Kwa wanaume. Hakikisha hukosi hivi nyumbani kwako

Kama uko dar tembea kariakoo, waduka ya hardware, ziko za kila aina hata chini ya bei hiyo, pia maduka ya used powertools zipo za kila aina
Unapata complete na bits?
Maduka ya used yanakuwa wapi?
 
Kile kinachowaka taa na kupiga sauti? Kile hata wewe waweza nunua

Mafundi wakija wataanza story nyingi
 
Tujifunze vitu vidogovidogo, si lazima kila kitu tuite mafundi.
Youtube kuna watu wanafanya mambo wenyewe hadi raha.
Mf ukitaka weka sehemu za siri chumbani fanya mwenyewe hata kama itatumia miezi 2 mafundi wakimaliza finishing yao, ingia anza na yako
 
Ndg,hivi vifaa ni kwa sisi BUSHMEN....kuna wenzetu hata nyundo hajawahi iona na wala hana mpango huo....vifaa ni muhimu ila pia mazingira yana ~determine!
 
Baadhi ya Hivi vitu nilivikuta kwa ndugu yangu ni askari,nilishangaa na kumuuliza "kwani umeacha kazi yako ya awali(uaskari) na kuwa fundi?" alijibu kwa kuniuliza swali pia "kwahyo feni likilegea nikaazime spana kwa jirani au niite fundi?" sikuendelea kuuliza na sasahivi nimeanza kununua kimoja kimoja.
 
Hv yale mafuta ya nazi yanaweza kutumika kama kilainishi.?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…