ni takribani miaka 5 tokea nianze kuwa mnywaji wa pombe kali ya korean drama na kadri ninavyoendelea kunywa cha kushangaza satisfaction inaongezeka tofauti na jinsi wachumi wanavyotuaminisha kama kadri unapo consume na satisfaction inapungua.
nahisi umefika wakati wa
Damushin kupunguza au kuacha kabisa kunywa ulevi huu mkali ili kuendelea kudumisha afya yake, hivyo basi
- kuanzia wiki ijayo akipenda Mungu nitakuwa nakunywa pombe chupa moja tu yenye ujazo kama wa chupa ya kahawa, naamini hii ni njia ya kwanza itakayonifanya nipunguze ulevi.
- nitapunguza kutembelea baadhi ya bar zinazotoa huduma ya ulevi pendwa bila ya malipo yoyote, miongoni mwa bar ninazopenda kuzitembelea ni pamoja na dramanice, kissassian,dramacool, kshow, ikshow na bar nyenginezo.
- nitapunguza kutembelea baadhi ya kuta zinazotoa matangazo na taarifa zinazohusu kuzalishwa kwa ulevi mpya ambao tokea nianze kunywa nimeshindwa kuachana nao,miongoni mwa kuta hizo ni pamoja na soompi, reddit,dramabeans,alkpop,soompi forum n.k
- bila ya kuathiri vifungu vya hapo juu nitalazimika kumalizia kreti zangu takribani 40 ambazo nimezihifadhi kwenye store yangu ndipo niache kabisa kunywa ulevi huu pendwa.
- nitalazimika kuwakimbia walevi wenzangu waliokubuhu kwenye ulevi huu kwani hii ndio njia nyengine itakayonisaidia nisipate taarifa zozote kuhusiana na kuzalishwa kwa ulevi mpya, aigoooo walevi wenzangu naomba munisamehe.
- kubadili mfumo mzima wa kimaisha ndani ya nyumba hii kama vile kutokutembelea kabisa chumba hichi cha hatari na vile vile nisipokee simu yoyote yenye lengo la kunishawishi kutembelea chumba hichi.
- je ! haya yote yatawezekana? wakati ambapo ulevi unaoitwa money flower,black knight, hwayugi ndio zinazidi kuninogea
- EMPTY dongsaeng, aminas, mjr95 na walevi wengineo kama mumegundua njia nyengine japo ya asili ya kuacha ulevi huu basi tupeane taarifa.
- hiii pombe ya leo imenifanya niwashwe washwe, niwe frustration na kuishia kutamani kukutana na rais wa korea ya kaskazini mwenye namba yake ya simu aiweke humu ndani.
- mwisho nawaambia walevi wenzangu tuendeleze kunywa ulevi huu wa korean drama hadi hapo wapishi wa ulevi wa bongo movies watakapoweza kutengeneza ulevi wao kwa kiwango cha juu.
- yote haya niliyoyaandika asilimia (x) nipo kwelini na asilimia (y) natania, hivyo basi wale wazee wa betting waje watabiri asilimia x ni ngapi na y ni ngapi, mshindi atapata nafasi ya kwenda joseon