Kwa wanaume na wanawake: Udongo (natural) Unaolainisha ngozi sasa unapatikana

Kama hauna madhara unawezaje kufanya ngozi laini!?

Mmeupeleka kwa mkemia kuupima? Isije ikawa una madhara yanayoweza onekana miaka kadhaa ijayo!!!..

Naamini mnaikumbuka DDT nimetolea mfano wa kemikali.


Sisi wenyewe si tumetengenezwa kwa udongo na hukohuko tutarudi? Sidhani kama kutakua na madhara hapo!

Mwalimu FaizaFoxy nimekosea?
 
Last edited by a moderator:
Mungu akubariki sana kwa kazi unayofanya.
Hapa ni kijana wa kiume wa miaka 21.
Sasa mimi tatizo langu ni hili:
Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikisumbuliwa na chunusi ambazo huwa huja na kuondoka. Kwa zamani ile kwa kutokujua nilikuwa nazikamua na hadi sasa nina chunusi chache lakini nina alama nyingi za makovu ya chunusi usoni.

je huo udungo unaweza kunisaidia kuondoa hizo chunusi na sana sana hayo makovu madogo madogo? Unapatikana kwa bei gani? Unaweza kuutumia kama sabuni ya usoni?
mimi nipo hapa maeneo ya fire je ninaweza kufikishiwa iyo dawa iwapo inanifaa? Kwa gharama gani?
je nikitaka niutafute mtandaoni unatambulika kwa jina gani?

samahani kwa maswali mengi ni kutaka kujua na kupata suluhisho ya tatizo. Mungu akubariki
 
Mie niliuchukua kwa wakala wako wa Dodoma ni mzuri kwa kweli japo mi sina chunusi ila nikiutumia wakati wa kuosha naisikia ngozi yangu vizuri (ulaini umeongezeka kwa kweli)
 

Bila samahani, huu udongo utakusaidia sana kwa ajili ya chunusi na makovu ya chunusi, sema makovu yanachukuwa muda kufifia kabisa inabidi uutumie kila siku lakini baada ya siku tatu tu utaanza kupata majibu.

Unaweza kuutumia kama sabuni ya usoni na mwili mzima.

Kwa ajili ya chunusi na makovu, unaupaka ukiwa mzito mzito (paste) baada kuuchanganya na maji na unauwacha usoni mpaka ukauke kisha unaunawa na ku scrub kidogo kidogo.

Kwa ajili ya matumizi kama ya sabuni unauchanganya na maji unakuwa mwepesi mwepesi (kama uji mwepesi) kisha unautumia kama sabuni, hauna povu lakini ukiutia maji unataleza kuliko hata sabuni.

Kwa hapo fire sehemu ya karibu utapoupata ni amma Kariakoo amma hapo mtaa wa Twiga na Nyamwezi na bei zao wanaongeza kidogo kwa ajili ya usafiri wanaotumia na faida yao, wasiliana na Raymond Mushi ndiyo anashughulikia Kariakoo na Ilala yote: Raymond Mushi - 0713422069 .

Soma post namba moja kwa kuona wapi utaupata kwa urahisi.

Mtandaoni huu wetu unajulikana kama Aunt Zainab's Natural Super Clay na ule wa nje ambao ni kama huu wetu unajulikana kama Clear Skin Clay. Waliokwisha utumia wanasema huu wetu 100% wa Kitanzania ni mzuri zaidi.

Usisite kuuliza zaidi na wala usiwe na shaka nipo kwa ajili hii na ni furaha yangu kuulizwa kuhusu huu udongo wetu.

Asante
Zainab
 
Ntajaribu inshaAllah ula ndio nafanya maarifa ntapataje

Tazama post namba moja sehemu utazoweza kuupata kiurahisi kama haupo kwenye sehemu hizo nijulishe nitatafuta njia ya kukufikishia. Unaweza ni PM.
 
Sawa sawa! Ntawasiliana naye
 

Haki ya mama, wewe mwanamke jinsi ulivyoandika hapo juu nimekupenda bure...

Ningekuwa sijaoa na wewe kuolewa, hakika ningeleta posa kwenu...
 
huu udongo una faida kwa mwanaume

Una faida kubwa sana kwani ngozi zetu zote ni sawa.

Matatizo ya ngozi kwa wanawake na wanaume ni sawa tena pengine wanaume ni zaidi kwani wao hunyoa mara kwa mara na huu udongo unawasaidia sana kutoa na kuzuwia mapele ya viwembe.

Chunusi na mapele ya mwilini inasaidia pia.
 
Samahani, huo udongo ndo ule unaitwa lukaria wanauza wamasai?
 
Haki ya mama, wewe mwanamke jinsi ulivyoandika hapo juu nimekupenda bure...

Ningekuwa sijaoa na wewe kuolewa, hakika ningeleta posa kwenu...

Umechelewa jamvini karamu imeshaliwa.
 
wa mikoani tukihitaji tunaupata ndanii ya muda gani na kama tunanunua kwa matumizi binafs tuanzae kununua kuanzia pakti ngapi?

Kuanzia kwa matumizi binafsi ni pakiti moja tu, samahani hili nilikuwa sijakujibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…