Kwa wanandoa: nani ana jukumu la kufua nguo zenu za ndani?

Kumbe mwenye kuchekesha ye'huwa hacheki, huishia tu kutabasamu?

... 'Tembeeni wizout'..., hili limenivunja mbavu na nimecheka kwa sauti kifala🀣🀣🀣🀣.

Bonge la ushauri na kweli 'mwenye masikio na asikie'
 
Kila mtu anafua zake.Tuache ulemavu wa kuigiza kwenye ndoa.Mtataka mpigishwe mswaki na kulishwa kama vichanga.
Siyo kupigishwa mswaki tu na 'kushikiliziwa' mi nataka.

Ingewezekana hata kutafuniwa nitafuniwe na kumeza nimezewe, kazi yangu iwe ni kushiba tu.

Hata kuendewa haja niendewe, lakini dunia inagoma, eti lazima niende chooni mwenyewe na ku piz lazima nihusike moja kwa moja bila kusaidiwa na mtu!
 
.......mimi nitakufulia hata kukufua na wewe......😘 Nimeipenda sana hii.
Btw, umeolewa?
 
Aise dunia ingekubali kuendewa chooni ingekuwa raha tupu.

Yaani mtu anaenda chooni kwa niaba yako
 
Nguo hufuliwa na mwanamke, ziwe nguo za ndani ama za kawaida, huo ndio upendo, Mwanaume atafua nguo hizo kama kuna changamoto ya namna fulani tu,kama mambo ya kiafya,mke mgonjwa, mke hayupo katika mazingira ya kalibu na ulipo nk.

Hakuna utaratibu wa kwamba kila mtu afue za kwake, eti za furani zinanuka,au zamu ya mme leo kesho ya mke nk. Mkianza mambo hayo hapo hakuna ndoa ila kuna washindanaji tu.

Mke mwema hufua nguo za mme wake, humuandalia mavazi mme wake na kuhakikisha usafi wote wa mme wake.

Kama mwanaume ukishaona umeanza kujifuria nguo mwenyewe , tambua kuna changamoto katika mahusiano yenu ya ndoa ambayo bado hayajiweka wazi , na utambue uzeeni utahangaika sana na huyo mwanamke. Mwenye masikio na asikie.
 
Kabisaaa, hata mke awe mtu wa ofisini , akirudi lazima afanye majukum yake ikiwemo na usafi wa wote wawili na watoto, mimi nawasha tv kabisa na kina junior tunanza kuangalia katuni zetu mama anafua boksa huko uani.

Hiyo ndio ndoa wakati wa amani, mkianza eti leo na wewe fua , boksa zako zinanuka , mara oooh mm leo nimechoka hiki kufanya , kwani wewe huna mikono, kwani zamani ulikuwa unafanyiwa na nani?. Kila kazi mm! Hapa na 50/50 hiiiiiiiiiii umekwisha mwanaume
HAPO NDOA HAKUNA ,ILA IPO NDOANO [emoji28][emoji28]
 
Wema Wangu uliniponza, nikasema KAMWE sitaingilia majukumu ya MTU, niliingia kuoga, nikajisahau kuvua boxer, basi baadae ya kuoga nikaamua niifue kabisa nikaiweka toilet. Duh hio kesi yake, imekuaje leo, kuna nini, blablablaaa. Nikajisemea eeghh Kumbe.....
 
Hata mim ningekuhoji au Kuna jambo limetendeka lakukufanya wewe ufue hiyo nguo? Maana sio kazi yako kufua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…