Kwa wanaoamini hakuna Mungu, njooni hapa

Kwa wanaoamini hakuna Mungu, njooni hapa

Umejibu jibu refu my nataka useme ndio au hapana kisha niendelee Sion hutaki Imani sema ndio au sio
Sasa kama unataka jibu fupi si usome maneno mawili ya mwanzo tu nimeanza kwa kuandika "Sitaki imani" nikijua kabisa kuna watu wavivu wa kusoma na hawawezi kufuatilia mlolongo wa maandishi ya kimantiki.

Tatizo lako lipi ikiwa maneno mawili ya mwanzo kabisa yanasema "Sitaki imani" na huko mbele ni maelezo tu ya kwa nini sitaki imani?

Umeshindwa kusoma hata maneno mawili ya mwanzo ya jibu?
 
Nafikiri amewaita nyie ndio mumtukane maana nyie people mna matus mazitoo mnooooo maana hamjali kama kuna huku end of time!?
Tusi zito kabisa kwa mtu ni kuaminishwa kuna Mungu asiyeonekana, asiyethibitishika kimantiki,mwenye contradictions nyingi sana katika maelezo ya kuwepo kwake.

Ukiambiwa uamini Mungu huyu yupo ndiyo tusi kubwa kuliko yote.

Hatuwezi kuwatukana tusi kubwa kuliko mnavyotutukana tuamini uwapo wa Mungu huyu.
 
Tusi zito kabisa kwa binadamu ni kuaminishwa kuna Mungu asiyeonekana, asiyethibitishika kimantiki,mwenye contradictions nyingi sana katika maelezo ya kuwepo kwake.

Ukiambiwa uamini Mungu huyu yupo ndiyo tusi kubwa kuliko yote.

Hatuwezi kuwatukana tusi kubwa kuliko mnavyotutukana tuamini uwapo wa Mungu huyu.
Sawa mkuu. Uzuri ninkwamba soote tutakufa. Hili ndilo huwa linanifanyaga nisiwe mbishi saana kuhusu masuala ya Mungu
 
Sawa mkuu. Uzuri ninkwamba soote tutakufa. Hili ndilo huwa linanifanyaga nisiwe mbishi saana kuhusu masuala ya Mungu
Kufa kunatakiwa kukufanya ubishie uwepo wa Mungu, hususan Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.

Watu wengi wanakufa bila kupenda, wanakufa kabla ya kumaliza kazi zao, wanakufa na kutenganishwa na familia zao wanazozipenda.

Surely, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwepo angewahurumia hawa viumbe wake na kuwafanyia wepesi kwenye kufa, ama wasife, ama wafe kwa kuweza kupanga wao wafe vipi na lini.

Kifo cha kufa bila kutaka wala kupanga kinaonesha Mungu huyo hayupo.
 
Kufa kunatakiwa kukufanya ubishie uwepo wa Mungu, hususan Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na uoendo wote.

Watu wengi wanakufa bila kuoenda, wanakufa kabla ya kumaliza kazi zao, wanakufa na kutenganishwa na famikia zao wanazozioenda.

Surely, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwepo angewahurumia hawa viumbe wake na kuwafanyia wepesi kwenye kufa, ama wasife, ama wafe kwa kuweza juoanga wao wafe vipi na lini.

Kifo cha kufa bila kutaka wala kuoanga kinaonesha Mungu huyo hayupo.
Sawa..ila naongelea fumbo baada baada ya kufa. What happens next?
 
Sawa..ila naongelea fumbo baada baada ya kufa. What happens next?
Hakuna fumbo hapo.

Baada ya kufa unaoza. Atoms zako zinaenda kuwa wadudu, mimea, nyingine zinabaki kwenye mifupa. Wewe kama wewe ndio mwisho wako hakuna utakachojua tena.

By all scientific evidence ukifa ndiyo mwisho wako, hizo habari za kuishi baada ya kufa ni hadithi za kiimani tu ambazo hakuna anayeweza kuthibitisha.
 
Kukosekana wa kuthibitisha haihalalishi kuwa hakuna hayo maisha!.
yaweza kuwa sawa na kumpa mtoto wa kayumba primary darasa la kwanza a solve integration question
Sisemi tu kwamba hakuna maisha baada ya kifo kwa sababu hakuna uthibitisho.

Nasema hivyo pia kwa sababu maisha baada ya kifo kwa aliyekufa yanapingana na kanuni za kibaiolojia, kanuni za kifizikia, kanuni za kisayansi.

Pia.

Kuna mambo hayathibitishiki, lakini yapo.

Na kuna mambo hayathibitishiki, kwa sababu hayapo.

Sasa wewe utajuaje maisha baada ya kifo yapo na hayathibitishiki, na si kwamba hayathibitishiki kwa sababu hayapo?
 
Sisemi tu kwamba hakuna maisha baada ya kifo kwa sababu hakuna uthibitisho.

Nasema hivyo pia kwa sababu maisha baada ya kifo kwa aliyekufa yanapingana na kanuni za kibaiolojia, kanuni za kifizikia, kanuni za kisayansi.

Pia.

Kuna mambo hayathibitishiki, lakini yapo.

Na kuna mambo hayathibitishiki, kwa sababu hayapo.

Sasa wewe utajuaje maisha baada ya kifo yapo na hayathibitishiki, na si kwamba hayathibitishiki kwa sababu hayapo?
in your science world, kuna mambo yanatajwa sana, vitu kama mind, soul, spirit!.
Has any body ever proved of them??
 
in your science world, kuna mambo yanatajwa sana, vitu kama mind, soul, spirit!.
Has any body ever proved of them??
Hata kama kwenye science hawaja prove. Hilo bado halithibitishi Mungu yupo.

Science haijawahi kusema ime prove kika kitu.

Ulichofanya hapo kinaitwa "Whataboutism".

Whataboutism inatokea pale unapoulizwa jambo, ukashindwa kulijibu, ukahamisha goli kuuliza "But what about that, what about this?".

Kifalsafa haya maswali ni logical fallacy ya logical non sequitur.

Hoja hapa ni Mungu yupo au hayupo?

Hayo mambo ya mind, soul, spirit kwanza mimi sikubali kwamba science inazungumzia soul na spirit. Wapi kuna scientific definition ya soul na spirit?

Somo la soul na spirit lipo katika sayansi gani? Topic gani ya biolojia inaongelea soul na spirit? Soul na spirit ipo wapi katika mwili wa mtu? Kuna experiment gani ya kisayansi ikiyofanyika kuthibitisha uwepo wa soul na spirit?

Mind inaelezewa, inapimwa kisayansi, kuna watu wanafanya experiments mpaka za kuona ubongo wako unavyofikiria.

Lakini, usititoe kwenye reli. Hoja ni Mungu. Thibitisha Mungu yupo.

Hata sayansi ikishindwa kuthibitisha uwepo wa chochote, sayansi haijawahi kusema haina makosa, inaweza kujiongeza hata kesho ikasema tulikosea hapa.

Thibitisha Mungu yupo, usiseme hata sayansi kuna vitu haiwezi kuthibitisha.

Ukisema hata sayansi kuna vitu haijaweza kuthibitisha, hata kama hilo ninkweli, bado hujathibitisha Mungu yupo.
 
Hiyo stage ya kufikiria uliyopo tulishapita zamani sana bado unasafar ndefu mdogo wangu, unatakiwa kuijua vizuri geography, biology na chemistry
Bado hujafikia stage ya kuthibitisha Mungu yupo, hiyo ndiyo naitaka mimi.

Na mandhali hujafikia stage hiyo, hujafikia stage ya kuridhisha matakwa ya hoja yangu.
 
Uwepo wa Mungu ungekuwepo, tungebaki kubishana kama ni yeye ndo kaumba kila kitu kweli.
Umejuaje? Unathibitishaje hili?

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na uoendo wote angekuwapo, kungekuwa hakuna ubishi wowote kuhusu uwepo wake na nguvu zake.

Kwa sababu, kwa uwezo wake, ujuzi wake na upendo wake angetupa uelewa mzuri kabisa wote, tujue yeye ni nani na amefanya nini bila utata.

Ukishaona dunia ina si tofahamu kubwa kuhusu Mungu ni nani, ukiona kuna dini nyingi tofauti zina miungu tofauti, zinapingana, ujue huyo Mungu hayupo na suala la dini na Mungu ni suala la kiutamaduni tu, la kutungwa na watu tu.

Ndiyo maana kila utamaduni una Mungu wake tofauti.
 
Back
Top Bottom