in your science world, kuna mambo yanatajwa sana, vitu kama mind, soul, spirit!.
Has any body ever proved of them??
Hata kama kwenye science hawaja prove. Hilo bado halithibitishi Mungu yupo.
Science haijawahi kusema ime prove kika kitu.
Ulichofanya hapo kinaitwa "Whataboutism".
Whataboutism inatokea pale unapoulizwa jambo, ukashindwa kulijibu, ukahamisha goli kuuliza "But what about that, what about this?".
Kifalsafa haya maswali ni logical fallacy ya logical non sequitur.
Hoja hapa ni Mungu yupo au hayupo?
Hayo mambo ya mind, soul, spirit kwanza mimi sikubali kwamba science inazungumzia soul na spirit. Wapi kuna scientific definition ya soul na spirit?
Somo la soul na spirit lipo katika sayansi gani? Topic gani ya biolojia inaongelea soul na spirit? Soul na spirit ipo wapi katika mwili wa mtu? Kuna experiment gani ya kisayansi ikiyofanyika kuthibitisha uwepo wa soul na spirit?
Mind inaelezewa, inapimwa kisayansi, kuna watu wanafanya experiments mpaka za kuona ubongo wako unavyofikiria.
Lakini, usititoe kwenye reli. Hoja ni Mungu. Thibitisha Mungu yupo.
Hata sayansi ikishindwa kuthibitisha uwepo wa chochote, sayansi haijawahi kusema haina makosa, inaweza kujiongeza hata kesho ikasema tulikosea hapa.
Thibitisha Mungu yupo, usiseme hata sayansi kuna vitu haiwezi kuthibitisha.
Ukisema hata sayansi kuna vitu haijaweza kuthibitisha, hata kama hilo ninkweli, bado hujathibitisha Mungu yupo.