Ndio Mzee , mimi nilifuatilia YouTube mkasa mzima wa Mwanangu Consigliere Song Joon Ki , nicheze kama
Nifah nikupe udaku ...
Baada ya kutoa Descendants jamaa wakapata tuzo nyingi kwenye tuzo maarufu kubwa Korea za "KBS " kama sikosei wakapata tuzo ya "best couple" of the year kwenye Drama ya Descendants. Baada ya hapo fans wakawa Wana push na kutamani wawe wapenzi kweli wakisema kwenye ile movie couple Yao ilinoga na itakuwa dharau kama watamua watengane bila kudate kweli.
Mahaba yalianza usiku wa tuzo , mwamba wakati wa kuchukua tuzo alikuwa anamtaja kwa hisia Kali sana yule manzi doctor SHK kwamba yeye kamsadia sana kwenye ile series maana kutokana na kutokuwa mzoefu sana alikuwa anapata ugumu manzi ndio alikuwa anampetipeti na kumpa moyo wakati mwingine alikuwa analia mbele yake demu anamfuta machoki Kamanda , kiufupi mwamba alikuwa akideka na manzi aliplay part yake vizuri ndio maana chemistry ikawa hot 🔥 🔥 mpaka kwenye scenes....
Baada ya event ya tuzo tetesi zikazidi kushika Kasi lakini mwamba akawa anakataa kwenye media mwisho wa picha akaona si kweli chap akavuta jiko na Kufunga ndoa nae rasmi..
Baadae kukaja tetesi kuwa hawapo vizuri mwamba akakanusha kuwa wanaendelea vizuri ana enjoy baadae hakukaa sana jamaa akafanya umafia talaka alifuatilia na kuandaa kimya kimya alimuacha juu kwa juu bila kumpa taarifa yaani Manzi aliona taarifa mitandaoni kama kashaachwa jambo ambalo fans hawakupenda na ikamuumiza sana Manzi.
Mwamba akazidi kuwakera Raia alipotoka hadharani na kumsagia kunguni Manzi na kuanika sababu za kuachana na mabaya yake kwenye media huku mwenzake akiwa kimya mda wote na mwamba alidai kuwa Mwanamke hajali mambo ya ndoa na ushirikiano na wazazi wake muda wote busy na anajali mambo , akawa anadai alikuwa anaishi kama haishi kwenye ndoa na safari za manzi zimekuwa nyingi.