Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Wanaume wenzangu naomba mtambue kwamba kama kuna kipindi ambacho unatakiwa kuonyesha mapenzi ya kiwango cha SGR / mapenzi ya hali ya juu ya kujali sana ni pale mkeo anapokuwa mjamzito.
Kipindi hiki mke huwa na mambo mengi sana na mpaka mengine unajiuliza hivi hii mimba inavyompelekesha ni yeye tu au wanawake wote wanakuwa hivi pia?
Kuambiwa umletee chakula fulani hlf baada ya kukileta akakitaa ni kawaida tu, kuambiwa usiku wa manane anahitaji soda ya baridi ni kawaida tu na viusumbufu vingi ambavyo havina kichwa wala miguu.
Huu ni wakati ambao mwanamke anapitia changamoto nyingi sana kihisia na mabadiliko makubwa ya vichocheo mwilini mwake,kwahiyo anakuwa katika hali ambayo sio ya kawaida, wengine wanakuwa hawana mambo mengi nawengine wanakuwa na mambo mengi.
Huu si wakati wa kushinda bar na kurudi nyumbani late bali ni wakati ambao uwepo wako ni muhimu sana kwa mwenza wako ili apate kufarijika
Si wakati wa kumpa stress na michepuko yako, ni wakati ambao anahitaji amani ya moyo wake sana,,ni wakati wa kujitoa mazima kwake na kumfanya awe malkia wako.
Kwasisi ambao kwa namna moja au nyingine kwa kipindi fulani tulizua taharuki katika kipindi hiki tuliona pale baby mama anapokuwa na stress mpaka kiumbe tumboni unakisikia kinavyo hangaika kana kwamba kinataka kitoke kimsaidie mama yake ,hii sio nzuri hata kidogo huwa sometime natamani ningerudisha siku nyuma na kuondoa makosa niliyofanya wakati baby mama alipokuwa mjamzito,,sitaki nawe ufanye makosa hayo.
Huu ni wakati wa kuwa mpole na laini sana kwa mkeo,,kwa kifupi jifanye fala sana kwa lengo la kufanya mkeo awe na wakati mzuri katika kipindi hiki,,hapa jishushe sana na uwe mwema sana kwake na uvumilie usumbufu wowote ambao utaupata kutoka kwake,,tambua sio yeye huyo bali ni ujauzito ambao anao ndio umebadilisha kila kitu katika maisha yake.
Onyesha upendo mkubwa sana kwa mkeo na hakikisha hatoi chozi katika kipindi hiki kigumu sana
Kuwa mwanaume na mume bora kabisa kupata kutokea hapa duniani.
Ni hayo tu!