Hii sio kweli kabisa ndio maana nimekwambia idurisi tena maana ya Imani. Imani sahihi hutanguliwa na elimu yaani ujuzi, kisha kauli au kitendo unakifungamanisha moyoni. Hii ndio Imani Sasa.
Kwa Hoja Hii Nathibitisha Kuwa Kuna Mstari mdogo sana Kati ya wanayosema Kuhusu Wewe Na Wewe halisi Ulivyo..
(Rejea kauli ya Inforpren...)
Ni dhahiri Nimegundua Hata Unachokitetea Hujui Maana Yake na Hata unachokisimamia Hukitambui..
Kwanza Kabisa Hakuna Imani Sahihi..
Kwa sababu Imani zote zinatokana na internal experience, Kama mwenyewe Ulivyotaja kufungamanisha Moyoni..
Sasa Kitu kilicho ndani ya mtu mmoja mmoja hakiwezi kulingana Baadhi ya mtu na mtu kama hakiwezi kulingana hakuna Kilicho sahihi au Kisicho sahihi..
Kwa mfano Hakuna Universal Standard ha Utamu Kwa sababu Vionja Utamu Taste buds Zinatofautiana so Huwezi kuniambia Huu ndo Utamu wa Kweli sasa...
Labda Tuzungumze kilicho thabiti yaani Imani Madhubuti..
Mimi nachoona Hujui Hata Unachoongea wala unachotetea..
Ulichozungumza Ni circle ya Faith/believe With Doctrine..
Doctrine kwa Kiswahili ni Mafundisho ama Dogma au Maandiko au Unaweza ukaita Utakavyo Hata Itikadi(Itiqad)..
sasa kwakuwa Sijafa Niko tayari Kukueleza..
Ujuzi unaouongelea na Kuutambia kwamba Lazima kwanza Upate elimu ndo upate Imani ni Ujuzi au Elimu ambayo kwa lugha Ya kigiriki Tunauita "
PseudoSophia" au Unaweza Kuuita kwa Kuipamba kama Doctine..
Ila Elimu yyoyote ambayo Haina ithibati (Haina Uthibitisho wa Hoja Zake Ni PseudoSophia
Na mara Nyingi aina Mojawapo wa PseudoSophia ni Doctrine yaani Mafundisho ya Kidini..
Kwa Sababu Imani Zake hazijathibitishwa na Kuwa Facts..
Na Ndo maana Hata Science za Kwenye Dini Tunaita PseudoScience kwa sababu baada ya Kuthibitisha Imegundulika hazina Ukweli wowote..
So Twende kwenye Circle ya Imani Mpaka Doctrine mpaka kuwa PseudoSophia..
Nakupa Mfano:-
Baada ya Mtu kuanzisha Imani Yake Lets say nikasema naamini kwamba Babu yangu Mzee Kombo au Mzee ngazija Ananiangalia Hapa nilipo na Kuniletea Kila nitakachoomba na Kila siku ananipa Maelekezo..ya Nini nifanye maishani mwangu na Ameniambia Niandike Haya mambo na Niwafundishe watu haya mambo yote..
So Mimi nitaamini Kwamba Mzee Kombo au Mzee Ngazija wananitembelea Na Kunipa Maelekezo na wenzangu pia wanaoniamini Mimi wataamini Hivyo..
Baada ya Kuamini Hivyo Tutatengeza Mafundisho kuwafundisha wenzetu kuhusu Imani yetu Lets call it Mzee Ngazija..
Saaa Imani yetu ya Mzee Ngazija ikaendelea na Ikakuwa kwenye Kijiji chote..
Unategemea Mtu Atakayetaka Kujiunga na Imani ya Mzee Ngazija kwanza Anatakiwa Afanyaje??
Anatakiwa Afundishwe kwanza ili ajue anadeal na Nini na Baadae Awe na Itiqadi kama yetu sisi..
So Inaendelea Ile ile Circle ambayo mwanzo ilianza na Mtu mmoja kuota kutokewa na Mzee Ngazija..
Kwa Hiyo ukiangalia Chanzo unagundua Kimeanza na Mtu mmoja kuhisi au Kusema alionana na Mzee ngazija...
Lengo langu mimi Sio Kumu "out smart" Msomi wa Mafundisho ya Mzee Ngazija Lengo ni kutaka Kujua Ithibati Uthibitisho wa Huyo aliyesema aliongea na Mzee ngazija Je Kweli aliongea naye na una uhakika Upi kwamba Hayo maneno ni kweli ya Babu yake au ni yake ???
Kwahyo hata Ikipita Miaka 1000 na Imani Mzee ngazija Ikiwa Bado imesimama Swali linabaki pale pale yule Mtu wa Kwanza Una uhakika Gani kwamba aliongea na Mzee Ngazija..
Ipi.Ithibati ya Maneno yake..na Unathibitishaje maneno yake na Hiyo ndo maana Ya Imani..
Nafikiri Leo Tujikite kwenye Huu Mjadala