Kwa wanaume wanaotarajia kupata watoto

Kwa wanaume wanaotarajia kupata watoto

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Wanaume wenzangu naomba mtambue kwamba kama kuna kipindi ambacho unatakiwa kuonyesha mapenzi ya kiwango cha SGR / mapenzi ya hali ya juu ya kujali sana ni pale mkeo anapokuwa mjamzito.

Kipindi hiki mke huwa na mambo mengi sana na mpaka mengine unajiuliza hivi hii mimba inavyompelekesha ni yeye tu au wanawake wote wanakuwa hivi pia?

Kuambiwa umletee chakula fulani hlf baada ya kukileta akakitaa ni kawaida tu, kuambiwa usiku wa manane anahitaji soda ya baridi ni kawaida tu na viusumbufu vingi ambavyo havina kichwa wala miguu.

Huu ni wakati ambao mwanamke anapitia changamoto nyingi sana kihisia na mabadiliko makubwa ya vichocheo mwilini mwake,kwahiyo anakuwa katika hali ambayo sio ya kawaida, wengine wanakuwa hawana mambo mengi nawengine wanakuwa na mambo mengi.

Huu si wakati wa kushinda bar na kurudi nyumbani late bali ni wakati ambao uwepo wako ni muhimu sana kwa mwenza wako ili apate kufarijika

Si wakati wa kumpa stress na michepuko yako, ni wakati ambao anahitaji amani ya moyo wake sana,,ni wakati wa kujitoa mazima kwake na kumfanya awe malkia wako.

Kwasisi ambao kwa namna moja au nyingine kwa kipindi fulani tulizua taharuki katika kipindi hiki tuliona pale baby mama anapokuwa na stress mpaka kiumbe tumboni unakisikia kinavyo hangaika kana kwamba kinataka kitoke kimsaidie mama yake ,hii sio nzuri hata kidogo huwa sometime natamani ningerudisha siku nyuma na kuondoa makosa niliyofanya wakati baby mama alipokuwa mjamzito,,sitaki nawe ufanye makosa hayo.

Huu ni wakati wa kuwa mpole na laini sana kwa mkeo,,kwa kifupi jifanye fala sana kwa lengo la kufanya mkeo awe na wakati mzuri katika kipindi hiki,,hapa jishushe sana na uwe mwema sana kwake na uvumilie usumbufu wowote ambao utaupata kutoka kwake,,tambua sio yeye huyo bali ni ujauzito ambao anao ndio umebadilisha kila kitu katika maisha yake.

Onyesha upendo mkubwa sana kwa mkeo na hakikisha hatoi chozi katika kipindi hiki kigumu sana

Kuwa mwanaume na mume bora kabisa kupata kutokea hapa duniani.

Ni hayo tu!
 
Mengine kuendekeza na kujikweza ,,,soda saa nane usiku,,,mara lete hiki sikitaki tena,,,, mbona mabeki tatu, wanafunzi wanapata mimba wanakomaa kigumu mpk kujifungua ? Au kwa vile hakuna wa kumdekea
Naamini kwakuwa huishi nao ndio maana huwezi ona hizi aza zao,,,lau ungeishi nae ungeyakuta haya

Hawajidekezi ila ndio hali inayowatokea kipindi hiki
 
Wanaume wenzangu naomba mtambue kwamba kama kuna kipindi ambacho unatakiwa kuonyesha mapenzi ya kiwango cha SGR / mapenzi ya hali ya juu ya kujali sana ni pale mkeo anapokuwa mjamzito.

Kipindi hiki mke huwa na mambo mengi sana na mpaka mengine unajiuliza hivi hii mimba inavyompelekesha ni yeye tu au wanawake wote wanakuwa hivi pia?

Kuambiwa umletee chakula fulani hlf baada ya kukileta akakitaa ni kawaida tu, kuambiwa usiku wa manane anahitaji soda ya baridi ni kawaida tu na viusumbufu vingi ambavyo havina kichwa wala miguu.

Huu ni wakati ambao mwanamke anapitia changamoto nyingi sana kihisia na mabadiliko makubwa ya vichocheo mwilini mwake,kwahiyo anakuwa katika hali ambayo sio ya kawaida, wengine wanakuwa hawana mambo mengi nawengine wanakuwa na mambo mengi.

Huu si wakati wa kushinda bar na kurudi nyumbani late bali ni wakati ambao uwepo wako ni muhimu sana kwa mwenza wako ili apate kufarijika

Si wakati wa kumpa stress na michepuko yako, ni wakati ambao anahitaji amani ya moyo wake sana,,ni wakati wa kujitoa mazima kwake na kumfanya awe malkia wako.

Kwasisi ambao kwa namna moja au nyingine kwa kipindi fulani tulizua taharuki katika kipindi hiki tuliona pale baby mama anapokuwa na stress mpaka kiumbe tumboni unakisikia kinavyo hangaika kana kwamba kinataka kitoke kimsaidie mama yake ,hii sio nzuri hata kidogo huwa sometime natamani ningerudisha siku nyuma na kuondoa makosa niliyofanya wakati baby mama alipokuwa mjamzito,,sitaki nawe ufanye makosa hayo.

Huu ni wakati wa kuwa mpole na laini sana kwa mkeo,,kwa kifupi jifanye fala sana kwa lengo la kufanya mkeo awe na wakati mzuri katika kipindi hiki,,hapa jishushe sana na uwe mwema sana kwake na uvumilie usumbufu wowote ambao utaupata kutoka kwake,,tambua sio yeye huyo bali ni ujauzito ambao anao ndio umebadilisha kila kitu katika maisha yake.

Onyesha upendo mkubwa sana kwa mkeo na hakikisha hatoi chozi katika kipindi hiki kigumu sana

Kuwa mwanaume na mume bora kabisa kupata kutokea hapa duniani.

Ni hayo tu!
Unafanya yote mwisho wa siku unaambiwa mtoto sio wako.

Binafsi huaga naona tu kawaida ukimwendekeza nae anazidii

kipindi kizuri Cha kumjali saana mwanamke ni pale mara tuu baada ya kuzaa miezi 6 ya mwanzo

kipindi Cha ujauzito si kizuri saana kuonyesha hayo yote unayoyasema maana yeye huaga anapata furaha Zaid kwa mwanawe aliypo tumbon kwake, baba hapa Huwa unajipendekeza tu.
 
Hapa nakupinga kwa asilimia mia,,,lakini nimepokea maoni yako
 
Back
Top Bottom