Kwa wanandoa: nani ana jukumu la kufua nguo zenu za ndani?

Kwa wanandoa: nani ana jukumu la kufua nguo zenu za ndani?

Kwenye ukuaj wangu had Sasa hiyo ni kazi ya mke watu wasilete uzungu wa et kusaidiana ooh sijui 50/50 mim sitak hayo wewe nenda katafute mim na watoto tule mim nitakufulia hata kukufua na wewe nitafanya ivo

Hiyo boxer hainigharim chochote as long as nakula nashiba [emoji4]
100% Bantu Lady Checked!
 
Nimetebasamuu halafu nikataka kucheka ila kicheko kikapotea....

Haya mambo banaa, na usishangae kuna walioachana kisa kufua nguo za ndani....

Mke anasema mimi sifui boksa zako unavaa wiki nzima unarudia...
Mume anakasirika kwanini hunijali na mimi nispoona boksa safi navaa ya jana...!!!🤔🤔🤔 (ana mkomoa nani...! Mbupuuu au mkee..!!?). Ukurutu unaanzia hapa..

Kuoa au kuolewa ni zaidi ya kufanya harusi, shurti kwanza uwe umepevuka kiakili/maarifa na uwe na busara za kutosha.

Ukiwa na mihemko, hasira za mkizi na maamuzi yasiyo na kichwa wala miguu, umekwisha.....!!

Jiulize tuu, kutoa/kutolewa mahari ndo sababu ya kubadili mfumo wako wa maisha?

Kama wakati uko mseja ulikuwa unajimudu, kwanini baada ya kuoa/kuolewa uwe mlemavu mwenye viungo vyote? Hii ni hata kina dada, kama ulikuwa unajigharamia kwanini baada ya kuolewa ugharamikiwe...!!

Fanya huduma unayopewa na mwenza kama zawadi/nyongeza isipokuwepo isokuletee masononeko, maumivu au kuona hutendewi haki au kudhulumiwa.

Sikuzote penda maisha ya kujitegemea na si kutegemea flani kwa namna yeyote ile. Atayekupenda kwa dhati atakufata hapo ulipo ukiwa unajimudu na yeye asikufanyie jambo ili umuelekee, afanye bila kutarajia malipo.

Suluhiso la kuondoa hiyo kero tajwa, wekeni bajeti ya luku ya kutosha kwa mwezi, bajeti ya bili ya maji, nunueni mashine ya kufulia, chupi/boksa za kuvaa mwezi mzima bila kurudia.

Siku ya kufua iwe mara moja au 2 kwa wiki mnatumbukiza visinda vyenu humo, vesti, soksi, hendikachifu, brazia, gagulo, skin tite kisha mnaanika kama hamna mashine ya dryer.

Mkishindwa hapo tembeeni wizout. Yaani wewe usivae boksa, nayeye asivae kufuli wala brazia, nawewe usivae vesti wala soksi kukwepa nani afue na pia mtapunguza gharama ya kuzinunua.

NB: Dada wa kazi asifue nguo yeyote ya ndani. Mpeni suruali mashati magauni sketi blauzi basi. Hata hendikachifu asifue.

HYGENE: Usirudie kuvaa nguo ya ndani, vaa nguo ya ndani.mara moja kisha ifue.

Mwenye sikio asikie.

Bibi Kasinde.
Happy new year bibi Kassie
Hapa umemaliza kila kitu
 
Kama umelelewa kwenye imani ya kikristo, kuna neno UPENDO... hili ni Tunda la Roho na lina matawi yake...

UPENDO- Haujivuni, Haubesabu mabaya, Hautakabari, na mengine 4 nimesahau atayekumbuka aongeze hapa.

Ukimpenda mwenza wako kwa Tunda la Roho = UPENDO huwezi kufika kwenye hii kesi ya nani afue kufuli...

Kila la Kheri.
 
Huko kwenu mnafanyaje? na kwanini?

(A) Kila mmoja anafua underwear yake
(B) Hakuna formula maalum
(C) Mume anafua ya kwake na ya mke
(D) Mke anafua ya kwake na ya mume
(E) Dada/kaka wa kazi
inategemeana na mnavyoheshimiana na kupendana. Kuna wanawake wanapenda usafi wakati wote, hufua boksa za waume zao kila siku ni lazima ubadilishiwe kila unapotoka bafuni, kama hutaki na uroda hupewi
 
Mke anaejieliwa hufanya kazi za mumewe mwenyewe, akianza kupangiana zamu na mumewe kufua nguo za ndani hashindwi kumpa hata kijakazi kufua

Mimi niko bize sana na kazi si shindi nyumbani lakini kila ki
tu cha Mume wangu na fanya mwenyewe hadi mafuta na mpka imefikia hatua, niki mtizama namuona hawezi lolote like a baby.

Nae ameshazoea maisha hayo.
 
Mke anaejieliwa hufanya kazi za mumewe mwenyewe, akianza kupangiana zamu na mumewe kufua nguo za ndani hashindwi kumpa hata kijakazi kufua

Mimi niko bize sana na kazi si shindi nyumbani lakini kila ki
tu cha Mume wangu na fanya mwenyewe hadi mafuta na mpka imefikia hatua, niki mtizama namuona hawezi lolote like a baby.

Nae ameshazoea maisha hayo.
Kufua boksa moja au kimwanandani/kyupi moja unapoenda kuoga inachukua muda gani?
 
Back
Top Bottom