Kwa wale wanaowacheka watu waliojenga nyumba badala ya kufanya biashara

Kwa wale wanaowacheka watu waliojenga nyumba badala ya kufanya biashara

Kila mtu afanye anachoweza, fainali uzeeni. Kuna wazee kibao wana majumba huku kitaa....hawana pesa tena, hawana uwezo hata wa kukarabati magofu yao, wanasumbua wapangaji kinoma. biashara ya kuzeeka nayo unayo?
Wazee wenye majumba wasumbufu kivipi wakati wanadai kodi zao kwa wapangaji waliozeeka na biashara zao. Akili kumkichwa.
 
Kwanza tungepata standard ya nyumba ambayo mtu unaweza kusema hapa nina nyumba. Utakuta mtu anasifiwa ana nyumba na gari kumbe nyumba ambayo thamani yake haivuki 25m na gari Passo au Vitz. Huwa inakera sana. Tukubaliane kama taifa kiwango cha nyumba inayompa mtu uhalali wa kusema ana nyumba.

Binafsi naona kama kuna uwezekano wa kujenga mapema bora ujenge hasa kwa ambao wameajiriwa. Hata kama unafanya biashara ukishaanza kutengeneza faida tumia kidogo kidogo hata 30% ya faida kwenye ujenzi. Kama faida yako ni 1m kwa mwezi sio mbaya kutumia 300k kwenye ujenzi. Hizi biashara tunazifanya ila hazitabiriki kabisa. Unaweza fuata kanuni zote ila bado ukapasuliwa tu. Nyumba ni muhimu kuwa nayo. Wapuuze wanaosema hapa tunapita.

Cha kukumbuka pia ni kwamba kuna baadhi mtajipinda na kufanya kazi kwa bidii ila hamtakaa mfanikiwe kiuchumi kwa sababu jamii pia inahitaji mifano ya watu kama ninyi.
 
Huwa NAJIULIZA mbona wahindi na waarabu wamepanga alafu ndo matajiri, nilicho kuja kigundua pesa nyingi tunapoteza kwenye ujenzi ilihali pesa hiyo ukifanyia biashara ya uhakika ikakulipa unatoboa fasta alafu utajenga badae, ila usijenge ukiwa masikini
Bora tu wajenge maana watu weusi kuna namna fulani tunakosa skills za biashara,consistency,commitment nk..Hao wahindi na waarabu wanaanza fundisha watoto wao biashara wakiwa na miaka 5 hivi... Sasa sisi ushasoma zako mpaka chuo kikuu ndio uje uanze biashara itakuwa ngumu
 
Fact
 
Back
Top Bottom