Kwa wanaume ambao mlikuwa na kazi lakini sasa hamna na wake zenu ndio wanaoendesha familia mliwezaje kutoboa?

Kwa wanaume ambao mlikuwa na kazi lakini sasa hamna na wake zenu ndio wanaoendesha familia mliwezaje kutoboa?

Nafikiri wanawake wengi wanaweza kuvumilia kuhudumia familia katika mazingira haya kwa muda Fulani pekee. Kuna threshold ikifika tunashindwa kuvumilia. Ndicho kili chotokea hapa.
 
Mwaka jana niliachwa na mpenzi wangu aliyekuwa mchumba wangu, nilikuwa sina hela, kazi zilisimama kwa hiyo nilikuwa kapuku haswaa. Aisee maneno niliyoyasikia sitakuja kumuamini mwanamke tena. Baada ya miezi kama 7 akanitafuta eti nimsamehe. Nilimsamehe lakini kila mtu na life yake, tukikumbukana tunawasilina au nikionana naye, lakini mapenzi hayapo tena kama ilivyokuwa mwanzo.
 
Sometimes huwa najichanya narudi na kiasi cha mboga lkh haki sustain na dharau ndio zinazidi tu

Wewe hutujui wanawake wala hutokaa utujue maana hata sisi hatujijui

Anayetujua ni Mungu tuu

Biblia takatifu - 1Petro 3:7​

Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.
 
Mkuu watoto watateseka vipi wakati huwahudumii KWA hela Yako,yaani haipo.
Jamani sio kama sichangii chochote kuna wkt huwa naotea narudi hata na mkate, samaki, nyama tuseme mboga kiujumla lkn sio consistency,

Ila ndio hivyo ni kama mapenzi yalishakufaga kitambo, na kuhusu watoto kama mnavyojua mama yao ashindi nyumbani then mnasema niende mbali huko nikatafute hawa watoto si nitawapoteza muangalie na hilo

Wengi wananichukulia mm kama marioo hapana, ni vile mambo hayapo poa
 
Mwaka jana niliachwa na mpenzi wangu aliyekuwa mchumba wangu, nilikuwa sina hela, kazi zilisimama kwa hiyo nilikuwa kapuku haswaa. Aisee maneno niliyoyasikia sitakuja kumuamini mwanamke tena. Baada ya miezi kama 7 akanitafuta eti nimsamehe. Nilimsamehe lakini kila mtu na life yake, tukikumbukana tunawasilina au nikionana naye, lakini mapenzi hayapo tena kama ilivyokuwa mwanzo.
Pamoja mwamba kuna watu wanajua hii chai lkn ukweli ni kwamba ni kweli yamenikuta na napitia kipindi kigumu
 
Nafikiri wanawake wengi wanaweza kuvumilia kuhudumia familia katika mazingira haya kwa muda Fulani pekee. Kuna threshold ikifika tunashindwa kuvumilia. Ndicho kili chotokea hapa.
Mbona cc tunawavumilia kipindi chote kwa shida na raha
 
mkuu tena bora akufukuze hapo yani umeshindwa kutafuta hata ajira ya udereva kichwa chako kimejaa maji
Hapan kifinga kichwa ipo vizuri tu sema she cought me offguard sikutegemea kama ange change so suddenly
 
mbona hata saizi wanamchakata na chupi unafua fuga hata kuku wa kienyeji wakiwa wengi utauza mmoja kwa hata elfu kumi itakufanya uweze kuchangia hata hela ya umeme hapo home
Naufanyia kazi ushauri wako
 
Unachozingua ni kushinda nyumbani.
Mwanaume kutafuta ni kila siku hakuna kushinda nyumbani mzee
UWe Unaondoka kila siku asubuhi, nenda katafute sio kukalisha trako tu
Kuna muda huwa nachomoka ku hustle na huwa narudi na mkate na kitoweo ila sio consistently
 
Hata mm hilo nmeliona the way jinsi anavyojib ni km karelax hv hana presha majib yake ni marahisi sana ila ni mtazamo tu
We hujui tu ndugu yangu usiombe yakukute, na sijui umeonaje kama nime relax sema tu mwenye shibe hamjui mwenye njaa

Kama kwako kuna amani na my wife wako muombe mungu
 
Nimefuatilia ushauri mzuri unaotolewa na watu na majibu ya mtoa mada. Nimegundua stori yake si ya kweli. Ingawa ina mafunzo ndani yake ila si ya kweli ametunga tu na ni mtu mwenye upeo mdogo sana hawezi kusoma mindset za watoa ushauri na kwenda nao sawa.

Ni akili kubwa tu ndio watanielewa
Funza dume ni kweli yamenikuta napitia kipindi kigumu sn dharau kwa mtu ambaye mlianza vizuri na ulitegemea muishi kwa amani sio jambo la kitoto... Mke anauma jamani
 
Pamoja mwamba kuna watu wanajua hii chai lkn ukweli ni kwamba ni kweli yamenikuta na napitia kipindi kigumu
Pole sana mkuu, wewe ni mwanaume usinung'unike sana, tulishaambiwa tutakula kwa jasho. Kwa hiyo mkuu haya tunapaswa kupitia ili kuwa wanaume kamili. Usife moyo mkuu, Mungu wa ajabu sana, Mungu haelezeki, lakini atakuvusha mpaka hutaamini ni wewe ulikuwa unamfulia mke wako?
Vilevile just mind your business ukimfuatilia huyo mwanamke utakuja kufanya vitu ambayo vitakushushia CV yako zaidi.
 
Back
Top Bottom