Zainab Tamim
JF-Expert Member
- Jan 15, 2015
- 1,293
- 583
- Thread starter
-
- #201
Bi Zainab, jana nimeupata huo udongo wako na nimeanza kuutumia, yah ni ule ule kama niliowahi kununuwa Canada, ni mzuri kweli. Dah Ahsante sana.
Na lile jukwaa la MMU kweli ni rusha roho, lakini usijali hawa wana MMU wengi wanajipenda. Ngoja nikakupigie debe waje kukusoma huku, kama kunshambulia wanshambulie mimi, maana wale kule utafikiri wamewekewa mizizi hawatembei kwingine.
Ntafurahi ukija..ntaufuata kesho..ntakupigia jioni kujua kama ameupataMorogoro
Wateja wa Morogoro tunategemea udongo utapatikana hapo Jumatano. Tutawajulisha wapi mtaupata msambazaji wetu atakapotujulisha akiupokea mzigo
Asante
Zainab
Nimemtembelea Dada Zainab Jumamosi iliyopita mpaka nyumbani kwake Sinza, tukala pamoja pilau la nguvu Ma sha Allah.
Udongo huo naufahamu na kweli kabisa unasaidia ingawa kuna baadhi ya nchi za Ulaya nafikiri kwa kutumia lobbying ya makampuni makubwa, waliupiga marufuku au kuuzuia kwa kuuwekea vikwazo. Nitaufanyia utafiti zaidi na kuangalia soko lake hapa SIKONGE na Tabora mjini.
Saa hivi ni jioni tayari na wengine tunajiandaa na MECHI ya mpira. Ntamtafuta kesho ili kuangalia biashara inakwendaje. Ila sijui kama ameshamalizana na watu wa TFDA maana hawakawii kuingiza timu kukuchunguza. Pia akishakuwa maarufu, ajiandae na SIKONGE TEAM ambayo ina-feki bidhaa si mchezo, si unaona mwenyewe kwenye picha?
From: TFDA YATEKETEZA BIDHAA FEKI ZENYE THAMANI YA SH MIL.5, SIKONGE MKOANI TABORA | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania Today
Vinginevyo, mie nashangilia sana bidhaa za Watanzania, tangu miaka mingi tu:
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...chi-yako-nunua-bidhaa-made-in-tanzania-2.html
Pilau hilo na mie ntakuja nile tu nikija kuchukua mzigo wa kwanza. Ila MSINILOGE sana watu wa Pwani nyie, nikaacha hela zangu zote za TUMBAKU na ASALI. Big Up Da Zainab na Mumeo.
Ntafurahi ukija..ntaufuata kesho..ntakupigia jioni kujua kama ameupata
Angel Nylon na Mrs Kharusy njooni mjirembe mana mama ngu mwenyewe FaizaFoxy kanisahau kajinunulia mwenyewe tu
Angel Nylon na Mrs Kharusy njooni mjirembe mana mama ngu mwenyewe FaizaFoxy kanisahau kajinunulia mwenyewe tu
Zainab Tamim simu yako haipokelewi.
Mimi uso wangu una mafuta sana na muda wote huwa nakuwa na pimples zisizoisha, nilipoanza kutumia huu udongo niliona mabadiliko sana kwani zilikauka na kubaki chache sana ambazo nazo zilikuwa zinaelekea kukauka.. lakini kuamka juzi najikuta zinarudi tena (tena kwa kasi ya ajabu) mpaka nimeanza kukichukia kioo, sasa sijajua kama ndo ufanyaji kazi wa huu udongo au vipi? Bado naendelea kuupaka japo nimeanza kuona uvivu kiasi fulani
Nisameh sana maana nilipoutumia huu udongo hata sina la kukwambia ikabidi niufate mpaka Sinza, siku ya pili niakaukoroga kwa wingi nikajijaza nao mwili mzima, kama alivyosema Bi Zainab. Mnhh, its so luxurious, so refreshing. Try it.
Aunt Zainab Tamim vipi huu udongo hauna tatizo kwa wenye sensitive skin?
Kuna mmoja alinitumia feedback hii na nikatoa ushauri huu:
Tunafuraha kuwajulisha kuwa, mmoja wa wateja wetu ana aleji ya ngozi ambapo hawezi kutumia sabuni za manukato na alikuwa na vipele vidogo dogo mwilini, tukamshauri ajaribu kidogo huu udongo mkononi aone kama utamfanyia aleji. Baada ya kuupaka kwa siku tano mfululizo kidogo mkononi haukumletea aleji na mapele ya pale alipopaka yamepungua sana. Jana ya tatu anaupaka mwilini na amefurahi sana na anasema mapele yanaondoka.
Aunt Zainab's Natural Super Clay si dawa ya aleji bali ni mbadala wa sabuni za manukato kwa wenye aleji na sabuni za manukato.
Tunashauri wenye aleji jaribuni, msijitie moja kwa moja kwanza jaribuni kwani kuna aleji aina nyingi na zinasababishwa na mambo mengi. Tunashauri wenye aleji kwanza wajaribu sehemu ndogo ya mkononi na udongo huu kidogo na wakiona hauna madhara waendelee kuutumia.
Udongo huu ni 100% Natural na haujaongezwa chochote.
Sijapata tatizo lolote kutoka kwa mwenye "sensitive skin" zaidi ya huyo mwenye allergy na udongo haujamfanyia allergy. Mimi mwenyewe binafsi nna allergy lakini huu udongo mwilini mwangu uko poa kabisa.