Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Nitafanikiwa kurejesha account yangu kweli?

Mkuu Vincenzo Jr naomba nipatie hiyo VPN
Tumia vpn hii 1.1.1.1 inapatikana playstore


Proxy hizi hapa
 
Tumia vpn hii 1.1.1.1 inapatikana playstore


Proxy hizi hapa
Shukran mkuu ngoja nifanye hivyo.
 
Ndio Mzee , mimi nilifuatilia YouTube mkasa mzima wa Mwanangu Consigliere Song Joon Ki , nicheze kama Nifah nikupe udaku ...

Baada ya kutoa Descendants jamaa wakapata tuzo nyingi kwenye tuzo maarufu kubwa Korea za "KBS " kama sikosei wakapata tuzo ya "best couple" of the year kwenye Drama ya Descendants. Baada ya hapo fans wakawa Wana push na kutamani wawe wapenzi kweli wakisema kwenye ile movie couple Yao ilinoga na itakuwa dharau kama watamua watengane bila kudate kweli.

Mahaba yalianza usiku wa tuzo , mwamba wakati wa kuchukua tuzo alikuwa anamtaja kwa hisia Kali sana yule manzi doctor SHK kwamba yeye kamsadia sana kwenye ile series maana kutokana na kutokuwa mzoefu sana alikuwa anapata ugumu manzi ndio alikuwa anampetipeti na kumpa moyo wakati mwingine alikuwa analia mbele yake demu anamfuta machoki Kamanda , kiufupi mwamba alikuwa akideka na manzi aliplay part yake vizuri ndio maana chemistry ikawa hot 🔥 🔥 mpaka kwenye scenes....

Baada ya event ya tuzo tetesi zikazidi kushika Kasi lakini mwamba akawa anakataa kwenye media mwisho wa picha akaona si kweli chap akavuta jiko na Kufunga ndoa nae rasmi..

Baadae kukaja tetesi kuwa hawapo vizuri mwamba akakanusha kuwa wanaendelea vizuri ana enjoy baadae hakukaa sana jamaa akafanya umafia talaka alifuatilia na kuandaa kimya kimya alimuacha juu kwa juu bila kumpa taarifa yaani Manzi aliona taarifa mitandaoni kama kashaachwa jambo ambalo fans hawakupenda na ikamuumiza sana Manzi.

Mwamba akazidi kuwakera Raia alipotoka hadharani na kumsagia kunguni Manzi na kuanika sababu za kuachana na mabaya yake kwenye media huku mwenzake akiwa kimya mda wote na mwamba alidai kuwa Mwanamke hajali mambo ya ndoa na ushirikiano na wazazi wake muda wote busy na anajali mambo , akawa anadai alikuwa anaishi kama haishi kwenye ndoa na safari za manzi zimekuwa nyingi.
Kaka upewe kitengo WBC😃😃
 
Baada ya kuachana na drama zilizoendelea kati yao Wakorea walikasirishwa na Mwamba Joong Ki kwa kuona kamuacha mwenzie kiholela na kuanza kumsema kwenye media badala ya kukaa kimya wakati mwenzie alikuwa amenyamaza .

Matokeo yako jamaa movies zake zikizofuatilia zile Hopeless , My name is ... waliziboycut wakawa hawazitazami na mauzo yakashuka pakubwa huku wakimsagia kunguni kwa comments mbovu mitandaoni na reviews za movies zake akawa na flop ya hali ya juu kabla ya kuibuka tena kwenye makali na series "Vincenzo" na " Reborn Rich" baada ya hapo zilizokuja movies " Bogota City" na nyingine zika flop tena .

Sasa ameoa mwingizaji huko Ulaya na ana mtoto mmoja ila wengi wanaona alijiharibia carrier yake na jinsi alivyodili na suala lake la ndoa .
Alafu ndo mwamba wako unamkubali kwel😃😃
 
Alafu ndo mwamba wako unamkubali kwel😃😃
Mwamba alizingua , hakutaka kuvunga ila ndio hivyo ukiwa superstar lazima ulizwe kwa nini mmeachana sasa Mwamba kajisafisha yeye huku roba la misumari kamuachia manzi .

Manzi series yake ya kwanza baada ya sakata la ndoa ilivynja rekodi viewers wengi na alapata na tuzo , support kwa manzi imeongezeka .

Ilihuzunisha tukio la uzinduzi wa series mwandishi wa habari alimuuliza kuhusu ndoa yao akasema "kwa Nini mmeachana mapema wakati mlikuwa mnaoneka ni watu Wenye furaha na couple nzuri na vipi kuhusu tuhuma za kwamba wewe ndio chanzo" Manzi akashindwa kuendelea na press akawa analia tu akashindwa kujibu akaondoka akarudi baadae na kumoumba radhi mwandishi wa habari na kusema sakata la ndoa limemfanya asiwe sawa Kisaikolojia muda mwingi alikuwa na stress na akikumbuka yalitokea anashindwa kujizuia.
 
Alafu ndo mwamba wako unamkubali kwel😃😃
Anapiga kazi chafu kwenye hisia yupo vizuri , kwenye usiriaz , uchangamfu nk halafu muonekano unambeba , Hana tu Martial skills kwenye mkono hawezi kabisa ana bahatisha na kupigana kivivu.

Mara ya kwanza nilimuona kwenye Arthdal Chronicles 1 nikadhani underground kumbe mkongwe
 
Back
Top Bottom