Zainab Tamim
JF-Expert Member
- Jan 15, 2015
- 1,293
- 583
- Thread starter
- #221
Nimekusamehe usijali itabidi nifanye na mie niupate mana napenda sana clay mask
Ujaribu mamii hata mwilini utaufurahia.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimekusamehe usijali itabidi nifanye na mie niupate mana napenda sana clay mask
Ujaribu mamii hata mwilini utaufurahia.
Kama hauna madhara unawezaje kufanya ngozi laini!?
Mmeupeleka kwa mkemia kuupima? Isije ikawa una madhara yanayoweza onekana miaka kadhaa ijayo!!!..
Naamini mnaikumbuka DDT nimetolea mfano wa kemikali.
Huu udongo hauna madhara kwani unatumika na makabila fulani ya hapa nchini kwa miaka na miaka, hujipaka mwilini wanapoenda kuchunga kwa muda mrefu ili jua lisiwachome. Wangine hujipaka wakienda kulima kuzuwia jua lisiwachome.
Wanapigia mpaka mswaki kung'arisha meno yao na kufanya kinywa kisinuke. Mpaka wakichubuka hujipaka kuzuwia nzi na wadudu wasinyemelee kidonda na wenyewe wanaamini unaponesha kidonda haraka sana.
Pia ushauri wako ni mzuri tutaupeleka kwa mkemia mkuu ili tuwe na uhakika zaidi. Lakini mpaka sasa wenyeji wa huko tunakoupata ukiwaona ngozi zao ni mororo na zenye kuvutia.
Asante sana.
Nimekusamehe usijali itabidi nifanye na mie niupate mana napenda sana clay mask
Mungu akubariki sana kwa kazi unayofanya.
Hapa ni kijana wa kiume wa miaka 21.
Sasa mimi tatizo langu ni hili:
Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikisumbuliwa na chunusi ambazo huwa huja na kuondoka. Kwa zamani ile kwa kutokujua nilikuwa nazikamua na hadi sasa nina chunusi chache lakini nina alama nyingi za makovu ya chunusi usoni.
je huo udungo unaweza kunisaidia kuondoa hizo chunusi na sana sana hayo makovu madogo madogo? Unapatikana kwa bei gani? Unaweza kuutumia kama sabuni ya usoni?
mimi nipo hapa maeneo ya fire je ninaweza kufikishiwa iyo dawa iwapo inanifaa? Kwa gharama gani?
je nikitaka niutafute mtandaoni unatambulika kwa jina gani?
samahani kwa maswali mengi ni kutaka kujua na kupata suluhisho ya tatizo. Mungu akubariki
Ntajaribu inshaAllah ula ndio nafanya maarifa ntapataje
Sawa sawa! Ntawasiliana nayeBila samahani, huu udongo utakusaidia sana kwa ajili ya chunusi na makovu ya chunusi, sema makovu yanachukuwa muda kufifia kabisa inabidi uutumie kila siku lakini baada ya siku tatu tu utaanza kupata majibu.
Unaweza kuutumia kama sabuni ya usoni na mwili mzima.
Kwa ajili ya chunusi na makovu, unaupaka ukiwa mzito mzito (paste) baada kuuchanganya na maji na unauwacha usoni mpaka ukauke kisha unaunawa na ku scrub kidogo kidogo.
Kwa ajili ya matumizi kama ya sabuni unauchanganya na maji unakuwa mwepesi mwepesi (kama uji mwepesi) kisha unautumia kama sabuni, hauna povu lakini ukiutia maji unataleza kuliko hata sabuni.
Kwa hapo fire sehemu ya karibu utapoupata ni amma Kariakoo amma hapo mtaa wa Twiga na Nyamwezi na bei zao wanaongeza kidogo kwa ajili ya usafiri wanaotumia na faida yao, wasiliana na Raymond Mushi ndiyo anashughulikia Kariakoo na Ilala yote: Raymond Mushi - 0713422069 .
Soma post namba moja kwa kuona wapi utaupata kwa urahisi.
Mtandaoni huu wetu unajulikana kama Aunt Zainab's Natural Super Clay na ule wa nje ambao ni kama huu wetu unajulikana kama Clear Skin Clay. Waliokwisha utumia wanasema huu wetu 100% wa Kitanzania ni mzuri zaidi.
Usisite kuuliza zaidi na wala usiwe na shaka nipo kwa ajili hii na ni furaha yangu kuulizwa kuhusu huu udongo wetu.
Asante
Zainab
Sawa sawa! Ntawasiliana naye
Nataka kutumiwa dozen moja, nipo arusha nipm itanigharim shngapi pamoja na usafiri?
Ma sha Allah Bi Zainab, nilikwambia umeweza, huyo mteja wako anahakikisha hilo. Mimi nnakwambia, nimeutumia huu udongo wako na nilikuwa nnatumia udongo natural nnaoununuwa nje kwa bei ya juu sana ukilinganisha na huu wako lakini toka last week nimeanza kuutumia huu wako nnadiriki kusema huu wako ni 100% mzuri zaidi na bei yako mama ni kama bure kama alivyosema Heaven Sent.
Nakushauri anza kufikiria kuusafirisha nje ya Tanzania, unajuwa USA kuna soko kubwa sana la hivi vitu natural na huu kwa kuwa ni mali ya Tanzania 100% kuna mpango wa AGOA unaweza ukapata soko kubwa sana. Jipange dada jipange.
Bidhaa unayo tena safi sana sasa changamkia fursa.
Hongera sana.
huu udongo una faida kwa mwanaume
Haki ya mama, wewe mwanamke jinsi ulivyoandika hapo juu nimekupenda bure...
Ningekuwa sijaoa na wewe kuolewa, hakika ningeleta posa kwenu...
Umechelewa jamvini karamu imeshaliwa.
wa mikoani tukihitaji tunaupata ndanii ya muda gani na kama tunanunua kwa matumizi binafs tuanzae kununua kuanzia pakti ngapi?