Nimetebasamuu halafu nikataka kucheka ila kicheko kikapotea....
Haya mambo banaa, na usishangae kuna walioachana kisa kufua nguo za ndani....
Mke anasema mimi sifui boksa zako unavaa wiki nzima unarudia...
Mume anakasirika kwanini hunijali na mimi nispoona boksa safi navaa ya jana...!!!🤔🤔🤔 (ana mkomoa nani...! Mbupuuu au mkee..!!?). Ukurutu unaanzia hapa..
Kuoa au kuolewa ni zaidi ya kufanya harusi, shurti kwanza uwe umepevuka kiakili/maarifa na uwe na busara za kutosha.
Ukiwa na mihemko, hasira za mkizi na maamuzi yasiyo na kichwa wala miguu, umekwisha.....!!
Jiulize tuu, kutoa/kutolewa mahari ndo sababu ya kubadili mfumo wako wa maisha?
Kama wakati uko mseja ulikuwa unajimudu, kwanini baada ya kuoa/kuolewa uwe mlemavu mwenye viungo vyote? Hii ni hata kina dada, kama ulikuwa unajigharamia kwanini baada ya kuolewa ugharamikiwe...!!
Fanya huduma unayopewa na mwenza kama zawadi/nyongeza isipokuwepo isokuletee masononeko, maumivu au kuona hutendewi haki au kudhulumiwa.
Sikuzote penda maisha ya kujitegemea na si kutegemea flani kwa namna yeyote ile. Atayekupenda kwa dhati atakufata hapo ulipo ukiwa unajimudu na yeye asikufanyie jambo ili umuelekee, afanye bila kutarajia malipo.
Suluhiso la kuondoa hiyo kero tajwa, wekeni bajeti ya luku ya kutosha kwa mwezi, bajeti ya bili ya maji, nunueni mashine ya kufulia, chupi/boksa za kuvaa mwezi mzima bila kurudia.
Siku ya kufua iwe mara moja au 2 kwa wiki mnatumbukiza visinda vyenu humo, vesti, soksi, hendikachifu, brazia, gagulo, skin tite kisha mnaanika kama hamna mashine ya dryer.
Mkishindwa hapo tembeeni wizout. Yaani wewe usivae boksa, nayeye asivae kufuli wala brazia, nawewe usivae vesti wala soksi kukwepa nani afue na pia mtapunguza gharama ya kuzinunua.
NB: Dada wa kazi asifue nguo yeyote ya ndani. Mpeni suruali mashati magauni sketi blauzi basi. Hata hendikachifu asifue.
HYGENE: Usirudie kuvaa nguo ya ndani, vaa nguo ya ndani.mara moja kisha ifue.
Mwenye sikio asikie.
Bibi Kasinde.