Kwa wanaume na wanawake: Udongo (natural) Unaolainisha ngozi sasa unapatikana

Kwa wanaume na wanawake: Udongo (natural) Unaolainisha ngozi sasa unapatikana

Kuna mtu kanitumia links za website za udongo ambao hauna tofauti na Aunt Zainab's Natural Super Clay, nimeweka link chini hapa mkajionee bei unayouzwa nje:

Order Clear skin clay product

Order Clear skin clay product

Kwa kifupi wanauza gram 225 kwa US Dollar 34.00 ambazo ni takriban TZS. 60,000 sasa tazama na bei zetu ambapo gram 225 haizidi TZS 5,000.
 
Tuache UTANI:

Nampa tano Da Zainabu kwa bidii yake na kujipanga kwake kwema. Zainabu, ntakutafuta ili kuangalia siku moja kama ntaweza kukuunga na hawa Wanyamwezi wa SIKONGE ili na wao wanawiri. Si unajua tena hizi kazi za mashambani, na hasa tumbaku na asali, wakirudi wamechakalika haswa na siku za sikukuu wanataka watokelezee kama Faizafoxy.

Ntakutafuta nikija Dar ili kuangalia ni kwa jinsi gani unaweza kuwa parked vizuri na kuweza kuuzwa hadi nje ya Tanzania. Wakenya wenzetu hapo ndipo huwa wanatupiga magoli. Siahidi chochote kwa sasa ila nikitokea Dar basi ntakupigia. Ngoja niufanyie utafiti kuujua kabla sijakurupuka na kuangukia PUA na mtani wangu FF anicheke 🙂

Bi Zainab, jana nimeupata huo udongo wako na nimeanza kuutumia, yah ni ule ule kama niliowahi kununuwa Canada, ni mzuri kweli. Dah Ahsante sana.

Na lile jukwaa la MMU kweli ni rusha roho, lakini usijali hawa wana MMU wengi wanajipenda. Ngoja nikakupigie debe waje kukusoma huku, kama kunshambulia wanshambulie mimi, maana wale kule utafikiri wamewekewa mizizi hawatembei kwingine.
 
Sikonge

Nimemtembelea Dada Zainab Jumamosi iliyopita mpaka nyumbani kwake Sinza, tukala pamoja pilau la nguvu Ma sha Allah.

Huyu mama ni wa kusifiwa sana na wa kupigwa tough katika hili, hana exposure. Mumewe anaenda maporini, anachimba udongo, anauchekecha anausaga anauleta Dar. Mama Zainab yupo busy ana pack anahakikisha upo free of any bacterias na anasambaza na kufanya marketing. Na ana u pack katika mazingira mazuri sana, anastahili kila sifa na nilimshauri apige picha na kuziweka mtandaoni.

Katika kuongea nae alinieleza kuwa yeye alisomea kuhusu packing na packaging na preservation ya vyakula hapo Sido na akanionesha na cheti chake. Akanambia chumba maalum anachofanyia packing alikitayarisha kwa ajili ya packing na packaging ya achari na sauce na kabla hajaanza kuzalisha ikatokea hii habari ya huu udongo wake, ikabidi atumie hicho chumba kwa ajili hii. Hapo nampa kila sifa na sitaki kusema mengi, ana kila sababu za kufanikiwa kwa hili.

Si unamuona anvyomeremeta kwa udongo wake kwenye avatar yake, ndio yeye huyo.

Dada Zainab, ahsante kwa pilau na mengi zaidi na wapi nimefikia tutaongea nikija mjini Jumamosi.
 
Last edited by a moderator:
Udongo huo naufahamu na kweli kabisa unasaidia ingawa kuna baadhi ya nchi za Ulaya nafikiri kwa kutumia lobbying ya makampuni makubwa, waliupiga marufuku au kuuzuia kwa kuuwekea vikwazo. Nitaufanyia utafiti zaidi na kuangalia soko lake hapa SIKONGE na Tabora mjini.

Saa hivi ni jioni tayari na wengine tunajiandaa na MECHI ya mpira. Ntamtafuta kesho ili kuangalia biashara inakwendaje. Ila sijui kama ameshamalizana na watu wa TFDA maana hawakawii kuingiza timu kukuchunguza. Pia akishakuwa maarufu, ajiandae na SIKONGE TEAM ambayo ina-feki bidhaa si mchezo, si unaona mwenyewe kwenye picha?

Baadhi%2Bya%2Bbidhaa%2Bzilizoteketezwa%2Bna%2BMaofisa%2Bwakaguzi%2Bwa%2BTFDA%2Bwilayani%2BSikonge%2B(Picha%2Bna%2BAllan%2BNtana).JPG

From: TFDA YATEKETEZA BIDHAA FEKI ZENYE THAMANI YA SH MIL.5, SIKONGE MKOANI TABORA | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania Today

Vinginevyo, mie nashangilia sana bidhaa za Watanzania, tangu miaka mingi tu:
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...chi-yako-nunua-bidhaa-made-in-tanzania-2.html

Pilau hilo na mie ntakuja nile tu nikija kuchukua mzigo wa kwanza. Ila MSINILOGE sana watu wa Pwani nyie, nikaacha hela zangu zote za TUMBAKU na ASALI. Big Up Da Zainab na Mumeo.

Hayo ndiyo mambo ambayo mnatakiwa kumuelimisha huyu mama. Mimi kwa upande wangu nnampa ushauri kwa niyajuayo na juzi nilimpa link ya udongo kama wake ambao ninao na nimeununuwa ghali sana Canada naona kazi copy link na kuziweka hapo juu kidogo.
 
sikonge

Karibu sana na ushauri wako tutauzingatia.

Kwa sasa tunauuza kama wajasiriamali wadogo na sidhani kama kuna tatizo kwani udongo aina nyingine kama vile ule wa kamasai upo mpaka sokoni na hauna tatizio ingawa huu wetu una ubora zaidi na unakazi nyingi zaidi.

Ikiwa mtaiona fursa iliyopo na kujitokeza mkawekeza kwenye packing, branding na marketing basi mnaweza kuufikisha na ukawafikisha mbali sana. Itabidi mfanye sheria zote na sina wasi wasi na huu udongo kwani ni natural 100% na unatumika kwa matumizi mengi sana.

Ninachohitaji sasa hivi ni management ama kampuni ya management tutakaoingia ubia ya kuweza kuufikisha huko kwenye viwango vya juu.

Bi Faiza kauchukuwa kwa wingi anasema anakwenda kufanya hivi:

mud-bath-.jpg

farkhina, Bi Faiza kauchukuwa udongo kwa wingi amesema anakwenda kufanya hivyo.
 
Last edited by a moderator:
Angel Nylon na Mrs Kharusy njooni mjirembe mana mama ngu mwenyewe FaizaFoxy kanisahau kajinunulia mwenyewe tu

Nisameh sana maana nilipoutumia huu udongo hata sina la kukwambia ikabidi niufate mpaka Sinza, siku ya pili niakaukoroga kwa wingi nikajijaza nao mwili mzima, kama alivyosema Bi Zainab. Mnhh, its so luxurious, so refreshing. Try it.
 
Mimi sio wale watu wenye ngozi perfect, lakini haikuwa mbaya sana. Kama miezi mitatu iliyopita nilianza kupata chunisi tena kubwa kubwa utadhani zinapandikizwa hapo nikiwa nimelala. Nikajiuliza hizi pimples za uzeeni zinatoka wapi tena. Nilijaribu a few things but nothing worked.

Tangu nilipoanza kutumia huu udongo pimples zimekauka kabisa na hakuna mpya tena. Najipatia miezi miwili hivi nikiwa natumia nione kama haya mafanikio yatadumu.
 
Mimi uso wangu una mafuta sana na muda wote huwa nakuwa na pimples zisizoisha, nilipoanza kutumia huu udongo niliona mabadiliko sana kwani zilikauka na kubaki chache sana ambazo nazo zilikuwa zinaelekea kukauka.. lakini kuamka juzi najikuta zinarudi tena (tena kwa kasi ya ajabu) mpaka nimeanza kukichukia kioo, sasa sijajua kama ndo ufanyaji kazi wa huu udongo au vipi? Bado naendelea kuupaka japo nimeanza kuona uvivu kiasi fulani
 
Asante sana kwa feedback, ushauri:

Wenye matatizo ya chunusi tunawashauri kwa kuanizia waanze kunywa maji kwa wingi, yanasaidia sana kwenye ngozi. Wasitumie kabisa madawa yenye kemikali kwani yanaharibu ngozi zaidi ya kuitengeneza.

Pima kijiko kimoja cha chai cha Aunt Zainab's Super Clay, tia kwenye kibakuli au kikombe kisafi, tia maji kidogo koroga na changanya mpaka udongo na maji vichanganyike viwe kama (paste), paka usoni kote, wacha udongo ukaukie usoni halafu kosha kwa maji safi, wakati unaosha uso fanya kama una scrub kidogo kidogo.

Kama hali inaendelea badilisha, badala ya kuchanganya na maji kamua limao au ndimu uchanganye na udongo.

Tumia mfululizo usiache kwa wiki nzima kila siku japo mara moja.

Pia chunguza vyakula ulivyokula kabla hizo chunusi hazijakutokea.

Naomba jaribu kama nilivyokuelekeza na naomba feedback.

Huu si ushauri wa kidaktari, huu ni ushauri mbadala wa asili. Haali ikiendelea onana na daktari.

Nisameh sana maana nilipoutumia huu udongo hata sina la kukwambia ikabidi niufate mpaka Sinza, siku ya pili niakaukoroga kwa wingi nikajijaza nao mwili mzima, kama alivyosema Bi Zainab. Mnhh, its so luxurious, so refreshing. Try it.

Nimekusamehe usijali itabidi nifanye na mie niupate mana napenda sana clay mask
 
Aunt Zainab Tamim vipi huu udongo hauna tatizo kwa wenye sensitive skin?

Kuna mmoja alinitumia feedback hii na nikatoa ushauri huu:

Tunafuraha kuwajulisha kuwa, mmoja wa wateja wetu ana aleji ya ngozi ambapo hawezi kutumia sabuni za manukato na alikuwa na vipele vidogo dogo mwilini, tukamshauri ajaribu kidogo huu udongo mkononi aone kama utamfanyia aleji. Baada ya kuupaka kwa siku tano mfululizo kidogo mkononi haukumletea aleji na mapele ya pale alipopaka yamepungua sana. Jana ya tatu anaupaka mwilini na amefurahi sana na anasema mapele yanaondoka.

Aunt Zainab's Natural Super Clay si dawa ya aleji bali ni mbadala wa sabuni za manukato kwa wenye aleji na sabuni za manukato.

Tunashauri wenye aleji jaribuni, msijitie moja kwa moja kwanza jaribuni kwani kuna aleji aina nyingi na zinasababishwa na mambo mengi. Tunashauri wenye aleji kwanza wajaribu sehemu ndogo ya mkononi na udongo huu kidogo na wakiona hauna madhara waendelee kuutumia.

Udongo huu ni 100% Natural na haujaongezwa chochote.

Sijapata tatizo lolote kutoka kwa mwenye "sensitive skin" zaidi ya huyo mwenye allergy na udongo haujamfanyia allergy. Mimi mwenyewe binafsi nna allergy lakini huu udongo mwilini mwangu uko poa kabisa.
 
Ahsante sana gorgeousmimi njoo huku ujirembe
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom