachkopeshwa ni biashara yako sio nyumba yako. Nyumba ni dhamana ya mkopo. Kama biashara haiwezi kulipa mkopo huo.......nyumba utabaki nayo na hela hukopeshwi.

Nenda leo bank na hati ya nyumba yako sema unataka kukopa milioni 20 ukaanzishe biashara fulani huna experience nayo yaani ndio startup, uone kama watakupa.
 
Hii budget inanifosha kununua FORD MUSTANG pamoja na kuicustomize then Ashraff atanikoma road labda usivae kiofficer
 
Back
Top Bottom