Top 3 ya drama ninazozikubali:
1. Empress Ki, hii ni moja kati ya drama niliyoangalia mwanzo hadi mwisho bila kupepesa macho sababu ya kuwa na mpangalio mzuri wa matukio. Pia characters wamevaa uhusika vizuri sana kiufupi wamezitendea haki nafasi walizocheza wakiongozwa na bi dada Ha ji won pamoja na mtaalamu Ji Chang Wook bila kumsahau mtaalam Wang Yu. Hii hata niirudie mara 100 siwezi ichoka.
2. The land of the wind/ The Kingdom of the wind. Hii ilikua all time favourite drama yangu kabla ya kuangalia Empress Ki. Pia hii ni drama yangu ya pili kuitazama ya kwanza ni Jumong na ndio iliyopelekea mimi kuwa mlevi wa hii burudani adhimu ya wakorea. Kwenye hii drama nimependa jinsi walivyoonesha maisha ya mwanzoni kabisa ya nguli Daemusin Muhyul wa Goguryeo pamoja na mtoto wake Yuri. Hii naikubali zaidi hata ya Jumong yaani kwenye hii drama Song il guk alitisha.
3. Hotel Del luna. Hii nimeimaliza wiki moja iliyopita. Binafsi mimi ni mpenzi wa movies, series na drama za adventure, fantasy au thriller pia napenda drama zenye story yenye kuumiza kichwa kama Kill me heal me na King Eternal Monarch.
Kwenye hii drama kilichonivutia zaidi ni story yake inayomuelezea bi dada Manweol mmiliki wa guest house of the moon na tragedy iliotokea hapo zamani kati yake na Chung Myung iliyopelekea yeye kuwa tied down kwenye Guest house of the moon kwa takribami miaka 1000. Ndani ya hii drama utamuona mtaalam Ku Chan Song pamoja na wa wafanyakazi wengine wa Guest house of the moon. Pia plot twist kati ya Chung Myung na Manweol ilinivutia zaidi pia ilinisikitisha but all in all nilipenda jinsi ilivoisha japo hawakumtendea haki Chung Myung ila ilikua na happy ending.
Kingine OST zake murua kama "Can you see my heart" ya Heinze pamoja na "Done for me" ya Punch...hizi ziliinogesha zaidi hii drama...Hawa wakorea wanajua sana kwenye uandishi wa hizi drama zao sijui lini wabongo tutafikia level hizi.
Honourable mentions: Hapa zinaingia Jumong, Kill me heal me, Queen Seondeok,Iris I,Arthdal Chronicles, Iljmae na Goblin.
Pia honourable mention iende kwa Mr Sunshine...katika drama zote nilizowahi angalia zenye sad ending hii ni ya pili ya kwanza ni Empress Ki. Hizi drama mbili zilijua kunisikitisha aisee.
Hio ndio list ya drama za kikorea nilizoangalia mpaka sasa na nikazikubali zaidi.