Zainab Tamim
JF-Expert Member
- Jan 15, 2015
- 1,293
- 583
- Thread starter
- #241
samahan huo udongo ndo ule unaitwa lukaria wanauza wamasai
Huu si kama ule wa kimasai, huu hauna harufu kabisa na unateleza zaidi ukiutia maji.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
samahan huo udongo ndo ule unaitwa lukaria wanauza wamasai
Kumbe umeolewa??
Mie niliuchukua kwa wakala wako wa Dodoma ni mzuri kwa kweli japo mi sina chunusi ila nikiutumia wakati wa kuosha naisikia ngozi yangu vizuri (ulaini umeongezeka kwa kweli)
Ahsante, I know you'll love it. I have enjoyed.
Bi Faiza, Jumamosi iliyopita uliniambia unakwenda kujisiriba mwili mzima, ulifanya hivyo? ninaomba feedback.
Dada Zainab, usiwe na shaka ntakupa feedback, ni nzuri sana, sasa hivi ngoja kidogo, nipo jukwaa la siasa kuna kitu nnakisoma, ntakuja kwa kituo. Mambo mazuri sana.
OK ninakungoja, leo nitakuwa Kariakoo, kama upo mjini please tuonane.
Wewe Bibie vipi? Mie nilikuwa nna plan kuja Sinza kuchukuwa udongo, anyway, nijulishe kwenye simu utakuwa wapi Kariakoo ntakufata. Udongo utakuwa nao Kariakoo? kama hauna ujuwe ntakurudisha Sinza ukanletee.
Ninao bibi wewe, njoo tu ninatembea nao niuwache tena? kabla hujaja nataka feedback niisome.
Ninao bibi wewe, njoo tu ninatembea nao niuwache tena? kabla hujaja nataka feedback niisome.
Kwanza nimefurahi sana jana kunikutanisha na wifi lako, ni mtu tunaejuana miaka mingi sana hapa Dar., Jamani kweli dunia ni ndogo. Kumbe yule ndiyo wifi yako na huyo unaemuita Mzee Abdul ni mumeo, nnatamani kumuona, nikija tena Sinza ntakuja kwa ajili ya kumuona tu huo uzee aliozeeka. Jana nimecheka sana. Nimecheza nae utotoni huyo, usitake kujuwa mengi sasa yatakushinda.
Jamani Bi Zainab, ingawa jana tulikuwa wote mpaka saa 7 za usiku na nimemueleza kila kitu lakini kakazania feedback lazima niilete JF, jamani bibi king'ang'anizi huyu.
Bi Zainab nakuahidi ntaileta feedback post ijayo. Usijali mrembo tupo pamoja.
Nilivyotoka kwako kurudi tu nyumbani, nikachukuwa vikebe vyangu vitatu nikavitia kwenye ndoo, nikajaza maji nusu, nikaukoroga mpaka ukachanganyika wote na maji, nikasema leo huu udongo amma ntaujuwa amma utanijuwa, nikauwacha. Lile pilau ulilonilisha si likanitia usingizi (wewe bibi hujatia kungu mle?). Nikalala fofofo.
Siku ya pili sasa, Jumapili. Kwenda kuutazama nikakuta umejaa ndoo tele, mzito, kuushika unateleza hadi raha. Nikasema leo ndiyo leo, nikaliamsha Gozi. Nikaliomba lije kunipaka mgongoni, loh! si likaingia kazini, likanisiriba mwili mzima, nikaona haitoshi nikajikandika nao usoni na kichwani, nikawa kama sanamu la udongo.
Nikauwacha mpaka ukaukia mwilini, ulipokauka nikaliambia Gozi njoo, unifanyie massage, liakjidai unataka kuchubuka, udongo umekuganda si utakuchubuwa nikikufanyia massage? nikamwamabi usiwe mjinga, chukuwa hili bakuli la maji chovya mikono yako maji ujaribu, aise, sipati kukwambia. Likawa linachovya maji mikono yako linaendelea na kazi, yaani sijapata kuona, hakuna mafuta wala nini, it was simply amazing, kumaliza massage nikaenda kukoga laini nakwambia rahaaa, bila sabuni bila nini. Sema nimetumia maji mengi, kama ni kindoo kimoja hakitoshi, ila Dah! sina la kusema. Simply amazing.
Zainab udongo wako ni mali, nimejaribu scrubbing umekubali, nimejaribu masking umekubali, nimejaribu massage umekubali, nimejisiriba mwili mzima umekubali, na nnaiona difference vividly.
Sasa jana tulivyoachana, kufika nyumbani tu nimeutia kwenye bath tub, nimelijaza maji nikaukoroga nimeuwacha, sasa hivi nnavyokuandikia Gozi limeingia bafu nasikia linaniita, nnajuwa limeshajiingiza kwenye tub linakula raha. Ngoja niende ntakujulisha baadae maana linapiga kelele huko.
Zainab thanks a million kwa huu udongo, talk to you later.
Hahahahhahaha lol umenichekesha sana ina maana hilo jina la gozi ndio unalomwita baba angu? Nakusemea lol
Gozi Kiswahili inaweza kuleta maana ya kuchekesha na ndiyo maana namwita hivyo na yeye mwenyewe anajuwa, kisa chenyewe kilikuwa hivi (kwa ufupi):
Mwaka 1983 mimi na "Gozi", tulitembelea Egypt kwa mara ya kwanza, hapo nilikuwa sijaanza kumwita jina hilo. Kufika Egypt, yule aliyekuwa tour guide wetu anatupeleka kwenye ma pyramid akawa anatuuliza kwenye gari (unajuwa Kiarabu cha ki Misri mpaka ukizowee "accent" yake, na siku hizo tulikuwa hatujakizowea) in fact anamuuliza mume wangu, "dhii gowzik" akimaanisha "is she your pair?" Hatukumuelewa, tukashindwa kumjibu swali lake, kwa kuwa tour guide alikuwa anajuwa Kiingereza na sisi tulijidai na Kiarabu chetu cha "fog dirisha na takht meza" ndiyo maana akatuuliza Kiarabu, kujuwa kuwa hatukumuelewa ndiyo akatupa darsa:
Gowz = Pair
Gowzak = Your pair (M)
Gowzik = your pair (F).
Gowzi = (My Pair) this is the one I am using, the way the Egyptians pronounce sounds exactly like "Gozi" in Kiswahili.
Hii wala si ajabu kwani hata Kiswahili "jozi" ndiyo pair.
Nikashika toka siku hiyo kumwita Gozi, it simply means "my pair". Indeed he is my pair.
Toka siku hiyo mpaka leo sikubali kuambiwa nimeolewa au kanioa, nasema tumeoana, how can you be a pair if you do not match? (kama hamjaoana mtakuwaje jozi?).
Na imekuwa ni mzaha nyumbani mpaka wanangu wanamwita Gozi when they refer to him, wakinipigia simu they go something like "Gozi yupo au katoka?".
Hahahahaha funny ahsante kwa maelezo lakini very romantic nimeipenda
Indeed its romantic, wasikudanganye hata siku moja kuwa wamekuoa. Mmeoana.
Wewe Bi Zainab, haya njoo huku uone feedback yangu.
Kama hujaja ndani ya dakika kumi, nnakupigia simu nikuamshe.
Bibi unagubu wewe sijapata kuonapo.
Nimeipenda hiyo ya Gozi, nimemwambia Babu Abdul, kacheka sana, anasema hujaacha vituko.